Laana ya Baba wa Taifa yawatesa J. Kikwete, E. Lowasa na J. Malechela | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Laana ya Baba wa Taifa yawatesa J. Kikwete, E. Lowasa na J. Malechela

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by eedoh05, Apr 23, 2011.

 1. e

  eedoh05 JF-Expert Member

  #1
  Apr 23, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 633
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 45
  Watanzania mnapaswa kuelewa kuwa kinachomsumbua J. Kikwete katika uongozi wake ni laana ya Baba wa Taifa mwl. Nyerere mwaka ulee kina Kikwete, Lowasa walipotaka kuteuliwa wagombea urais kupitia CCM walitolewa maneno ambayo baba yetu hakuyameza na kuyarudisha. Malechela alisodolewa kipindi kileee yeye alipokuwa Waziri Mkuu akiwa kigeugeu juu ya Muungano zama za G55.

  Watu hawa watatu kila wanapotaka kuibuka na kuinuka linatokea la kutokea wanazimika. Ebu, mwanglie Kikwete anadanganywa, aumbuka (alisaini sheria mpya kwa mbwembwe, akambwembweka); amechanganyikiwa, mwaka jana kawaambia watanzania kwamba Monduli na Igunga wawachague Lowasa na Rostam kwamba ni watu saaafi. Leo anawaambia watanzania hao ni mafisadi. (mwl. Nyerere alisema, tunayaona sasa).

  Nimwambie Nape Nauye, kwamba mpendwa wetu mwl. Nyerere alishamwona Kikwete hafai kutuongoza, Lowasa hafai kutuongoza, Malechela halikadharika. Leo wewe unasimama kidete kumtetea na kumwosha Kikwete atakate, mbona humwoshi Lowasa pia? Swali ni hili kati ya wewe na mpendwa wetu, baba yetu mwl Nyerere nani yuko sahihi? TUNAOMBA MKOME KUMFANYA BABA YETU MWL. J.K. NYERERE AONEKANE KUWA ALIKUWA MZUSHI!
   
 2. S

  Simon B james Member

  #2
  Apr 23, 2011
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Duuh nimekubali ujumbe wako. Kweli nape anacheza ngoma asiyo ifahamu. KIKWETE KAMwe hasafishiki. Kwa heri marehemu Ccm
   
 3. G

  GJ Mwanakatwe JF-Expert Member

  #3
  Apr 24, 2011
  Joined: Mar 26, 2011
  Messages: 241
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Viongozi wa tz wakitaka kufanikiwa kiuongozi na nchi kusonga mbele, na kukubaliwa na wananchi ni lazima wafuate nyayo za nyerere kwa dhati ya mioyo yao la hamna kitu.
   
 4. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #4
  Apr 24, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,175
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280
  tanzania haina rais; ila ina mtu anayetaka na yeye aitwe rais.
   
 5. Pasco_jr_ngumi

  Pasco_jr_ngumi JF-Expert Member

  #5
  Apr 24, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 1,811
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Thanks
  nimeelewa sana
  nimeelimika sana
  ingawa naumia...... Nchi niipendayo! Inanuka
   
 6. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #6
  Apr 24, 2011
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,306
  Likes Received: 5,596
  Trophy Points: 280
  Nadhani mtu mmoja tu amebakia kuja kuikomboa hii nchi huyo mtu alishaanza kufundwa na wachina miaka ya 80 kuja kuchukua nchi na akapewa vipaumbele vya kuja kufanya....mkakati wa miaka 30 tungekubali kufuata urafiki wa wachina na chama chao ambao wanatujua nje ndani na siasa zetu na nchi yetu na matatizo yetu....nadhani tusingekuwa hapa...ule mpango kwenda china kwa chama ccm kupata mafunzo na miongozo ingewajenga sana upeo na uzalendo pia!!!wajuzi wanamjua huyo hazina aliepikwa wakati ule na bado ana ethics za uongozi ingawa naomba asije akawa na visasi!!!!ni SAS pekeee atakaeunganisha hii nchi na kuijenga upya!!
   
 7. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #7
  Apr 24, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Nimeshaketi vizuri tayari kukusikiliza kiundani zaidi juu ya maono haya mazito.
   
 8. Dadii

  Dadii Senior Member

  #8
  Apr 24, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 142
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35

  Awamau ya kwanza kuna mema na mabaya tuliyoyafanya tatizo lenu mnachukua mabaya na kuyaendeleza badala ya kuchukua mema.

  Ujinga wa Nyerere akiri ya Kikwete.
   
 9. Avatar

  Avatar JF Gold Member

  #9
  Apr 24, 2011
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 676
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 35
  Umeniacha mkuu!..
   
 10. Silas Haki

  Silas Haki JF-Expert Member

  #10
  Apr 24, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 368
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Heh, what kind of a person is this? Too shame for Tanzanians.
   
 11. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #11
  Apr 24, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  SAS!! Ni kweli?
   
 12. m

  matawi JF-Expert Member

  #12
  Apr 24, 2011
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 2,055
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Mbona una ujuzi mdogo sana wa kufananisha yaani kikwete angefanana na nyerere hata robo tanzani ingekuwa mbali sana
   
 13. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #13
  Apr 24, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145

  Wana JF,
  Mwanzoni nilikaaa nikatafakari sana nikadhani Nape anakwenda swa ila baadae nikuja kugundua huko Nape anapokwenda kuna ulakini esp Tukirudi nyuma wakati wa Mwl. JK Nyerere kuwakosoa Kikwete kuambiwa bado sana na Lowassa aliambiwa kuwa Katibu wa CCM kipindi hicho akasema bado mchanga kisiasa wakati ndipo palikuwa mahali pa kupandia haraka na kuwa rais, Malecela ndi yeye Mwl. alimtegemea kabisa na ndio walikuwa watiifu wa Mwl.nyerere usipime sijui alilogwa wapi na alipo pewa kuwa PM kwa asilimia kubwa ni kufanikisha Serikali kuhamia Dodoma na akashindwa kabisa na kujiingiza na OIC G55 nakumbua, uwanja wa Dodoma Mwal. aliwaambia narudisha kadi ya CCM na katika chumba cha kusubilia cha wageni huku mwl.akisubilia ndege baadhi ya vingozi walitolewa ndani akabakia na M/kit wa CCM Mkoa wa dodoma enzi izo Mr. Pancras Ndejembi kwenye hicho chumba kilicho ongelewa humo ilikuwa ni siri yao na mwalimu hakurudisha kadi which mean huyo mzee aliweka mambo sawa kwa mwl.Nyerere kwani huyo mzee alikuwa mtiifu sana kwa mwl.Nyerere na ndio maana mpaka leo ni wazee wachache walio stahafu CCM na wanao sikilizwa ndani ya Taifa hili kuliko hata Rais Kikwete.

  Narudi kwa Nape kasi aliyo anzanayo ni nzuri ila ina mkubwa kupita uwezo wake kwa njia nyingine usikute anatumika bila kujijua na kama anajijua basi labda anajeshi lake kubwa la UVCCM ambalo sidhano kwa muda huu mchache kama amelijenga au alilijenga zamani lakini bado kuna ulakini kwani UVCCM ndio kuna machafuko makubwa mean kumepasuka kuliko. nataka kumkubusha kuwa Lowassa anabebwa sana na Makanisa kwa taarifa yake na anagenge kubwa nyuma na akitaka kushinda hiyo vita ni kurudi chini kwa wananchi ambaka hiyo kauri mzee ndejembi alishawahi kuitoa na kuwatahadharisha viongozi wa CCM wote kuwa wana CCM walioko chini wametengwa sana nanndio maana CCM yaenda kubaya sasa Nape ndiko anatakiwa aanzie huko na siraha ya kumshinda Lowassa ni kuwamaliza wapambe wake na wako wengi wameisha neemeshwa kwa hali na mali na Lowassa alijijenga kupitia makanisa hawa wakina Askofu Laizer wako nyuma yao. Nape akumbuke JK,Lowassa Rostam still ni kitu kimoja nakama wamekorofishana asithubutu kuingilia ugonvi usio muhusu kwani atakuja potea kuliko maelezo Politics kwa watu hao wakiongozwa na JK mwenyewe alisha wahi sema huko nyuma Politics is dirty game ni kuzungusha maneno hapo tosha kabisa kuamini kuwa Rais tuliye nae ni hakuna hapo ni kupigwa danganya toto.

  Njia nyepesi tu na ya kidemocrasia ni viongozi walio wengi nadni ya CCM waliokaa muda mrefu ni wajibu wao kikatiba ya CCM wapumzike ili kupisha taswila mpya za vijana hapo CCM itaepukika kupasuka kabisa ila kama wananyoosheana vidole imekula kwao nipo hapa nawaambieni.

  Siasa za CCM sasa zimefika wakati zibadilike kabisa ziendane na wakati uliopo na sio za 60's,70's,80's au 90's wakumbuke moto wao ndio walio uanzisha pale chimwaga wanamtandao walipo cheza faulo na kuchakachua mambo ili kuingia IKULU na wakajikuta hawajui kuiongoza nchi
   
 14. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #14
  Apr 24, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Ama kweli tungekuwa mbali sana,

   
 15. e

  eedoh05 JF-Expert Member

  #15
  Apr 24, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 633
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 45
  Soma hapo chini mtanganyika kama alivyofafanua Jethro. Ahsante
   
 16. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #16
  Apr 24, 2011
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 863
  Trophy Points: 280
  Labda useme kuwa hiyo ni laana kwa watanzania wote waliowapa jamaa hawa madaraka. Watanzania ndio wanaoumia sana kutokana na uongozi wa jamaa hawa.
   
Loading...