Ladies, let’s do the real talk...

Ni kweli sio lazima uolewe na mtu fukara au kapuku ila alichotaka kuwasilisha nadhani hakijaeleweka kirahisi kwa baadhi ya wachangiaji.

Kwa jinsi nimeelewa ni kuwa alimaanisha ile hadhi na heshima apewayo mwanamke ambaye mmeanza nae from scratch ni tofauti na ile apewayo ambae amekuta everything in place. Hivyo anaekuta mazingira mazuri basi lazima awe na sifa ya ziada ya kuongezea thamani maisha ya yule mwanaume ili apate hadhi sawa na ambaye alichuma nae.

On the other hand, mwanaume kubadilika akipata depends on how you both lived and treated him. Kama ulimdharau na kumsimanga kwamba si lolote si chochote maana hakusaidii kitu wewe ndio kila kitu. Ukimjengea mentality kwamba wewe kuwa nae unamfanyia favor na unajuta hata kuwa nae kimahusiano basi tegemea tu siku mrija wa pesa ukifunguka atakubwaga bila kujiuliza mara 2! Na hili ndio kosa wanawake wengi hufanya bila kujijua ila sie wanaume huwa hatuongei tunauguliaga moyoni tu tukisubiria njia za riziki zifunguke.

Yani huu muda wa msoto ndio huwa una reveal true colors za wanawake tulio nao by 100% kama wako real na sisi au wanajilazimisha tu kwa kutuonea huruma tu iliojaa masimango. Mwanamke mshenzi atakudhalilisha mbele za watu, atakufedhehesha na atlast atakupora kauli yako kama kidume sababu anakupa tuff. Hizi tabia mie lazima nikuache at the end!

Mwanamke wa ukweli ndio anachukuaga point 3 katika kipindi hiki. Yani kuna wanawake wanajua kuziba ma gap ile mbaya. Huwa na heshima full, hawezi kuacha udhalilike na pia hawezi kukunyima sauti kama mwanaume.
Unajua nimegundua wanaume wengi mnataka mwanamke akiwa nacho ilihali mwanaume hana basi mwanamke awe na heshima kama kawaida! Ila mwanaume akiwa nacho ilihali mwanamke hana basi mwanaume anatakiwa amdharau huyo mwanamke sababu kamkuta navyo mwanaume!
 
Hivi kuna tofauti ya kuchepuka huku nafsi inakusuta na kuchepuka huku unachekelea?
Si ndio hapo sasa! Kuchepuka ni kuchepuka tu na wanaume wanaochepuka wote wanafurahia ila wanakuja hapa kujifanya nafsi zinawasuta na huku wanaendelea sasa kwanini wasiache?
 
Zama hizi Ukimkuta mwanaume ana kila kitu, jiulize mara tatu tatu, sio rahisi akuoe, mtapoteza muda halafu atakuja kumuoa mwingine kabisaa...either atakaeolewa ana mchango wa namna fulani kwenye mafanikio ya huyo mwanaume

Ila wanawake inabidi wajifunze at some point, maisha ya kuanza pamoja from the scratch ni maisha mazuri na yana bond kubwa sana,hii bond inaletwa na your love history, ups and downs, better and worse, mvua na jua...na pia yanakua na value kwenu wote wawili yaani kila mmoja anaona thamani ya mwenzake, upendo wa kweli na uvumilivu.

Sasa wanawake wengine anabahatika kumpata mwenye kila kitu, akifika yeye kazi yake ni total destruction kwa huyo mwanaume, hana uchungu hata wa mali aliyoikuta, hawazi namna ya kuendeleza pale mwenzake alipoishia, hana mawazo chanya, zaidi anataka kuweka tamaa kwa sababu ya ubinafsi, ndio maana wanaume wanawaogopa sana wanawake, tena wanaume wengi ambao wamefanikiwa na hawajabahatika kuoa, huwa wanaogopa kuoa sijui kwa nini...labda kwa sababu ya hizi tabia

Wadada kama ukimkuta mwenza amejiandaa kimaisha na amekamilika, jaribu ku add value kwenye ulichokikuta, kithamini na uweke mchango wako, acha ubinafsi na tamaa, heshimu mali ulizozikuta at the end of the day Mwanaume nae atakuona una thamani na mchango kwa namna fulani kweye maisha yake
Hii ni sahihi japo kuna kuanza wote maisha kwenye dhiki mnalala kwenye kigodoro kimoja na upside down za hapa na pale, Mara paap mwanzako akatusua akapata shavu mambo ya ubinafsi yakaanza Mara hiki cha kwangu Mara chumba mm ninaelipia kodi,maneno ya kebehi yanaanza mpaka unasema hii sasa mbona sikuiona mwanzo iweje sasa

Mm imenitokea hii nilikua nafanya biashara za tigo pesa baadae mtaji ukafeli, baadae mwenzangu akaja kupewa mtaji na kaka yake akafungua yeye hyo hyo tigo pesa sasa naona mambo yanaenda vizuri mm mambo yangu yamebuma,nyodo sasa ndo zimeongezeka ,ubinafsi ndo usiseme na kitu kinanikeraga sana mtu kua na ubinafsi maneno ya kero kero yaan daaah
 
Back
Top Bottom