Laana kuu Ubungo mataa!

Exorcist

JF-Expert Member
Feb 28, 2014
1,236
1,254
Baada ya kukaa foleni masaa mawili pale ubungo mataa ninaomba kujua yafuatayo.

  1. Ni hasara kiasi gani tumepata kama Taifa katika kipindi cha miaka kumi mpaka Leo kutokana na foleni hizi.
  2. Inagharimu kiasi gani kujenga daraja la magari kupita juu pale junction.
  3. Tukijua hizi data basi tutaweza kukadiria ni kwa kiasi gani serikali Yetu imelala. =======================

    Update: 16/05/2020
    E975ACF1-F560-428A-B147-FE4ECAF5D830.jpeg

    ==================================== Update: 09/09/2020. Naona Punde si punde flyover itakamilika, hongereni waTanzania!
 
Baada ya kukaa foleni masaa mawili pae ubungo mataa ninaomba kujua yafuatayo. 1.) Ni hasara kiasi gani tumepata kama Taifa katika kipindi cha miaka kumi mpaka Leo kutokana na foleni hizi. 2.) Inagharimu kiasi gani kujenga daraja la magari kupita juu pale junction. 3.) Tukijua hizi data basi tutaweza kukadiria ni kwa kiasi gani serikali Yetu inawazimu.

Binafsi napinga Kujengwa Daraja Ubungo Mataa kwa sasa na badala yake hizo Fedha kama zipo zipelekwe kujenga Br. za Mikoani na Wilayani! Bado kuna Mikoa Mingi sana haijaunganishwa na Br. za Uhakika na Dar tayari ina miundombinu mizuri na ya kutosha! Kwa Mf. waunganishe Mbeya mpaka Tabora na mwishowe Kigoma n.k

Viongozi wapo kwenye usingizi wa pono...
 
Binafsi napinga Kujengwa Daraja Ubungo Mataa kwa sasa na badala yake hizo Fedha kama zipo zipelekwe kujenga Br. za Mikoani na Wilayani! Bado kuna Mikoa Mingi sana haijaunganishwa na Br. za Uhakika na Dar tayari ina miundombinu mizuri na ya kutosha! Kwa Mf. waunganishe Mbeya mpaka Tabora na mwishowe Kigoma n.k

Hasara tunayoipata ubungo ndo inasababisha tusijenge hiyo mibarabara ya mikoani..
 
Kutatatua foleni Dar ni rahisi sana wala hakuhitaji kupoteza fedha kujenga Midaraja mikuubwa, ni kuhakikisha tu kila halmashauri br. zake zote zinapitika, siyo lazima waweke lami hata wahakikishe tu kila baada ya Miezi 3 zinapigwa greda, hilo litapunguza foleni kwa zaidi ya 1/3 na kwa gharama ndogo sana, unafikiri kwa nini Oysterbay hamna foleni? Ni kwa sababu Serikali wamejenga br. zote na zinapitika hivyo kuna njia nyingi sana, kwa hiyo walipaswa wafanye kama Oysterbay kupitisha greda tu br. za Mitaani kunatosha sana tu!

Hizo greda unakodisha wewe au..?!
 
Hizo greda unakodisha wewe au..?!

Bado haunielewi, nimekwambia gharama ya kupitisha greda ni ndogo sana ukilingisha na kujenga daraja kubwa ama kuweka lami, Halmashauri zote zina magreda hivyo ni swala la kuweka mafuta tu... Ni kazi rahisi sana Mimi diwani wangu huwa anafanya kwenye Kata yetu na hatuna shida, kila baada ya miezi 3 greda linapita!
 
Baada ya kukaa foleni masaa mawili pae ubungo mataa ninaomba kujua yafuatayo. 1.) Ni hasara kiasi gani tumepata kama Taifa katika kipindi cha miaka kumi mpaka Leo kutokana na foleni hizi. 2.) Inagharimu kiasi gani kujenga daraja la magari kupita juu pale junction. 3.) Tukijua hizi data basi tutaweza kukadiria ni kwa kiasi gani serikali Yetu inawazimu.

Mkuu,
Huo ni ukweli mchungu!

Bila kujenga MADARAJA ambayo yatatoa nafasi kwa magari kupita bila kusubiriana kwenye foleni ni ndoto kuisha ndani ya Dar es Salaam na mradi wa DART ndo bomu kubwa la foleni linalosubiriwa.

Huwa najiuliza hivi hii miradi uchwara inayoanzishwa imejadiliwa na kupitiwa na wataalamu kweli au ni ile iliyofanikiwa kutoa 10% au ndo hvo tena nguvu za wanasiasa!

Maana hata kwa akili ya chekechea ,bila kuweka madaraja kwenye hizi junction km za ubungo na Tazara ni kuzidi kutengeneza bomu la foleni huko tuendako!
 
Baada ya kukaa foleni masaa mawili pae ubungo mataa ninaomba kujua yafuatayo. 1.) Ni hasara kiasi gani tumepata kama Taifa katika kipindi cha miaka kumi mpaka Leo kutokana na foleni hizi. 2.) Inagharimu kiasi gani kujenga daraja la magari kupita juu pale junction. 3.) Tukijua hizi data basi tutaweza kukadiria ni kwa kiasi gani serikali Yetu inawazimu.

Hebu jisomee kidogo: TANZANIA STARTS CONSTRUCTION OF FLYOVERS - Corporate Digest
 
Nimesikia wameextend muda wa kupiga fujo pale bungeni,ni kweli?huku na foleni mtajijuu wenzenu wanakula nchi...
Ubungo pale ni disaster kusema kweli...kama una gari ndo inazidi kuwa mbaya mana kuliacha huwezi
 
Kutatatua foleni Dar ni rahisi sana wala hakuhitaji kupoteza fedha kujenga Midaraja mikuubwa, ni kuhakikisha tu kila halmashauri br. zake zote zinapitika, siyo lazima waweke lami hata wahakikishe tu kila baada ya Miezi 3 zinapigwa greda, hilo litapunguza foleni kwa zaidi ya 1/3 na kwa gharama ndogo sana, unafikiri kwa nini Oysterbay hamna foleni? Ni kwa sababu Serikali wamejenga br. zote na zinapitika hivyo kuna njia nyingi sana, kwa hiyo walipaswa wafanye kama Oysterbay kupitisha greda tu br. za Mitaani kunatosha sana tu!

point yako ni kweli..ni kama vule ile barabara inayochepuka kimara kuja UD,mbezi kuja Makongo huku,nk..zinasaidia sana,zikiwekwa kwenye hali nzuri haina haja ya mtu kupita ubungo ,msongamano utapungua,
 
Ujenzi wa flyovers ni kiini macho.unahamisha tatizo kutoka junction A kwenda B.nafikiri tujikite zaidi kwenye ujenzi wa ring roads hii itasaidia. Kwa mfano ukijenga daraja Tazara utahamishia tatizo Buguruni na kwingineko au ukijenga Ubungo unaogeza volume Magomeni na kwingineko kwenye junction .tuache tabia ya kutaka kujionesga na tujikite kwenye utaalamu.
 
Tatizo kuchanganya siasa na kazi zinazohusu wataalam nje ya siasa Huyo jiki mwenyewe kwa ushamba wake alikataa jengo la tanesco mkoa wa Dar lisibomolewe eti ni vitu vya ki historia si unajua tena msoga hakuna ghorofa?
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom