Laana!! Binti wa miaka 16 anaswa Akijiuza nyakati za Usiku Akiwa na mtoto mgongoni..!!

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,266
33,039
Ama kweli shida haina aibu wala huruma! Binti wa miaka 16 aliyetajwa kwa jina la Mama K, amenaswa laivu akifanya shughuli haramu za uchangudoa akiwa na mwanaye mgongoni, akidai chanzo cha kufanya hivyo ni kutokana na shida inayoiandama familia yake.

Binti (kulia) aliyenaswa na OFM akijiuza akiwa na mwanae jijini Mwanza.

Binti huyo alibambwa hivi karibuni akijiuza huku mgongoni akiwa na mwanaye wa mwaka mmoja katika Barabara ya Uhuru (kwenye taa za kuongozea magari), jijini hapa.
Timu ya Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ambayo imetinga rasmi mkoani hapa ilinasa tukio hilo usiku wa manane ambapo ilifanikiwa kufanya mahojiano na Mama K aliyekuwa na wenzake wengi
walio chini ya miaka 18.
Paparazi wa OFM akiwa kazini jijini Mwanza.


OFM ilichukua maelezo pamoja na picha za mnato huku wenzake wakitoka nduki baada ya kuona mwanga wa kamera.
Cha kushangaza, wakati akihojiwa na OFM, Mama K alidai kuwa haogopi kupigwa picha kwa sababu alishanaswa na kuhojiwa runingani kuhusiana na ishu ya kujiuza hivyo siyo ishu kwake na wala haoni aibu.
Huku akiwa na mwanaye mgongoni, binti huyo alidai kuwa amekuwa akijiuza kutokana na ugumu wa maisha.
OFM: Wewe unatokea maeneo gani na ulianza lini kujiuza? Mama K: Mimi ni mwenyeji wa Misungwi (wilaya), kwa hapa mjini naishi Mabatini. Sikumbuki nilianza lini lakini yote hii ni kutokana na ugumu wa maisha. OFM:Huyo mtoto mgongoni ni wa kwako? Mama K: Ndiyo ni mwanangu wa kumzaa, ana zaidi ya mwaka. Nilijifungua nikiwa na umri wa miaka 15. OFM: Baba wa mtoto yuko wapi? Mama K: Sijui. OFM:Ukipata mteja unamuweka wapi mtoto au unaenda kulala naye na mwanaume?
Mama K: (huku akiondoka) Nawaachia wenzangu.
Katika kujikusanyia data za kutosha, uchunguzi wa OFM uliogusa viunga mbalimbali jijini hapa ulibaini kuwa biashara hiyo haramu imeshika kasi ya ajabu ikihusisha vitoto vidogo kati ya umri wa miaka 12 hadi 16.
Kuhusu bei, tofauti na Dar ambako bei huwa ni ghali, jijini hapa vibinti hivyo vidogo hujiuza kwa kati ya shilingi elfu saba hadi kumi na tano kwa usiku mzima. Hakuna mambo ya ‘short time’.
Katika kubainisha ukweli wa mambo kuhusiana na vitendo vya ukahaba ndani ya Jiji la Mwanza, OFM ilimtafuta meya wa jiji hilo ambapo simu yake ya mkononi haikupatikana hewani.
Akizungumzia na gazeti hili kuhusiana na ishu hiyo ya watoto wadogo kujihusisha na biashara hiyo haramu ya ngono, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Evarist Ndikilo alikuwa na haya ya kusema:
“Sina taarifa yoyote kuhusiana na watoto hao wanaojiuza ndiyo nasikia kwako labda unipe muda niongee na uongozi wa chini nitalichukulia hatua mara moja.”


CREDIT: GPL
 
Mabadiliko hasi katika maisha na tamaduni zetu. Mila zinashindwa kuhimili mtikisiko na mabadiliko kwenye mazingira yake.
 
mbona wabakaji akina kapuya hamuwafichui badala yake mnawatetea? hiyo operation yenu inatenda haki kweli?
 
Kama ulijua hastahili kufanya biashara hiyo na analazimika tu kwa ajili ya kunusuru maisha ya mwanae, nyie mnaojiita OFM, mlimsaidiaje?
 
^^
OFM msiishie kufichua uchafu tu,,saidieni wachache wao kama mfano
^^
 
Hiyo Operetion ya kikuda! Inafichua tu halafu hakuna mwendelezo wake, yaani wakishatolewa magazetini basi baadae vitoto vinarudi kujiuza. Sioni kama zoezi linasaidia. Nilitegemea wakaombe sponsorship kwa watu kama kina Lowasa wanaotoa makanisani, Chenge na matajiri wengine wachangie ifunguliwe Ngo au mfuko wa kuwasaidia hawa watoto. Wapelekwe hata ufundi wapate ujuzi wajiajiri au wawezeshwe hata kwa biashara ndogo ndogo itasaidia. Lakini sio style hii ya kufichua na kuwaacha. I wish ningekuwa kama Lowassa ningewasaidia hawa watu walioingia huko kwa ugumu wa maisha GOD GIVE ME MONEY I HAVE SO MANY PEOPLE TO RUB THEIR TEARS.
 
huyo binti naamini hapendi kujiuza isipokuwa ni shida,hao OFM wanaofanya hiyo operation wawasaidie hao mabinti kwa kuwawesha na mitaji ili wafanye hata biashara ndogondogo,siyo watoe habari ili mradi wawachafue.
 
Inatia huruma watoto hawa hawana namna wamesubiri kibwagizo cha maisha boro kwa kila mtanzania wameona sio kweli sasa wanahangaika. kila kona mnyonge amebanwa watanzania walio wengi 85% wanaishi vijijini na kutegemea kilimo huku serikali ikifunga mipaka kuzuia wasiuze mazao yao yanaendelea kuliwa na wadudu , kisa tu kuna vigogo wanafanya biashara za nafaka , serikali imeongeza kibwagizo kingine eti KILOMO kwanza wakati serikali haijatoa uhuru kwa mkulima kuuza mazao yake kwa mnunuzi anaye mtaka nchi hii mnyonge hana haki matokeo yake mabinti wanachukua njia za mkato nakujiuza ili waishi
 
Kwa nini huyu shigongo anadhalilisha watu namna hii? akili ya kawaida ingemtuma kutoa picha za WATEJA wa mtoto wa miaka 16 badala ya mtoto mwenyewe! sasa hii imeleta faida gani zaidi ya kumuumiza zaidi huyu mtoto? Au ndio harakati za kumsafisha Kapuya zinaendelea?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom