Laana kuu Ubungo mataa!

Binafsi napinga Kujengwa Daraja Ubungo Mataa kwa sasa na badala yake hizo Fedha kama zipo zipelekwe kujenga Br. za Mikoani na Wilayani! Bado kuna Mikoa Mingi sana haijaunganishwa na Br. za Uhakika na Dar tayari ina miundombinu mizuri na ya kutosha! Kwa Mf. waunganishe Mbeya mpaka Tabora na mwishowe Kigoma n.k


Usisahau dar inchngia sana pato la taifa viwanda vingi vipo dar mahotel ya kifahari mengi wasipofanya hivyo watakosa mapato stahiki kutoka mkoa wa dar pekee yake.Chamsingi hapo siyo barabara za mikoani tu bali waendeleze mikoa hiyo ili wahamiaji wa ndani wahamie na mikoa mingine mfano waendeleze bandari ya bagamoyo, mtwara, tanga na mikoa mingine kuwahamasisha wawekezaji waje kuwekeza mikoani kujenga mahotel , mawakala wakubwa wakuuza magari ma vipuri kwa ujumla kuifanya hiyo mikoa kuwa na mzunguko wa pesa wakutosha we hebu angalia jiji la mbeya juzi juzi wamezindua lifti ya kwanza? Kwa nini watu wasuhamie dar kunakoptikana kila kitu?
 
Niko foleni ya ubungo mataa, tokea Tazara all the way hadi ubungo, malori yameshona mwanzo mwisho, masaa mawili sasa sijavuka ubungo
 
Binafsi napinga Kujengwa Daraja Ubungo Mataa kwa sasa na badala yake hizo Fedha kama zipo zipelekwe kujenga Br. za Mikoani na Wilayani! Bado kuna Mikoa Mingi sana haijaunganishwa na Br. za Uhakika na Dar tayari ina miundombinu mizuri na ya kutosha! Kwa Mf. waunganishe Mbeya mpaka Tabora na mwishowe Kigoma n.k

Mkuu kuna barabara moja inaunganisha Burundi, Rwanda, Uganda na kuelekea Congo. Ybaaani hiyo inachachandua bandari ya Dar kuweza kufanya kazi vyema. Hiyo imesahauliwa kabsaaaa. Kutengenezwa kwa barabara hii yenye kipande cha takriban 90km kingekuwa na tija mno kwa bandari ya Dar. Haieleweki kwa nini flyover za DAr ni kipaumbele hivi.
 
Teh teh umenikumbusha ile " Anayeona miambili ni ghali alive mbizi mpaka Kigamboni" dah! Hawa watu wanajisahaugi mno, nchi za watu huezi jibu upuuzi kama ule. Tena utajuta kwenye siasa uliingilia nini.
Kwani JPM alivyosema mpige mbizi nyie mlimchukulia serious?
 
Bado haunielewi, nimekwambia gharama ya kupitisha greda ni ndogo sana ukilingisha na kujenga daraja kubwa ama kuweka lami, Halmashauri zote zina magreda hivyo ni swala la kuweka mafuta tu... Ni kazi rahisi sana Mimi diwani wangu huwa anafanya kwenye Kata yetu na hatuna shida, kila baada ya miezi 3 greda linapita!
Daraja linakaa miaka mingapi na hayo magreda tutapitisha mapaka lini??? Remember the growth, population and car ownership rates in City

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu katika kiswahili hakuna uwingi wa neno taa. Unavyosema mataa sijui unamaasha nini, lakini ulitakiwa useme taa za ubungo na sio MATAA
Naona unaforce kuto kuelewa thou unaelewa. Katumia jina maarufu kama ww ni mkazi wa mji wowote wenye traffic lights nadhani unajuu hii kitu
Mswahili yoyote anajua kuwa Taa haina prural form

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ujenzi wa flyovers ni kiini macho.unahamisha tatizo kutoka junction A kwenda B.nafikiri tujikite zaidi kwenye ujenzi wa ring roads hii itasaidia. Kwa mfano ukijenga daraja Tazara utahamishia tatizo Buguruni na kwingineko au ukijenga Ubungo unaogeza volume Magomeni na kwingineko kwenye junction .tuache tabia ya kutaka kujionesga na tujikite kwenye utaalamu.
Miundombinu inapendezesha mji

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu,
Huo ni ukweli mchungu!

Bila kujenga MADARAJA ambayo yatatoa nafasi kwa magari kupita bila kusubiriana kwenye foleni ni ndoto kuisha ndani ya Dar es Salaam na mradi wa DART ndo bomu kubwa la foleni linalosubiriwa.

Huwa najiuliza hivi hii miradi uchwara inayoanzishwa imejadiliwa na kupitiwa na wataalamu kweli au ni ile iliyofanikiwa kutoa 10% au ndo hvo tena nguvu za wanasiasa!

Maana hata kwa akili ya chekechea ,bila kuweka madaraja kwenye hizi junction km za ubungo na Tazara ni kuzidi kutengeneza bomu la foleni huko tuendako!
Mbona watanzania mnapenda kulalamika lalamika si ndo mchakato wa kujenga flyovers umeanza, juzi wafanyabiasha wa pale ubungo walitolewa,.. Zabuni ilishatolewa,
 
Mbona watanzania mnapenda kulalamika lalamika si ndo mchakato wa kujenga flyovers umeanza, juzi wafanyabiasha wa pale ubungo walitolewa,.. Zabuni ilishatolewa,
Achana nao hawa.. hata mradi wa mwendokasi ulipokuwa unajengwa waliongea sana.. ila leo wanapanda mabasi na wanausifia.. watu kama hawa wapo wengi sana, cha muhimu hakikisha hawakucheleweshi kwenye mafanikio yako, mtaji wao huwa kelele tu.
 
Zikivunjwa nyumba bara bara za treni zipite zipunguze foleni jpm mbaya na vilio juu mnataka nini sasa watu wa dar mkishindwa maisha karibuni sumbakalesa
 
Poleni hazizalishi hasara bali faida kwa wauza mafuta ya petrol na dizel na hivyo kuongea mapato ya kodi za serikali zilzomo kwenye mafuta.Gari inavyokula mafuta kwenye foleni ni kicheko cha wamiliki vituo vya mafuta
 
Tatizo kuchanganya siasa na kazi zinazohusu wataalam nje ya siasa Huyo jiki mwenyewe kwa ushamba wake alikataa jengo la tanesco mkoa wa Dar lisibomolewe eti ni vitu vya ki historia si unajua tena msoga hakuna ghorofa?
Ndio JPM analivunja sasa
 
Baada ya kukaa foleni masaa mawili pae ubungo mataa ninaomba kujua yafuatayo.

1.) Ni hasara kiasi gani tumepata kama Taifa katika kipindi cha miaka kumi mpaka Leo kutokana na foleni hizi.

2.) Inagharimu kiasi gani kujenga daraja la magari kupita juu pale junction.

3.) Tukijua hizi data basi tutaweza kukadiria ni kwa kiasi gani serikali Yetu imelala.


Na cha kushangaza zaidi labda chadema, H.Rungwe & Co. wanapinga sisi kujenga flyover Ubungo!
 
Jamani, kujenga madaraja sio suluhisho. Tatizo la nchi yangu ni kwamba hatuna wataalam wa mipango ya aina yeyote. Wanawaza sasa hivi tu. Mbona mji flani niliona ma flyovers na hakuna foleni? Huo si utaalam wala sio mpango. Kujenga flyover Ubungo Mataa hakutaleta suluhisho kwani msururu utaanzia magomeni mpaka magari yatakuwa hapo juu yamekwama.
Tutengeneze michepuko tu na hizo hela ka zipo mzee Magufuli. Michepuko ikiwa mizuri na yenye lami ikiwezekana nnani atapoteza mda wake Ubungo Mataa?
Watu wanakuja na solutions rahisi rahisi tu. Watu hawataki kufikiri ni kutamka tu. Unaamuru watu waende Mabwepande. Unaenda kumtupa mtu msituni na kumwacha huko. Hujali watoto walio athirika na usumbufu huo, hujali wamama walio athirika na usumbufu huo. Ni majambazi tu unazalisha kwa ile chuki kuwa umemtoa mjini ukampeleka porini na kumtupa huko. Unaamua, boda boda zisifike mjini, unataka watu watembee toka wapi mpaka wapi. Ati, sababu ni kwamba boda boda zinatumiwa na wezi. Hivi hilo ndo tatizo kweli? Ama kweli, vichaa wanapopewa rungu, tujiandae.
Tafuta suluhisho la tatizo kwanza halafu ndo marufuku isimamie. Tanzania bila uongozi huu uliopo, yawezekana. Watu wamekata tamaa, hata kupiga kura hawataki. Anaona heri alale usingizi kuliko kwenda mchagua kichaa mwingine kwani ni wale wale tu kila siku. Ahadi kibao na flana na chepeo tu, sana sana na wali maharage sinia moja watu 10. Hiyo yaitwa Takrima. Nasema, Tanzania bila huu uongozi uliopo, YAWEZEKANA.
Nasema flyover sio suluhisho. Tengenezeni michepuko.
Ndio tunajenga sasa
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom