Laana: Usije ingilia ugomvi wa wazazi hata siku moja

KijanaHuru

JF-Expert Member
Jan 7, 2017
1,822
2,290
Habari ya siku nyingi ndugu zangu, ngoja niende kwenye hoja moja kwa moja

Masuala ya ugomvi na migogoro ya ndoa kwa wazazi wetu ni mambo ambayo huwa tunakumbana nayo mara kwa mara na kwa asilimia kubwa sana japo sio kila familia au kila mtoto huweza kuyapitia haya mambo.

Ila niwape angalizo ndugu zangu katika masuala ya matatizo ya kifamilia ya wazazi usije hata siku moja ukaegemea upande wa mtu mmoja hata kidogo, kubwa unaloweza kulifanya ni kumfariji tu yule aliyeathirika zaidi kuwa na moyo mmoja wakusimama naye na kuhakikisha msongo na kukata tamaa isiwe sehemu yake.

Ukimchukia baba na akajua sababu ya mama au ukimchukia mama akajua sababu ya baba nakuhakikishia ndugu yangu nenda hata kwa mwamposa na shehe unayemjua wewe hii laana itakutafuna sana tena sana utakuwa ni mtu wa hatua mbili mbele tatu nyuma pasipo hata kuwa na suluhisho.

Narudia tena Mzazi awe na kosa au asiwe na kosa ila ukaingilia ugomvi wao ukamchukua mmoja wapo na akakufuta katika akili yake na moyo wake umekwisha kabisa.

HIli suala halina tiba yoyote zaidi ya kwenda kujiungamanisha na mzazi wako tena kabla hajaondoka hapa duniani na kama haujajifungamanisha naye akaondoka katika maisha haya hata ungekuwa mlokole wakuhamisha milima kwa maombi utahusika tu kwenda kutambika kumuomba msamaha mzazi wako.

Ndugu zangu hili suala limekaa kiroho sana namna ambayo huwezi tambua kiwepesi wepesi, laana ya kuingilia ugomvi wa wazazi na mzazi akaju umeegemea upande mmoja na akakukatia tamaa hii laana hakuna kiumbe wakuitoa chini ya jua na ulimwengu mzima zaidi ya mzazi wako,

Lasivyo itaendelea kuwasumbua hadi watoto wako pamoja na wajuu zako,

Na mara nyingi hizi laana zao zikisha kukalia wewe katika maisha hautaona la maana lolote wala hautakuwa na ahueni mahusiano yatakusumbua kama sio mahusiano basi maendeleo itakuwa shida kama sio maendeleo kipato kugumu kama sio kipato kigumu basi ipo sehemu ya muhimu kwako utakwama na hautaweza kujinasua hata kidogo,

Ukienda kuombewa na kuroga kwa waganga utapata ahueni ya mwezi mmoja tu na wala hautapata jibu la moja kwa moja hata siku moja.

Laana Hii ikikuvaa inatoka kwa njia moja tu wewe kwenda kwa mzazi wako ili arudishe moyo wako tena kwa ajili yako.

Sababu kubwa ya laana ya mzazi kuwa na nguvu nikwasababu kiroho kwa hapa duniani wazazi ndio miungu yako , wawe hai wasiwe hai wazazi wako ndio alfa na omega wako hapa duniani,

Siku nyingine nitakuja kueleza aina za laana ambazo wazazi wanaweza kukuachia,
Ukiwa na swali lolote unaweza ukauliza jisikie huru kabisa.

NASISITIZA HAKUNA MTUMISHI WALA SHEHE WALA MUNGU WALA SHETANI ANAYEWEZA KUITOA HII LAANA.

Muwe na jioni njema...!
 
Attachments

  • Untitled.png
    Untitled.png
    86.8 KB · Views: 18
Mouu natambua unachomaanisha, lakini nikupe tu ukweli kwamba kwenye ugomvi wa wazee huwezi kua neutral hata siku moja

Nikupe tu mtano mwepesi, kuna gomvi zinazohusisha kupigana maknde kuchomana visu kuharibiana mali n.k,

Katika vurugu za dizaini hizi ni lazima utakua na upande na ni wazi kwamba utasimama upande wa HAKI bila kujali ni mzazi yupi unamtetea

Kwa kufanya hivyo tu utakua umeingia moja kwa moja kwenye mgogoro ea wazi ama wa siri baina yako na mzazi ambaye hukusimama naye

Itoshe tu kusema kama umeamua kusimama upande wa HAKI basi hakuna laana yoyote inayoweza kuiparamia haki na kufanikiwa NEVER

La mwisho hapa kwenye hili ni kwamba hata kama upande wa HAKI ulioamua kusimama utamgusa mzazi mmoja pekee,

Jaribu kumaintain heshima yako vilevile kwa wote, upendo vilevile n.k na hata ikitokea mmoja unampa salamu hapokei... Wewe endelea tu kumsalimia hivyo hivyo na kumjali hata ipite miaka 50
 
Mwenye sikio na asikie
 
NIkukumbushe tu kuhusu hili ugomvi wa wazazi hauna huyu mwenye haki huyu mwenye makosa,
nakusisitiza tena hakuna mwenye haki ugomvi wa wazazi mtoto unayeweza kumuona,

ndio maana hata siku moja hata kama unaweza kusuluhisha ugomvi wa wazazi ni mwiko hata siku moja kumkalisha chini mzazi mmoja au wote kusuruhisha ni mwiko na haiwezekani hata kidogo.

narudia tena ndugu ugomvi wa wazazi mtoto haumuhusu hata kidogo, unaloweza kulifanya nikuwa mfariji tu ila usijaribu hata kidogo kujaribu kusema huyu ana haki au hana haki,

sheria za ulimwengu hazilitambui hilo la mzazi mwenye haki ama asiyekuwa na haki sheria za ulimwengu zinatambua mtoto hupaswi kujihusisha na ugomvi wa wazazi.

pia kwa ziada ugomvi wa wazazi haujakaa kimwili hukumu zake kama unavyofikiria utamuona nani ana haki nani hana haki,

mbaya sana mzazi akajifanya mjinga na akakubaliana na kauli zako akakusikiliza, lakini ndani ya moyo akasema huyu mtoto leo anajifanya mkubwa wakunikanya mimi,
yaani unacheka na mzazi afu kumbe moyon kakukunjia ogopa sana tena sana ndugu yangu ni hatari mno.

nisikuchoshe na maelezo mengi ila tambua tu hauna uhakimu wowote katika kesi ya wazazi wala hauna hata asilimia ya 000000000.00001 kuingilia mgogoro huo, usije kujaribu kamwe ndugu yangu
 
Kuna wakati unaona kabisa mzazi fulani anakosea, je ni vibaya kumwambia anakosea?
Mfano kuna mzee alioa akaingia mgogoro mkubwa na mke wake wa kwanza, akawa anamfukuza kwake kisa ana bibi mdogo, kijana wa yule mama akaona mamaake anateseka anatanga tanga, akaamua kumjengea mamaake mbali kidogo na kwa mzee lakini mzee bado akawa anaenda kumpiga na kumfukuza, hapo napo uwe neutral au mpaka usubiri mmoja afe?
 
Wazee wengine wanazingua mi mzee wangu alinunua kiwanja akaanza msingi alichukua mkopo mara kaacha kujenga ananunua vitu anapaleka kijijini kwao huku town nyumba ya kupanga bahati mbaya zaidi kijijini Kuna ndugu shazi mjini anao wengine analelea kule ajenge huku umaskini unazidi wamezaliwa 12 ataweza kweli ye ndo wa kwanza maendeleo hamna wenzie aliyokuwa anafanya nao kazi wanashusha mijengo

Unadhani Kuna mwanamke fala ataweza kuvumilia lazima aondoke maendeleo hamna miaka 15 kazin wengine Wana nyumba mpaka 3
 
Mzazi hakoseagi kwa mtoto utabaki kuwa mtoto milele na mara nyingi usipende kubishana na mzazi au ukafikia hatua ya kumnyooshea kidogo Kuna mifano mingi tunaiona kwenye jamii tunayoishi na laana ya mzazi ni mbaya Sana na huwezi ukafanya jambo likaenda na mwisho wake ni kifo Mimi Kuna mdogo wangu alimtukana baba alichomwambia ni Siri bt mdogo wangu tumeshamzika na tumeshamsahau kwenye maandiko yametuambia waheshimu baba na mama yako ili siku zako zipate kuwa nyingi kwa nchi upewayo na mwana mungu wako
 
... lile tendo la baba kukojoa mbegu mama akazipokea kwa raha zao ukazaliwa wewe ni tendo la ajabu sana. Kaa mbali na ugomvi wa wazazi.

Kwa wale wa imani wanasema ni katika tendo hili Mungu ameshirikisha viumbe wake katika kazi yake ya uumbaji.
 
Mzazi hakoseagi kwa mtoto utabaki kuwa mtoto milele na mara nyingi usipende kubishana na mzazi au ukafikia hatua ya kumnyooshea kidogo Kuna mifano mingi tunaiona kwenye jamii tunayoishi na laana ya mzazi ni mbaya Sana na huwezi ukafanya jambo likaenda na mwisho wake ni kifo Mimi Kuna mdogo wangu alimtukana baba alichomwambia ni Siri bt mdogo wangu tumeshamzika na tumeshamsahau kwenye maandiko yametuambia waheshimu baba na mama yako ili siku zako zipate kuwa nyingi kwa nchi upewayo na mwana mungu wako
well said ndugu yaani hilo halina mzani hata kidogo wala mbadala
 
Kuna wakati unaona kabisa mzazi fulani anakosea, je ni vibaya kumwambia anakosea?
Mfano kuna mzee alioa akaingia mgogoro mkubwa na mke wake wa kwanza, akawa anamfukuza kwake kisa ana bibi mdogo, kijana wa yule mama akaona mamaake anateseka anatanga tanga, akaamua kumjengea mamaake mbali kidogo na kwa mzee lakini mzee bado akawa anaenda kumpiga na kumfukuza, hapo napo uwe neutral au mpaka usubiri mmoja afe?
nikweli mkuu umeuliza swali sahihi sana na lenye kujenga sana
ila ugomvi wa wazazi haijarishi mmoja kaonewa kwa namna gani mtoto hauna hata asilimia sifuri yakushauri au kuingilia,
jambo pekee la busara unaloweza kufanya nikufuata wazee wenye busara na hekima kuwaeleza juu ya ugomvi huo japo hapa unaweza wafuata hao ikiwa akina babu na bibi wapo mbali, maana tunasema ni mwiko kutoa siri za ndani,

nimewahi shuhudia watoto wamepeleka mashitaka kwa babu na juu ya tabia ya mama jibu la babu lilikuwa ni kabebeni nguo nyumbani kwenu hamieni kwangu kwa muda.

hivyo anza na wazazi husika wa wazazi wa wazazi wako kuwaeleza ila narudia tena mkuu MZAZI HAKOSEI KWA MTOTO HIYO NI ASILI HUWEZI LAZIMISHA MAJI KUPANDA MLIMA HATA SIKU MOJA, KAA MBALI KABISA NA UGOMVI WA WAZAZI MAILI ELFU KUMI.
 
Wazee wengine wanazingua mi mzee wangu alinunua kiwanja akaanza msingi alichukua mkopo mara kaacha kujenga ananunua vitu anapaleka kijijini kwao huku town nyumba ya kupanga bahati mbaya zaidi kijijini Kuna ndugu shazi mjini anao wengine analelea kule ajenge huku umaskini unazidi wamezaliwa 12 ataweza kweli ye ndo wa kwanza maendeleo hamna wenzie aliyokuwa anafanya nao kazi wanashusha mijengo

Unadhani Kuna mwanamke fala ataweza kuvumilia lazima aondoke maendeleo hamna miaka 15 kazin wengine Wana nyumba mpaka 3
Mzazi hakosei kwa mtoto hilo weka akilini haijarishi unayaona makosa kwa kiwango cha namna gani,
ukiona imeshindikana kabisa kuvumilia peleka mashitaka kwa wazazi wao, wao binafsi ndio watayajenga na watajua ni ni namna gani ya kuliweka sawa.

ila katika yote unaloweza kulifanya nikuwa mfariji tu kwa mzazi anayeonewa wala sio kuwa mshauri namna yakumaliza mgogoro wewe nikuwa mfariji tu baaaasi,

Ulimwengu umeweka sheria zake na kanuni zake mzazi hawezi kosea hata siku moja, mtoto ukiona mzazi anakosea kaa nalo moyoni usiingilie ugomvi hata kidogo,
labda nikusisitize kwa kauli hii NI MWIKO MTOTO KUINGILIA UGOMVI WA WAZAZI, NI KOSA KUBWA SANA TENA SANA MTOTO KUINGILIA KOSA LA WAZAZI, ACHA KABISA HILO NI BOMU LA NYUKLIA KABISA MKUU.
 
Back
Top Bottom