Labda mnielimishe nyie, sioni faida ya paka ambae mke anamgharamia sana bila faida

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,032
1612786471342.png

MUHIMU: PICHA HII SIO YA PAKA WA HAPA KWETU

Hapa kwangu napoishi tuna paka, Sio mimi niliemleta bali ni mke wangu.

Hatuna tatizo la panya kwa hio bado sielewi paka anahitajika wa nini.

Kuna jirani ana fuga ngombe huwa anatuuzia maziwa nyumba chache, Mke wangu alilipia ujazo wa ziada alipomleta huyu paka wake ili anywe nae maziwa, huwa aakunywa kila asubuhi na jioni, huu ni ufujaji wa pesa.

Kila mara 2 kwa wiki lazima mke wangu amletee paka samaki, huwa naumia sana kuna paka anagharamiwa wakati hakuna kitu anachofanya, kuna watu wana njaa mitaani her wao wangepewa.

Muda mwingi huyu paka huwa kasinzia na kunenepa tu, anaweza kulala juu ya friji, kwenye kochi, n.k

Huwa sitaki kabisa awe karibu na mimi ila cha ajabu ni kama analazimisha nimzoee huwa anapenda kujipitisha miguuni badala ya kwenda kwa wanaopendaga kumchezea.

Faida pekee ambayo mke wangu anaisema ni kwamba kamfundisha kujisaidia kwenye ka box kake na huwa anamuogesha kila wiki, sasa hii ni faida gani?
 
paka mzuri sana anaonekana anapata kweli raha ndomana yuko ivo miguu juu...love cat
 
Paka wa hivyo akiona mjusi tu anatoka nduki mpk miguuni kwa mkeo afu ndio anaanza kulia nyauuuuuuu,nyauuuuuuuu
 
Mkuu mi nakushauri tegea siku ametoka. Mfunge huyo paka kwenye kiroba (maana wanasemaga wakiona njia wanarudi) nenda naye mbali Kisha mfungue halafu mtelekeze huko. Ukirudi kausha kama hakijatokea kitu.
 
Back
Top Bottom