Toosweet
JF-Expert Member
- May 27, 2012
- 2,141
- 1,982
Kwenu,
Tunaomboleza bado. Ni siku ya mwisho.
Kila Mtanzania anaona kwamba urais wa nchi yetu unakwenda kwa zamu,;Mkristo-Mwislamu, Muislamu-Mkristo. Jambo hill halifanyiki kwa kuwa ni utaratibu ulioandikwa mahali, hapana. Ni 'uungwana' wa kuachiana kijiti ili kupunguza manung'uniko kuwa upande mmoja unapedelewa na mfumo. CCM ndiyo waasisi na hakuna aliyepinga.
Wakati wa uhai wake, Mwalimu Nyerere aliwahi kusemea jambo hili kwa tahadhari. Inakuwaje katika kuachiana, upande wenye zamu ukikosa mtu makini,lakini akalazimika kugombea ili kusiwe na kelele? Tutapata rais bomu. Hii ni true zaidi kwa upande wa CCM.
Kwa upande mwingine, kwa kuwa utaratibu huu ni wa 'kiungwana', haujapingwa na Watanzania, aghalabu kwa wazi, hata opposition parties(CHADEMA na labda CUF bara)wanaweza kuu-adopt.
Je, inawezekana Chama cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA, wanapanga kumsimamisha Maalim Seif Sharrif Hamad, Katibu Mkuu wa CUF kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020?
Ziko habari kuwa CHADEMA wanapanga kumwalika Maalim Seif kuja upande wao. Bado maombi rasmi hayajatumwa, wala Maalim Seif mwenyewe kutangaza kuridhia.
Kwa sasa Rais ni John Magufuli, Mkristo.
Labda plan hii inaweza kuwavutia waumini ambao ni sensitive linapokuja suala la imani na kiongozi wa nchi. Ni mtazamo tu. Just trying to think loud. No hard feelings.