labda upole na ufahamu wetu ndio unatutesa

JUKUMU

Member
Apr 5, 2009
76
125
Wana Jf niseme kwamba hali ilivyo sasa si nzuri kwa watu wengi, ila kwa upande mwingine watanzania kwa ujumla wetu tunaweza kuomba kukutana na mkuu wetu asikie kilio cha wengi kama alivyokuwa anaomba kura wakati wa kampeni.

Alitoa ahadi nzuri na wengine tukasema mkombozi kaja, ila hali imekuwa tofauti kwa watu wengi. Kuna vitu ambavyo kwa kweli havitakiwi kuwa juu kama ilivyo sasa, mfano sukari, unga na vyakula kwa ujumla.

kwenye biashara kila mfanyabiashara anajua yanayomsibu, walioko kwenye ajira nao wanakilio chao. Sasa mimi nakosa majibu ninapojiuliza kwani watanzania hatujui kuhoji pale bei zinapopanda kila kukicha? Je haturuhusiwi kuhoji sera za chama na ahadi zake? Je watetezi na wale wanaharakati wamepotelea wapi? Tunambiwa uchumi uko imara, sasa huo uimara ni kwa kigezo gani? yaani mtu unakaa kwenye biashara yako inabidi ujiungishe mwenyewe kama unauza vinywaji unywe hata kachupa chochote ili uhisi umeuza. Kazi tunafanya lakini kwa hali ilivyo sasa ni wachache wanapata unafuu.

Mkuu wetu naomba utusikilize watanzania wenzako huku kwetu kugumu, kila siku bora ya jana...watanzania kwa ujumla ni watu wasikivu, wapole na wanafuata sheria, tafadhali tupunguzie huu mzigo wa maisha.
 
Ulongupanjala

JF-Expert Member
Apr 9, 2013
3,353
2,000

Hii elimu na malamiko yako nakushauri,print halafu nenda kijijini kwako ukawape wasome,pia usisahau kupita vijiji jirani nao waone maudhui ya andiko lako huenda 2020 wakabadilika,ila hapa JF kila MTU mjuaji!
Ni ushauri tu mkuu!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom