Laana iwe juu yako Profesa Rwekaza Mukandara kwa 'Slogan' hii

Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,872
1,891
Ndiyo nadiriki kusema ulaaniwe tena kwa herufi kubwa mno. Umesoma kwa pesa ya Mtanzania na mlalahoi leo unatesa na hujali tena uloko toka. Matunda ya Uhuru wewe na JK mmeyafaidi lakini mnatunyima sisi. Ulaaniwe kwa maneno yako kwenye Ilani ya CCM. Kazi Mpya, Nguvu Mpya na Ari mpya.

Ulaaniwe kwa maneno ya Maisha bora kwa kila Mtanzania, Laana hii iwe juu yako kwa kuwa umempa JK anayatumia kuwaimbisha Watanzania mwaka wa 3 sasa na matumaini yao yana yeyuka na sasa wanasema Maisha bora ni kuchapa kazina si ukaa vijiweni.

Maneno yako uliyo wapa CCM na wao wamesha kupa cut lako kwamba Tanzania yenye Neema inawezekana lakini Neema iko wapi hadi sasa? Nasema Ulaaniwe sana tu.

Maisha bora kwa kila Mtanzania leo yako wapi?
 
lunyungu fanya uwe na rangi ya kijani kama wenzio kazi kubwabwaja t u

fanya kweli kwa kuiga mfano wa mkjj na mzee es na wengineo

kazi kuja na maneno mengi utadhani umekunywa matapu tapu
 
lunyungu huyu ana habari nzito tatizo lake hamalizi maneno anatutega.

kama anatoa kitendawili ili tuague
 
lunyungu fanya uwe na rangi ya kijani kama wenzio kazi kubwabwaja t u

fanya kweli kwa kuiga mfano wa mkjj na mzee es na wengineo

kazi kuja na maneno mengi utadhani umekunywa matapu tapu

Mtu wa Pwani haya ndiyo majibu yako kwa hoja yangu ama umeamua kunipomoshea matusi tu ? Si lazima uchangie unaweza uka skip na bado utakuwa mtu yule yule . Au haya maneno yamekuchoma ?
Hoja ijibiwe kwa hoja .
 
sasa na ww ukweli ndio huutaki?

yaani kuiga mfano wao wa kuipata hiyo rangi ya kijani rangi ya uhai na maendeleo utapungua nn?

au ww kazi yako kuja kumwaga pumba tu?
 
Mtu wa Pwani,

Mimi siihitaji rangi ya Njano ama Kijani. Niko tayari kuwa na rangi ya Blue ama nyingine yeyote lakini si njano na CCM. Pumba nazo ni zipi? Unataka kusema kwamba si Mkandara ambaye aliwapa haya maneno wana CCM na JK kuanza kuruka nayo ama nimekugusa pabaya? Laana Mwenyezi ikushukie nawe uungane na Mkandara kwa kuwaimbisha watanzania na kumbe CCM tunawafanyia kitu kibaya wananchi. Tunawaibia na kuwahadaa kila mara.

Nasema laana hii ishuke .Imesha washukia watu wa serikalini ndiyo maana kila walicho kiiba sasa ni mkorogo mtupu. Mukandara na redet wako kimya wanaangalia namna ya kumuokoa mzee maana majuzi redet imesema nyumba ni chafu lakini mwenye nyumbani ni msafi . Slogans hizi sasa zitakufa soon Mukandara anza kutafuta mpya .
 
Last edited by a moderator:
Lunyungu,

Nilidhani utatumia hekima kupinga hayo maneno lakini, ulichofanya ni sawa sawa na hao unaowalaumu kwamba wanaimbisha watanzania kwa ... ari,nguvu, kasi.... na Maisha bora kwa Kila Mtanzania...

Ni UZEMBE wa hali ya juu... kwa Mtanzania kukaa chini akidhani ataletewa maisha bora...

Maisha bora yana definition nyingi... nitakupa moja...

Watu wa Arusha wana Maisha bora kuliko wa Eldoret, Watu Dar es Salaam wana-maisha bora kuliko wa Mogadishu....

Mzazi aliyekuwa hawezi peleka mtoto wake sekondari... sasa hivi anaweza ana maisha bora zaidi....

Mwalimu aliyekuwa anapokea mshahara tareye 45 hadi 60, ana maisha bora kwa kuwa anapokea tarehe 23-25 tena kwa uhakika...

Mwananchi wa Dar es Salaam ambaye hajawahi ona maji yanatoka bombani kwa nyumba ya jirani au nyumbani kwake ana maisha bora zaidi... etc. etc...
 
Last edited by a moderator:
Slogans hizi sasa zitakufa soon Mukandara anza kutafuta mpya .
Sasa wewe Lunyungu si ukubali hiyo rangi ya njano kwa kuenzi timu ya yako ya Yanga! si kila njano maana yake CCM kuna njano nyingine zina maana ya Samba la Brazil muulize mkuu Brazameni atakusaidia kwa hilo
 
Sijaelewa Mukandara alaaniwe kwa kutoa maneno au am i missing something here?

Soon watu watakuwa wanaogopa kutumia creativity na akili zao kuja na slogans za nguvu kuogopa kulaaniwa.
 
huyu mbishi tu sasa tuseme huyu halali mchicha?

au tuseme miti yeye haitizami akiitizama inamtia kiwewe?

unajua rangi ya kijani ndio rangi ya amani na ndio rangi ya uhai.

hivi kama unaendesha gari na ikawaka rangi ya kijani lunyungu unafanya nn?
 
huyu mbishi tu sasa tuseme huyu halali mchicha?

au tuseme miti yeye haitizami akiitizama inamtia kiwewe?

unajua rangi ya kijani ndio rangi ya amani na ndio rangi ya uhai.

hivi kama unaendesha gari na ikawaka rangi ya kijani lunyungu unafanya nn?


Nasisitiza kutotaka kuitumia hii rangi full stop
 
sawa mkuu lakini unaelewa kwa mzee es na mkjj na kichuguu na mtanzania na wengineo wana rangi ya kijani?


sasa fanya kama walivyofanya wao halafu mwambie mkuu wa kaya akuwekee nyekundu au nyeupe sio tatizo.

ujumbe wangu ulikuwa ni huo

na matashi yako yataheshimiwa
 
Wanajamvii leo nataka tujadiliane kuhusu nafasi ya makamu mkuu wa chuo kikuu cha dar es salaam (UDSM) Prof Mukandala katika siasa za Taifa letu na maendeleo kwa ujumla katika Taifa letu MODE NAOMBA USITOE HII THREAD:

Nianze na utangulizi

Prof Mukandala ni kati ya washauri wakuu wa mh JK katika masuala ya siasa kwa kipindi ambacho nimemfaamu Prof Mukandala ni mtu katili dikteta ambaye hajawai kutokea kuwa VICE CHANCELLOR WA CHUO.

Huyu jamaa ndiye anaempa JK kiburi kila kitu kitakachotokea atasema NI UPEPO WA KISIASA. Ila ninachojua ni kwamba ukitaka kumpima binadamu yeyote mpe madaraka katika taasisi yoyote akika Prof Mukandala nakusikitikia unavyoendeshwa kisiasa na wanasiasa ambao kielimu umewazidi na kujikuta unawakatili watoto wa wauza mkaa, gongo na mama ntilie hadi wanapoteza haki yao ya msingi ya kupata elimu.

NI HUYU HUYU PROF ALIEANDAA FUND RISING YA KUKUSANYA HELA ILI KUJENGA STUDENT CENTRE UKU KWA MAKUSUDI KABISA AKIIPA KISOGO MABWENI YA WANAFUNZI WANAOLALA CHUMBANI 12 MABIBO HOSTEL NA ZAIDI HUKU KAMPASI KUU MAJENGO YAKIWA CHAKAVU HASA HALL 2 NA 5.

Kati ya watu ambao wameifanya ELIMU NA SIASA YA TANZANIA IFIKIE PABAYA NI PROF MUKANDALA. Nawasilisha.
 
Huyo jamaa ni zaidi ya shetani kwa anayowafanyia watoto wa wakulima.
 
Bepari la kihaya!

Maisha yake yote Mukandara hajawahi hata kuwa na bajaj ya kukodisha ; sasa huo ubepari kaupatia wapi kama sio kuiba fedha za REDET!!! Sintashangaa kama nae amekuwa mwizi kwani hao anaowashuri wanafamika kuwa ni mafisadi papa! Similar birds flock together.
 
J.K ndo mburula,hana za kujiongeza licha ya Mukandara kuwa na ya kwake ila kwasababu nchi alikabidiwa yy,yy ndo mjinga.
 

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom