GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 59,949
- 119,212
Kweli sasa nimeamini kuwa hata umfanyie nini Binadamu mwenzio ambaye pengine wakati wa mateso hayo unayompa wala hakuwa na jambo lolote lile baya ila Wewe tu kwa chuki zako au kwa maelekezo ' maalum ' uliyopewa ama hakika ipo siku tu yale ' machungu ' na ' maumivu ' yake Mwenyezi Mungu atayabadilisha kuwa ' laana ' kubwa sana ama Kwako binafsi au kule ambako hao Watu wabaya wametokea.
Na siku zote ' laana ' za walioteswa, kupigwa, kunyanyaswa na hata kuuliwa Mwenyezi Mungu huzisikiliza haraka na kutoa majibu ya upesi mno ambayo huwa na athari au madhara makubwa tena pengine hata kushinda yale ambayo ' wahanga ' au ' wahusika ' walifanyiwa.
Binadamu tukumbuke tu kuwa hapa duniani tujikite sana katika kuheshimiana, kupendana na kusaidiana pale tunapokuwa na matatizo na hata siku moja usije kudhani kuwa utamfanyia fulani jambo baya la kumuumiza au kumuangamiza kabisa halafu Mwenyezi Mungu asimjibie mapigo.
Ben Saanane sijui ulipo kwa sasa ila kama umeshatangulia mbele ya haki basi jua ya kwamba yale ' maumivu ' yako uliyoyapata hadi ukafika huko ' ahera ' ulipo sasa majibu yake tunayaona na ambayo Roma Mkatoliki nae ameyazidisha hasa kutokana na aliyotendewa yeye na wenzake.
Mnaojijua kabisa kuwa mlishiriki katika kuwafanyia ' Ukatili ' hawa Watanzania wenzetu nadhani huu ni wakati wenu muafaka kabisa wa kumpigia Mwenyezi Mungu magoti, kukiri makosa na kumuomba msamaha kwani yawezekana haya tunayaoyashuhudia sasa ikawa ni ' laana ' kali za waliofanyiwa huo ' Ukatili ' hivyo Maulana ameamua kuwajibia.
Ama hakika ' malipo siku zote ni hapa hapa duniani '.