mwanamichakato
JF-Expert Member
- Mar 20, 2015
- 1,168
- 1,071
Maji ya shida kila kona ya nchi, mahospitali hayana dawa za kutosha, madaktari hawana vitendea kazi, polisi mishahara yao haikidhi haja zao, watumishi wa serikali wanalia kila mei mosi, shule zina uhaba mkubwa wa madarasa /madawati /walimu, nchi inadaiwa ndani na nje, huduma za nishati bado ni anasa kwa watanzania wengi....
Leo wachache wanachota mabilioni na kuyatumia kudhihaki watanzania maskini sababu tu ya ukaribu wao na watawala waliopewa dhamana ya uongozi na wananchi walio maskini..leo watuhumiwa wa wizi mkubwa wanageuka mashujaa, wafanyabiashara maarufu, waheshimiwa,...
Eeh mwenyezi mungu nakuomba utende muujiza ili viongozi wachache walio waadirifu ambao umewateua na kuwachagua kupitia kura za malaika wako na wanadamu wasimame kidete /wafanye maamuzi magumu /watende haki /wathubutu pasipo woga kuiokoa nchi yetu tanzania dhidi ya uozo, dhambi za ufisadi..mwenyezi mungu tuepushe na laana ya kuchekea wizi, udhalimu, unyanyasaji.
Nasema asante kwa sababu wewe Mwenyezi Mungu hakuna lisilowezekana kwako na sikio lako si zito hata ushindwe kuwashughulikia wote walioliibia taifa kupitia vyeo vyao, nyadhifa zao,...wote tuseme Amen.