Ndugu yangu wa Kiume anaoga baada ya siku mbili, maji yapo ya kutosha. Hii ni kawaida?

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,032
Wadau huenda labda Mimi ni mshamba.

Kuna ndugu kaja hapa home, sasa inapokuja suala la kuoga Mimi ninachojua inabidi uoge mara moja kwa ila ndugu naona utaratibu wake ni hadi siku mbili zipite

Mkoa nilipo ni Mbeya, kwa sasa hali ya hewa kuna jua kali kiaina japo mvua ni hizi zinanyesha mara 2 kwa wiki.

Maji ya bomba sio tatizo kabisa , pia jikoni kuna lile dude la kuweka mkaa kupasha maji, maji ya moto sio tatizo.

Je, ni kawaida?
 
Wadau huenda labda mimi ni mshamba.

Kuna ndugu kaja hapa home, sasa inapokuja suala la kuoga mimi nachojua inabidi uoge walau kila asubuhi ila ndugu naona utaratibu wake ni hadi siku 2 zipite

Je, ni kawaida?
Kama yupo peke yake na shughuli zake(binafsi - kuuza duka) sio za kutoka jasho hata wiki unakaa tu fresh.
 
Mkuu umezingatia jasho la kwapa na kwenye msitu wa kati linavyoweza kusumbua wengine??
kila mtu ana jasho lake mkuu, kuna wengine wana jasho kali na kuna wengine wapo kawaida tu.
Hilo la kuoga inategemea mnapoishi, sehemu zenye baridi kali watu washazoea hizo issue ila sehemu za pwani kuna joto sana na kupitisha siku bila kuoga hasa joto likichanganya ni issue
 
Kuna mpaka wanawake...anapendeza sana ila ..siku 2..naa..hakogi na hujui..
kuoga sana kuna punguza vitu asili kwenye mwili...argh!
 
Wadau huenda labda mimi ni mshamba.

Kuna ndugu kaja hapa home, sasa inapokuja suala la kuoga mimi nachojua inabidi uoge walau kila asubuhi ila ndugu naona utaratibu wake ni hadi siku 2 zipite

Je, ni kawaida?


Wewe umepata wapi kwamba mtu anatakiwa walau aoge kila asubuhi??
 
Back
Top Bottom