Laana kubwa imeikumba CCM nzima kwa dhuluma kubwa kwa watu masikini -Umemuona Bi.Mwajuma Ramadhani?

Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,873
1,894
Ndugu wana JF nilikuwa naangalia news hapa kweli nime shake .Yule mama wa miaka 106 kutoka Geita hadi Dar kutafuta haki tena hana nauli kwa kuomba lift.

Kamtaja Ngeleja, Kamtaja Kafumu, na wengine. Katishiwa maisha , kaporwa eneo lake la madini na ni urithi. Kweli laana iko CCM na serikali yetu .Yule mama akahamie wapi afanye nini? Jamani nyie mnasemaje? Mmemuona mama analia hadharani ITV?
 
katumika kisiasa... mwenye 106 years anamjuaje ngeleja??

i dont like ufedhuli lakini siasa ikizidi balaa
 
katumika kisiasa... mwenye 106 years anamjuaje ngeleja??

i dont like ufedhuli lakini siasa ikizidi balaa

Mkuu hebu nifafanulie katumikaje kisiasa ? Ina maana unapinga madai yake au mimi ndiye sijakuelewa ?
 
katumika kisiasa... mwenye 106 years anamjuaje ngeleja??

i dont like ufedhuli lakini siasa ikizidi balaa

kama alichokisema ni kweli, haitajalisha kama alikuwa anafanya siasa au laa.
 
No, yule Bibi sio chizi anaelewa anachokisema! She is right na docs zote anazo! yule ni mfano mdogo wa waTZ wengi, nakumbuka sana sana mwaka juzi Mama yangu alivyoporwa Nyumba kule kijijini kwetu na kupewa kwa mtu mwingine ambaye wala hakua mtumishi wa serikali! Duniani kuna mambo jamani
 
Mkuu if I read well between the lines naona kuna kitu .Nyumba akaporwa akapewa mtumishi ambaye si mtumishi je unaongelea hizi nyuma za sirikali ambazo Mkuu Slaa anazililia hata sasa ?
 
Wazee kama hawa waliodhulumiwa wapo wengi sana. Amemtaja kafumu kama mtu hatari aliyemtisha atamweka ndani akija Dar.
 
Ndugu wana JF nilikuwa naangalia news hapa kweli nime shake .Yule mama wa miaka 106 kutoka Geita hadi Dar kutafuta haki tena hana nauli kwa kuomba lift .Kamtaja Ngeleja, Kamtaja Kafumu, na wengine .Katishiwa maisha , kaporwa eneo lake la madini na nij urithi.Kweli laana iko CCM na serikali yetu .Yule mama akahamie wapi afanye nini ? Jamaniu nyie mnasemaje ? Mmemuona mama analia hadharani ITV ?

Hamna dhulma hapo, haman anaemiliki kilicho chini ya Ardhi wala huwezi kukirithi. Yeye chake ni cha juu ya ardhi. Huyo bibi akajipumzikie hao wanaomtumia kisiasa ndio wanaomdhulumu na ndio wenye laana.
 
Atakuwa ametishiwa ili asimchafue jamaa maana si alikuwa yuko kwenye kinyan'ganyiro? Na kwa kuwa watanganyika ni wadangayika ndio maana kafumau aliwaongopea wana Igunga kwamba yeye alikuwa hausiki na kuidhinisha maeneo wakati leo bibi anamtuhumu halafu wengine mnasema siasa na sio hayo tu kuna document nyingi kafumu alisaini na bibi yule sio chizi abebe karatasi zake hadi huku wakati hana anachodai.

Okay sawa anatumika kisiasa wazee wa Africa mashariki nao hawadai, juzi mlivyokuwa mnawapiga kupitia vibaraka wenu polisi ilikuwa je? Leo uje useme bibi hadai vipi? Endeleeni kudhulumu na unyanyasaji
 
katumika kisiasa... mwenye 106 years anamjuaje ngeleja??

i dont like ufedhuli lakini siasa ikizidi balaa

:shock:Ushindwe na ulegee! unadhani kuwa na umri mkubwa ni chanzo cha utahira? ndio tuseme wewe ukizeeka utakuwa bongo sinzia na udenda ukikutoka? Naona ungekuwa Shinyanga ungewa mwuaji mkubwa wa vinkongwe. Baba yangu ana 92 lakini ana sound mind, anaweza kujenga hoja na anajua news za yanayoendelea duniani!!
 
Wazee kama hawa waliodhulumiwa wapo wengi sana. Amemtaja kafumu kama mtu hatari aliyemtisha atamweka ndani akija Dar.

Kafumu huyu huyu wa Igunga?Nadhani ndio maana Serikali ilihamia kule kuhakikisha anashinda,ni malipo ya kazi aliyofanya ya KUIUZA nchi na rasilimali za madini wakati ule ni Kamishna wa Madini.CCM Magamba,bila Kukwanguliwa hawawezi kuliwa!!
 
katumika kisiasa... mwenye 106 years anamjuaje ngeleja??

i dont like ufedhuli lakini siasa ikizidi balaa

Chunga, bibi wa miaka 106! hiki ulichoandika itakuwa ni laana yako!
 
.hawa wazee wanatakaga wenyewe angesema kipindi cha kampeni kamfumu angempa haki yake na angesaidia wana igunga kumfahamu huyu mtu sasa mwache akome na liwe funzo kwa wengine na wazee wenzake wanayo ipa kura ccm
 
Kafumu kugombea Ubunge kumemshangaza sana hata Dr.Lwaitama leo kwenye ITV sijui kipindi gani kile .Yaani kamfanya anajiuliza kwamba ni kitu watu wana kazi na kukimbilia mjengoni ? Kafumu kalipwa fadhila for sure ila Igunga watajuta .
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom