Laana na mikosi inayotokana na zinaa, hii kitu ina uhalisia?

Mzee baba hebu acha hizo ramli chonganishi
hakuna cha laana, mikosi wala mizuka hebu acha kutisha watu

Ikumbukwe unapokua deep in love mtu hutumia muda mwingi kuwaza mapenzi halikadhalika pesa nayo hutumika hivyo kama hatokuamakini wa kubalance kati ya shughuli ya kumwingizia kipato na mapenzi lazma itakucost tu

Nashauri tufanye vitu kwa kiasi
 
Kiasi chako wewe si sawa na Cha mtu mwingine.
Mkuu Usibishe, Kuna ndugu wametoa practical experience zao juu ya ubaya wa tendo Hilo hasa Kama litafanywa bila uangalifu.
Hili jambo la Imani, waweza kuamini au hapana.
Uzinzi unapunguza umakini pia.
 
Nimekupata mzee elimu yako imefanya kazi
Wanadamu tumepangiwa vipawa/karama mbali mbali tangu tukiwa wadogo,vipawa hivi vinaweza kuchafuka kutokana na matendo machafu ya kidunia ayatendayo mhusika.
Uzinzi au uasherati ni moja kati ya vitu vikubwa na rahisi vinavyoweza kuchafua nyota au kibali cha mtu,

Watu wanatembea sehemu mbali mbali na wanatenda mambo mengi mazuri kwa mabaya,sasa unapokuja kukutana na mtu ambaye mwili wake tayari umeshachafuka na ukafanya nae uzinzi tayari na wewe unakuachia vitu vyake ,nuksi mikosi na mabalaa aliyonayo munayashare wote

Tendo la ndoa huhusisha mwili na roho pia,makutano hayo ya wawili huwa ni makubaliano ya kiroho na mwili ndio mana kuivaa mikosi ya mtu ni kitu cha kawaida tu.

Wewe jifikirie mtu katoka kwa mganga na kaelezwa akakutane na mwanamke yeyote alale nae,kachanjwa machale na ndumba za kutosha,anatoka pale anaenda kwa kahaba,anamtangazia dau,anafanya yote anayojua kwa kahaba huyo.
Kisha na wewe unaenda kwa kahaba huyo huyo unalala nae ,unazani utakuwa salama?,hiyo mikosi yote aliyoachiwa kahaba na wewe unaivaa,

Haya mambo unaweza ukachukulia poa poa lakini huwa yanatesa sana watu.
Ndo maana hata vitabu vya dini vinapiga vita sana uzinzi,si kwa sababu ya kuonewa wivu kwa huo utamu,hapana,ni kutokana na tendo lenyewe adhimu lilivyo na mambo yanayoendana nalo,

Kuna watu waovu,wanamashetani,maruhani ya kutosha na wanamikosi na nuksi za kutosha hata ndege wa angani huwa wanawazomea wakipita,kuna watu hata akipita kwako mchana kweupe lakini utasikia anabwekewa na mbwa wako,hawafai ,hawana jambo linalowaendea sawa ,kila kukicha wao na waganga ,kila kukicha wanalazwa makabulini harafu leo unakuja na tamaa zako unachomeka dudu yako na inazama kabsa unaenjoy ,mmmh! Nakwambia hutatokapo salama,si mwanamke si mwanaume hiyo mikosi ipo pote na watu wanatembea nayo.

Wewe jiulize kwa nini unaenda interview mmoja anachukuliwa na mwingine anaachwa,huenda mmesoma chuo kimoja na taaluma yenu ni moja na viwango vya ufaulu huenda vipo sawa,kuna vitu wanadamu tunavyo vinavyotupa kukubalika mbele za watu au jamii na vyenyewe vinazidiana viwango classes, A to F,
Waswahili ndo huita nyota ,mimi ninakiita kibali,hiki kikikosekana ndo pale mtu anakuwa mtu wa kuonekana hana mana katika jamii,anakuwa ni mtu wa kupuuzwa tu,hata ukijaribu kuongea unashangaa anatokea mtu anatoa kejeri kwako na huenda ulikuwa na point nzuri tu.
Haijalishi uwe na elimu au usiwe na elimu,kibali kikikosekana ni shida katika maisha,utazunguka kuomba kazi hupati,utatafuta pesa usiku na mchana utatoka kapa tu.utasemesha mrembo balabalani lakini atakuignore kana kwamba anakujua mpka unapo lala ,kumbe waaala, ndo mmekutana

Tena waogope sana wadada wanaojiuza ,hao nuksi kwao huwa ni zakufikia,wanakutana na watu kutoka machimboni wameoga madawa na kuambiwa wakalale na wanawake, yani yale mabalaa wakawaachie,

Unakuta katoto miaka 16-18 kanajiuza kakipewa 20k jamaa linalala nako usiku kucha na asubui linaenda bafuni linaoga tena madawa linasepa,limekaachia mikosi yote na kubeba hata kidogo kalichonacho matokeo yake hako ka mdada kanakuwa na roho ya kukataliwa hadi uzeeni wake.

Mikosi wazee ipo na pia tuwe tunaangalia na familia za kuoa au kuolewa kuna zingine zina laana ya vizazi,ukijichomeka na wewe unaunga tela utashangaa mambo hayaendi kumbe mwenzako ana roho ya kuanguka na wewe imeshakuvaa hamuwezi kufika mbali .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapa pana ukweli asilimia mia moja. Watoto wa kike wengi wanamajini na mapepo wachafu, hivyo ukitaka mikosi ikuandame wewe fungulia zipu tu, utakiona cha mtema kuni.
 
😂😂😂😂 Acheni ujinga ase
21st Century Kweli...
Ngoja nianze kudoo na mademu clean watoto wa matajiri niambukizwe utajiri ......Kwani Hakuambukizi utajiri..
Kama una Matatizo yako unayo tuu acheni kisingizia watoto wa watu...
 
Kwakweli inasikitisha kuona waswahili walivyo washirikina! Yaani kila kitu lazima kihusishwe na imani fulani.. Ndio maana hatuendelei
 
Hata maandiko yanasema mzinifu hawezi kupata mafanikio,imagine una madem 10 halafu kila dem unamhudumia ww unategemea nin?!,hata kama una maendeleo lazima u drop
 
Unapofanya mapenzi na mtu jua kabisa mnabadilishana roho chafu na nzur, mizimu na laana zote za mabibi mnabadilishana, kama mmoja wenu alikuwa na mikosi inamwandama jua kabisa umeibeba na wew hio mikosi

Tendo la ndoa ni jambo kubwa mno watu siku hizi wamelichukulia kama kiburudisho, mpaka nyuma ya choo wanavuana vyupi

Ndio maana unaweza fanya na mtu leo mapenz ghafla kazin ukaanza kuchukiwa bila sababu, pesa inaanza kuonekana ngumu na inapotea kabisa, mambo yanaenda ovyo mpaka kazi unaweza timuliwa, unabaki unajiuliza tuu bila kujua

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa hiyo ukizini na mtu anayetoka familia tajiri bila shaka nawe unatajirika si ndio maana yake?
 
Wanadamu tumepangiwa vipawa/karama mbali mbali tangu tukiwa wadogo,vipawa hivi vinaweza kuchafuka kutokana na matendo machafu ya kidunia ayatendayo mhusika.
Uzinzi au uasherati ni moja kati ya vitu vikubwa na rahisi vinavyoweza kuchafua nyota au kibali cha mtu,

Watu wanatembea sehemu mbali mbali na wanatenda mambo mengi mazuri kwa mabaya,sasa unapokuja kukutana na mtu ambaye mwili wake tayari umeshachafuka na ukafanya nae uzinzi tayari na wewe unakuachia vitu vyake ,nuksi mikosi na mabalaa aliyonayo munayashare wote

Tendo la ndoa huhusisha mwili na roho pia,makutano hayo ya wawili huwa ni makubaliano ya kiroho na mwili ndio mana kuivaa mikosi ya mtu ni kitu cha kawaida tu.

Wewe jifikirie mtu katoka kwa mganga na kaelezwa akakutane na mwanamke yeyote alale nae,kachanjwa machale na ndumba za kutosha,anatoka pale anaenda kwa kahaba,anamtangazia dau,anafanya yote anayojua kwa kahaba huyo.
Kisha na wewe unaenda kwa kahaba huyo huyo unalala nae ,unazani utakuwa salama?,hiyo mikosi yote aliyoachiwa kahaba na wewe unaivaa,

Haya mambo unaweza ukachukulia poa poa lakini huwa yanatesa sana watu.
Ndo maana hata vitabu vya dini vinapiga vita sana uzinzi,si kwa sababu ya kuonewa wivu kwa huo utamu,hapana,ni kutokana na tendo lenyewe adhimu lilivyo na mambo yanayoendana nalo,

Kuna watu waovu,wanamashetani,maruhani ya kutosha na wanamikosi na nuksi za kutosha hata ndege wa angani huwa wanawazomea wakipita,kuna watu hata akipita kwako mchana kweupe lakini utasikia anabwekewa na mbwa wako,hawafai ,hawana jambo linalowaendea sawa ,kila kukicha wao na waganga ,kila kukicha wanalazwa makabulini harafu leo unakuja na tamaa zako unachomeka dudu yako na inazama kabsa unaenjoy ,mmmh! Nakwambia hutatokapo salama,si mwanamke si mwanaume hiyo mikosi ipo pote na watu wanatembea nayo.

Wewe jiulize kwa nini unaenda interview mmoja anachukuliwa na mwingine anaachwa,huenda mmesoma chuo kimoja na taaluma yenu ni moja na viwango vya ufaulu huenda vipo sawa,kuna vitu wanadamu tunavyo vinavyotupa kukubalika mbele za watu au jamii na vyenyewe vinazidiana viwango classes, A to F,
Waswahili ndo huita nyota ,mimi ninakiita kibali,hiki kikikosekana ndo pale mtu anakuwa mtu wa kuonekana hana mana katika jamii,anakuwa ni mtu wa kupuuzwa tu,hata ukijaribu kuongea unashangaa anatokea mtu anatoa kejeri kwako na huenda ulikuwa na point nzuri tu.
Haijalishi uwe na elimu au usiwe na elimu,kibali kikikosekana ni shida katika maisha,utazunguka kuomba kazi hupati,utatafuta pesa usiku na mchana utatoka kapa tu.utasemesha mrembo balabalani lakini atakuignore kana kwamba anakujua mpka unapo lala ,kumbe waaala, ndo mmekutana

Tena waogope sana wadada wanaojiuza ,hao nuksi kwao huwa ni zakufikia,wanakutana na watu kutoka machimboni wameoga madawa na kuambiwa wakalale na wanawake, yani yale mabalaa wakawaachie,

Unakuta katoto miaka 16-18 kanajiuza kakipewa 20k jamaa linalala nako usiku kucha na asubui linaenda bafuni linaoga tena madawa linasepa,limekaachia mikosi yote na kubeba hata kidogo kalichonacho matokeo yake hako ka mdada kanakuwa na roho ya kukataliwa hadi uzeeni wake.

Mikosi wazee ipo na pia tuwe tunaangalia na familia za kuoa au kuolewa kuna zingine zina laana ya vizazi,ukijichomeka na wewe unaunga tela utashangaa mambo hayaendi kumbe mwenzako ana roho ya kuanguka na wewe imeshakuvaa hamuwezi kufika mbali .

Sent using Jamii Forums mobile app

Ilinitokea iyo nilikutana na m'ke nikiwa form2 nilishangaa nikafeli mtihani hafla.nikamuoa Nikamfungulia duka likaibiwa na cha kushangaza zaidi akiwa mbali na mimi muda mrefu mambo yangu yananyooka.Ni mtihani mkubwa kukutana na mwanmke wa aina hiyo. Mchunguze sana mwanamke katika maisha.hasa kama ulikua uko vizuri kabla ya kukutana nae.
 
Hi ni kama kula mayai ukiwa mjamzito tuliambiwa watoto watazaliwa wakiwa hawana nywele, turejee historia, Mfalme Suleimani na Mfalme Daudi

Kwenye 1 WaFalme 11:1-3, kwa nini Suleiman alikuwa na wake 700 na Masuria 300, kinyume cha amri ya Mungu ya kwenye Kumb 17:17?

Jibu: Kumbukumbu 17:17 inasema mfalme asiwe na wake wengi, na kwa kitendo hicho, Suleiman alifanya dhambi. Kuoa wake ilikuwa ni njia ya kuimarisha ushirikiano na falme nyingine, lakini pia ilikuwa ni makosa kutokumtii Mungu. 1 Fal 11:1-4 inasema kuwa Suleiman alifanya dhambi kwa kuoa hawa wake wageni, na kuugeuzia moyo wake kuwa mbali na Mungu.

Hard Sayings of the Bible uk.229 inalitumia jambo hili kwa njia ya kupendeza sana. Ingawa Suleiman angeweza kuweka viwango vya juu kama mfano, alianza kujiona kama hana haja ya kuzuiliwa na Mungu kwa njia hii. Leo hii kama kiongozi wa kikristo anajiona kuwa hayumo kwenye mipaka ambayo Mungu ameiweka kwa Wakristo wa kawaida, kiongozi huyu atakuwa kwenye shida kubwa sana ya kiroho. Kwenye Kurani, hakuna mwanaume anayeruhusiwa kuwa na zaidi ya wake wanne, isipokuwa Muhammad tu, ambaye alitokea kuwa na wake karibu 24 baada ya Khadija, na Masuria kumi na wawili.
Zaidi ya hayo, Muhammad na Waislam wengine walikuwa na wasichana mateka na watumwa, na Kurani inawaruhusu Waislam kufanya tendo la ndoa na wanawake ambao wanawamiliki kwa nguvu ya mikono yao. (Sura 4:24; 23:5-6; 70:29-30; 33:50,52 Abu Dawud juzuu ya 2 na.2150 uk.577)

Kama tukisoma kwenye BIBLIA, 2 Samweli 11:2-27

Daudi alifanya makosa, alizini na mke wa Uria (Bathsheba) na kumuua mumewe, baadae Bath-sheba alimzaa mfalme Suleman ambaye Biblia inasema Mungu alimpenda sana 2 Samweli 12:24. Na Biblia inasema Mungu anaupenda moyo wa Daudi. Je katika maisha ya Daudi, Mungu alimpangia hayo yote yatokee? Je nini kuhusu watumishi wa Mungu ambao Mungu anawatumia wanafanya dhambi ambazo zi wazi au sirini? Itakua ni mpango wa Mungu?
 
Back
Top Bottom