Laana kuu Ubungo mataa!

Tatizo ni kwamba moja ya sababu inayotufanya tuendelee kuwa Masikini huwa tunakimbilia kufanya jambo jipya kabla ya kuhahakikisha tumetatua tatizo tulilonalo kwanza.
Kwa Mfano Raisi mzima anaongelea kujenga Reli mpya mpaka Burundi na nyingine mpaka Musoma wakati iliyopo ina Miaka 100 na haitumiki sasa kwa nini tusihakikishe kwanza iliyopo inatumika kwa 100% halafu baade ndio tuanze kujenga nyingine?






hapo ndio shida ya viongoz wetu,
kila siku na mipango mipya...... et waziri mwakyembe kaanzisha route ya treni
kwa hapa mjini dar kwa miundo mbinu ya Zamani huuu c uchizzzz.
 
mzee kwani hizo gari hata bila flyover si zinaendaga huko huko...kwa hiyo flyover itakuwa imetatua tatizo ubungo ambalo ndio lengo..

Hapa mkuu kutatua tatizo sehemu moja na kutengeneza tatizo sehemu nyingine si njia ya kitaalam.
 
Tatizo wabongo wengi mbulula halafu wanajifanya wanajua kuchangia upuuzi, flyover ndo huwa suluhisho la foleni sio lazima ujenge zote kwa pamoja mfano bara bara kutoka manzini swaziland to mbabane kuna flyver za kumwaga ambazo wala hazioneshi kuwa gharama sana pia kutoka Johburg mpaka pretoria so mchezo ,najua watakuja kutetea ule uf.a.la wao ku SA imeendelea kiuchumi je swazi wana uchumi gani? Nairobi je Nigeria je,nadhani Tanzania ndo nchi ambayo haina flyover hata moja,swala kwamba barabara zipigwe grader ni hoja chakavu japo itasaidia kidogo coz kila m2 atataka kupita huko kwa tunaojua chocho za bongo liko wazi hili,halmashauri nyingi najua hazina foleni kabisa ukiacha majiji magreda yanatosha ila provision ya bara bara nyingi tena za flyover zinatakiwa sio barabara mbili kila cku kwenye majukwaa na tv juu mnajicfia wakati kila kukicha mko ulaya mnaona wanaume wenzenu walivyotumia akili zao na rasilimali.

Nigeria zipo flyover nyingi sana lakini traffic yake unaweza sema Dar hakuna traffic. Pia wana road network kubwa mno. Flyover si suluhu kwa Dar. Njia zilizopo zifanywe zipitike, sio mtu anatoka Tabata anaenda kimara au mbezi apite ubungo ilihali zipo njia mbili za kumfikisha huko ambazo hazipitiki kirahisi, n.k
 
Binafsi napinga Kujengwa Daraja Ubungo Mataa kwa sasa na badala yake hizo Fedha kama zipo zipelekwe kujenga Br. za Mikoani na Wilayani! Bado kuna Mikoa Mingi sana haijaunganishwa na Br. za Uhakika na Dar tayari ina miundombinu mizuri na ya kutosha! Kwa Mf. waunganishe Mbeya mpaka Tabora na mwishowe Kigoma n.k


Kwahiyo hii itaondoa foleni za dar?
 
Nigeria zipo flyover nyingi sana lakini traffic yake unaweza sema Dar hakuna traffic. Pia wana road network kubwa mno. Flyover si suluhu kwa Dar. Njia zilizopo zifanywe zipitike, sio mtu anatoka Tabata anaenda kimara au mbezi apite ubungo ilihali zipo njia mbili za kumfikisha huko ambazo hazipitiki kirahisi, n.k

Mkuu tatizo la foleni bongo linatokana na mambo mengi kubwa ikiwa ni miundo mbinu yenyewe hii nakubali ila nachoona mm hatuna barabara za kutosha nadhani sababu ni kua maeneo mengi hayajapimwa yako kiholela. Huwezi kulinganisha nigeria na tanzania wana magari takribani mil 12 wakat kwetu hayafiki hata milion 1 kwa mujibu wa takwimu za shirika la afya duniani. Unaweza kuangalia hapa.
Registered vehicles: Number of registered vehicles - Data by country
 
Baada ya kukaa foleni masaa mawili pae ubungo mataa ninaomba kujua yafuatayo.

1.) Ni hasara kiasi gani tumepata kama Taifa katika kipindi cha miaka kumi mpaka Leo kutokana na foleni hizi.

2.) Inagharimu kiasi gani kujenga daraja la magari kupita juu pale junction.

3.) Tukijua hizi data basi tutaweza kukadiria ni kwa kiasi gani serikali Yetu inawazimu.

Kwa Tanzania ukiona kuna tatizo ujue ni kafara kwa neema za wakubwa!
pengine hii foleni kuna wakubwa wanfaidika au watafaidika nayo in future, si bure maana Kama si hivyo wangefikiria Kutatua kwa haraka!
 
Baada ya kukaa foleni masaa mawili pae ubungo mataa ninaomba kujua yafuatayo. 1.) Ni hasara kiasi gani tumepata kama Taifa katika kipindi cha miaka kumi mpaka Leo kutokana na foleni hizi. 2.) Inagharimu kiasi gani kujenga daraja la magari kupita juu pale junction. 3.) Tukijua hizi data basi tutaweza kukadiria ni kwa kiasi gani serikali Yetu inawazimu.
Mkuu wakishajenga flyovers; CCM watatumia njia gani kuomba kura kwa wananchi. Maana kila uchaguzi ahadi ni zile zile barabara na maji. Sasa wakitekeleza hizo ahadi, wataahidi nini kwenye uchaguzi unaofuata?
 
Baada ya kukaa foleni masaa mawili pae ubungo mataa ninaomba kujua yafuatayo.

1.) Ni hasara kiasi gani tumepata kama Taifa katika kipindi cha miaka kumi mpaka Leo kutokana na foleni hizi.

2.) Inagharimu kiasi gani kujenga daraja la magari kupita juu pale junction.

3.) Tukijua hizi data basi tutaweza kukadiria ni kwa kiasi gani serikali Yetu inawazimu.

Hao ni mpaka watoke madarakani, maana hawana jambo lolote la maana wanalofanya. Miundombinu yote ni hovyo tu, kila siku kuongea tu bila vitendo...hovyoooòoooooooooooooo
 
Pale panaudhi aisee. Kuna rafiki yangu aliwahi kusema eti ni heri uwe kwenye foleni nyuma kuliko mbele. Ukiwa mbele eti husogei! Nilicheka sana.

Nafikiri tuwe wabunifu maana situation yenyewe haionekani ku-improve siku za usoni. Muwe mnatembea na audio books msikize huko kwenye magari yenu...au msikize kwa simu etc. Acheni kuchokonoa simu kutwa...ukiwa kazini wewe na simu; ukiwa out baada ya kazi wewe na simu; kwenye usafiri wakati wa kurudi nyumbani vivyohivyo. Ni kuchat tu na kutafuta charger muda wote! Kama mnabisha fanyeni utafiti mdogo kesho kuangaoia abiria wa daladala au wadau waliojaliwa usafiri wao. Kama hawasikizi nyimbo basi wanashangaa nje. Tutumie muda ule unaokaa folenini kwa kulisha ubongo na mambo mapya.
Kila lakheri wadau
wazo zuri saaana
 
Back
Top Bottom