Laana!Mke aishi na wanaume wawili ndani ya nyumba moja, mmoja ni mume wa ndoa na mwingine ni hawara


MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Messages
39,988
Likes
5,383
Points
280
MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2009
39,988 5,383 280
Laana!! Mke Aishi na wanaume wawili ndani ya Nyumba Moja, Mmoja ni Mume wa Ndoa na Mwingine ni hawara huko Kigogo-Mburahati...!!DUNIA ina kila kituko, kama hujawahi kukisikia omba Mungu akupe uzima! Mama mmoja, aitwae Elizabeth Selestine, mkazi wa Kigogo-Mburahati, Dar hivi karibuni alizua timbwili nyumbani kwake baada ya majirani, wajumbe na ndugu zake kumjia juu kwa kitendo chake cha kuishi na wanaume wawili kwenye chumba kimoja, Ijumaa lina mkasa kamili.

[TABLE="class: tr-caption-container, width: 540, align: center"]
[TR]
[TD]
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption"]Elizabeth Selestine anayeishi na wanaume wawili.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Ndani ya timbwili hilo, watu kibao walikuwepo, lakini muhimu sana ni mdogo wa mwanamke huyo, Oscar Selestine (17) ambaye alianika kila kitu.
Oscar alisema shemejiye anaitwa Benedicto Ludovic na dada yake huyo walipanga kwenye nyumba ya akina Juma Ngulumo ambaye ndiye mwanaume wa pili, yaani hawara.

[TABLE="class: tr-caption-container, width: 540, align: center"]
[TR]
[TD]
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption"]Mume wa ndoa.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

“Baada ya kuanzisha uhusiano na Juma, mwenye nyumba (baba wa Juma) aliwafukuza akiogopa kuwa kwa tabia ya dada lisije likatokea balaa kubwa. Hata mimi na mdogo wangu tuliishi kwa dada na shemeji.
“Dada na shemeji wakahamia kwenye chumba kimoja nyumba ya jirani, dada akaniambia mimi na mdogo wangu mwingine tuishi nao huku tukitafuta pa kulala kwa sababu wao walipata chumba kimoja ambacho tulikuwa tunalala wote, mimi, mdogo wangu, dada, shemeji na watoto wao wawili.

“Lakini siku moja nilishangaa kumwona Juma akija na godoro hapo hapo kwenye chumba kimoja huku shemeji akiwemo,” alisema Oscar na kuwashangaza hata mapaparazi. Dunia ina mambo mengi.
[TABLE="class: tr-caption-container, width: 540, align: center"]
[TR]
[TD]
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption"]Mama mwenye nyumba.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

“Nilishtuka sana! Kulala kwenyewe, shemeji na dada kitandani, Juma akawa analala chini wakati na yeye ni mtu mzima tena ana watoto,” alisema Oscar.
Oscar aliendelea kusema kuwa, siku moja alishangaa kumwona Juma akimpiga dada yake, alipojaribu kuuliza dada huyo akamjibu: “We mtoto, hayakuhusu.” Mwisho yeye na mdogo wake wakafukuzwa na kuambiwa wasifike nyumbani hapo.
Oscar hakuona sababu ya kufunga kinywa bila kumalizia kusema yote, akaanika kwamba ilifika mahali Juma alianza kumpiga shemeji yao kisa eti amekuwa na wivu kwa mke wake. Makubwa hayo!

“Kumbe mtoto mmoja wa dada alikuwa akiona kila kitu, siku moja akaanika siri kwamba, Juma huwa anampiga shemeji usiku na ili amuache dada alale naye chini,” alisema Oscar.
[TABLE="class: tr-caption-container, width: 540, align: center"]
[TR]
[TD]
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption"]Ndugu wa mke.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Oscar akasema hakuna siri ya watu wawili, baadaye habari zilizagaa kwa ndugu wote kuwa dada yao anaishi na wanaume wawili, ndipo mama mwenye nyumba alimuita na kumkanya lakini hakusikia.
Mwenye nyumba alipoona jeuri hiyo alimuita tena na kumpa siku saba aondoke ndani ya nyumba yake lakini bado Elizabeth hakufanya hivyo.

Oscar tena: “Huwezi amini ilifika wakati shemeji akileta chakula kinapikwa halafu yeye hatengewi, anatengewa Juma, shemeji akiuliza anaambiwa akale na watoto. Sisi hatumuelewi shemeji, kama ni madawa basi yamemkolea sana.”


Ikadokezwa kwamba tukio hilo lilifika mbali, hadi kwa wazazi wa mwanaume, Kilosa, Morogoro ambao walifunga safari mpaka Dar lengo lilikuwa kuwachukua wajukuu na mtoto wao Benedicto, lakini ilishindikana kwani waliambulia kutukanwa na mwanamke huyo, wakaondoka wakiacha laana nyuma.


Vituko viliendelea siku hadi siku, siku moja Benedicto au maarufu kwa jina la ‘baba Gire’ alikwenda kwa mjumbe wa eneo hilo, Maua Thabiti huku akilia na kuapa ipo siku atafanya kitu kibaya ambacho mkewe na Juma hawatakaa wakisahau.

Mjumbe huyo ambaye ni wa shina namba 48, mtaa wa National Housing Mburahati, Dar alikiri kupokea malalamiko hayo lakini akasema mwanaume huyo anaogopa kuweka wazi kwa sababu atapigwa, hivyo anamuachia Mungu.


Mwenye nyumba wanayoishi watu hao, Flora Mtumbati alipoulizwa naye alikiri kuwa, Eliza anaishi na wanaume wawili.

“Baada ya kubaini hilo, Eliza aliitwa na Jumuiya ya Katoliki anakosali na kuonywa. Mimi nilimpa siku saba za kumtoa Juma na kubaki na mumewe, aliniahidi lakini hakufanya hivyo, bora watu wa magazeti mmekuja mnaweza kunisaidia,” alisema Flora.
Baada ya kuongea na vyanzo vyote, gazeti lilimtafuta Elizabeth:


“Huyu bwana (Juma) alikuja kwangu kwa matatizo, alikaribishwa na mume wangu, nilimkaribisha chumbani kwangu kwa sababu ndiyo chumba hichohicho. Hata hivyo, leo (Ijumaa iliyopita) anahama

Baada ya waandishi kuondoka, mwanamke huyo alitishia kujiua. Siku ya pili, waandishi waliambiwa kuwa mwanamke huyo alikimbilia Kimara kwa wifi yake ambaye ni ndugu wa Juma.


Benedicto alipopatikana alisema: “Sikuamini kama mke wangu anatembea na Juma ingawa niliwahi kusikia. Kuhusu kupigwa ni kweli hasa akilewa pombe. Baada ya sakata hili mke wangu amesema kwa watu kuwa hata mtoto wa mwisho si wangu, ni wa Juma. Inauma sana


Baada ya waandishi kuibua ishu na watu kujaa, inadaiwa Juma alitafuta vijana na kumpa kichapo cha nguvu baba Gire ambapo ameshonwa nyuzi kumi na mbili mdomoni na jichoni.
Kesi hii ilifikishwa Kituo cha Polisi Mburahati na kufunguliwa jalada namba MBR/RB/1204/13 KUJERUHI.


---Gpl
 
CYBERTEQ

CYBERTEQ

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2012
Messages
7,420
Likes
246
Points
0
CYBERTEQ

CYBERTEQ

JF-Expert Member
Joined Feb 11, 2012
7,420 246 0
Hahahaa, uswahilini kazi kwelikweli! Kwanza niwie radhi mkuu Mzizi Mkavu kwa sababu nilopoona title tu nikaanza kujisemea "kaka mzizi naye amekosa za kukopi, mwanamke anaishi na wanaume wawili kama wamekubaliana inatuhusu nini"! Inavoonekana huyo mume mtu ana matatizo ya akili, yaani ameletewa mwanaume mwingine ndani, na anapigwa...hapo ni kwake au kwa mkewe, si afukuze wote abaki peke yake, au kama vipi asepe akaanze maisha sehem nyingine kivyake!..kweli duniani kuna wanaume zezeta!
 
Last edited by a moderator:
Mentor

Mentor

JF-Expert Member
Joined
Oct 14, 2008
Messages
19,936
Likes
10,928
Points
280
Mentor

Mentor

JF-Expert Member
Joined Oct 14, 2008
19,936 10,928 280
Mh!:A S-confused1::A S-confused1::shocked::shocked::shocked::faint2::faint2::faint2:
 
kabanga

kabanga

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2011
Messages
31,849
Likes
5,210
Points
280
kabanga

kabanga

JF-Expert Member
Joined Dec 12, 2011
31,849 5,210 280
upuuzi mtupu kwa hawa jamaa....
 
Watu8

Watu8

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2010
Messages
47,724
Likes
3,407
Points
280
Watu8

Watu8

JF-Expert Member
Joined Feb 19, 2010
47,724 3,407 280
Ukisikia zombie basi ndio huyo Benedicto...mwanaume jina
 
Vitaimana

Vitaimana

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2013
Messages
3,554
Likes
819
Points
280
Vitaimana

Vitaimana

JF-Expert Member
Joined Nov 2, 2013
3,554 819 280
Dunia sasa yaelekea kubaya.
 
HHHK

HHHK

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Messages
762
Likes
55
Points
45
HHHK

HHHK

JF-Expert Member
Joined Aug 20, 2013
762 55 45
Hahahaa, uswahilini kazi kwelikweli! Kwanza niwie radhi mkuu Mzizi Mkavu kwa sababu nilopoona title tu nikaanza kujisemea "kaka mzizi naye amekosa za kukopi, mwanamke anaishi na wanaume wawili kama wamekubaliana inatuhusu nini"! Inavoonekana huyo mume mtu ana matatizo ya akili, yaani ameletewa mwanaume mwingine ndani, na anapigwa...hapo ni kwake au kwa mkewe, si afukuze wote abaki peke yake, au kama vipi asepe akaanze maisha sehem nyingine kivyake!..kweli duniani kuna wanaume zezeta!
Kaka usicheze na limbwata utashangaa chumvi ina kua sukari


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
The Boss

The Boss

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2009
Messages
37,831
Likes
23,171
Points
280
The Boss

The Boss

JF-Expert Member
Joined Aug 18, 2009
37,831 23,171 280
Maendeleo ndo Haya...wamewezeshwa sasa wanaweza..
 
Hajar

Hajar

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2014
Messages
25,470
Likes
66,044
Points
280
Hajar

Hajar

JF-Expert Member
Joined Mar 12, 2014
25,470 66,044 280
Ama kweli dunia ina mambo na mambo yenyewe ndio kama haya.
 
samsun

samsun

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2014
Messages
7,434
Likes
5,075
Points
280
samsun

samsun

JF-Expert Member
Joined Feb 9, 2014
7,434 5,075 280
Safi sana haki sawa kwa wote kama sisi tunavyofanyaga (wanaume) basi na wao wanaweza
 

Forum statistics

Threads 1,252,114
Members 481,989
Posts 29,795,876