Ladha ya Wafalme wa Underground. Nikki Mbishi, One the Incredible na Stereo Singasinga

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,009
9,874
THE UNDERGROUND TASTE WITH
THE BEST TRIO/ TRINITY
SISI THE TRIO
NIKKI MBISHI, ONE THE INCREDIBLE NA STEREO SINGASINGA.

Wachora ramani na wachonga njia ya Rap ya kisasa Bongo iliyojikita katika matumizi sahihi ya midundo ya HIP HOP.

Walimu wazuri na wakuu wa mtindo wa vina mshono ambao unaitwa multisyllabic rhymes.
Walimu wazuri wa matumizi sahihi ya lugha mbili (Kiswahili fasaha na Kiingereza "kizuri"), undoubtedly, the best English spitting MCs.

Waasisi wa familia kubwa ya TAMADUNI MUSIC.
Watu walioifanya Jumamosi ipate umaarufu mkubwa wa pili na upekee baada ya ule uliokuwa umezoeleka kuwa ni siku ya SABATO, sasa Jumamosi ikawa siku ya KILINGE.

Watu sahihi waliokuja kutuaminisha kuwa ili upate heshima kama mwana Hip Hop mkali lazima ufanye kazi na FATHER CHRISTMAS, DUKE GERVALIUS "DUKE TOUCHES"

Watu sahihi waliorudisha mzani Kati ya HIP HOP na BONGO FLEVA msimu wa 2009/2010.
Watu waliosimama na kufanya uzinduzi wa albam zao; SAUTI YA JOGOO, SOGA ZA MZAWA na THE AFRICAN SON kwa kutumia asilimia kubwa ya rasilimali zao wenyewe.

Watu waliorudisha mizuka ya wana kufanya album ili kupata heshima ya ki- Hip Hop na kuondokana na kasumba ya mkondo mkuu ya kuachia ngoma moja na kuiuza na kufanyia maonesho.

Watu sahihi zaidi waliokuja kuwaelimisha wengi kuhusu utofauti kati ya Bongo Fleva na Hip Hop lakini baada ya kutengana na uongozi wa M Lab, hawa ndiyo waliotoa dhana sahihi ya independent artists.

Kama tulikubaliana kuwa UWILI BORA NI ULE WA DOMO NA DOJO, BILA SHAKA TUNAKUBALIANA KUWA UTATU BORA BONGO NI HUU WA HAWA WATU WATATU.
THE IMPECCABLE
CLASSIC MATERIAL
HISIA
SISI THE TRIO
Ndiyo ngoma ambazo walizitoa kwa pamoja ukiachana na zile ambazo walifanya na members wengine wa TM.

BINAFSI, NIMEVUNA ELIMU YA KUTOSHA KUTOKA KWA HAWA WATU.
HESHIMA SANA KWA TAMADUNI
BROTHER PATRICK GONDWE
NA WANA WOTE WALIOKIWASHA PANDE ZA MSASANI.
HATA ISIPOJIRUDIA, HISTORIA ILISHAANDIKWA.
 
Nikki Mbishi & Stereo - TamaNgumi

Hii ngoma naikubari saana ukiacha ile Swahili na African Son

Cheza kila gemu Ila usicheze bila nguo/
Bongo Fleva ni km Demu yule mliekutana Chuo/
 
Mwamba uliishi historia, btw movement ilikua kubwa sana na athari zake ziliweza kugusa karibia kila kona ya nchi hii, vijana tuliskiza, tukajifunza na kutoa tongotongo
 
Nipo Poa Aiseee Ukiuona Duke mpe Bapa Aisee ,Kila Dress code inakaa mazee ni sawa kuwa na case 1st degree murder king zilla in da house salasala we go harder nipo na texas yes hes my broda.

Wasananii wanauza sura cd dukani kina dada wanaigiza ulokole miili buchani - B-Boy stereo
 
Mwamba uliishi historia, btw movement ilikua kubwa sana na athari zake ziliweza kugusa karibia kila kona ya nchi hii, vijana tuliskiza, tukajifunza na kutoa tongotongo
Kitambo sana, kipindi hiko album moja 5k
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom