La umeme Watanzania ni waelewa, wavumilivu na linavumilika. Assuarance hii from "The Horse's Mouth" ni toshelevu. Lakini la maji linavumilika?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,337
113,180
Wanabodi,

Kama kawaida yangu, kila nipatapo fursa, huja na makala zangu za " Kwa Maslahi ya Taifa", makala ya leo ni kuzungumzia kidogo hali ya umeme nchini ambayo kwa sasa inapitia changamoto mbalimbali mojawapo ni kupungua kwa kina cha maji katika mabwawa ya uzalishaji wa umeme, hili linaeleweka na linavumilika, ufafanuzi huu wa Waziri husika from the horses mouth

ni toshelevu na ùmeeleweka.

Ila hili la mgao wa maji!, kutokana na yatizi hilo hilo, kiukweli kabisa sio tuu halieleweki, bali pia, halivumiliki!.

Tumeelezwa tutapata maji kwa mgao, mgao huu ni mgao wa aina gani ambapo kwenye baadhi ya maeneo, ni zaidi ya mgao! Mgao gani leo ni 10 days bila tone la maji! Hili la ukosefu wa maji jee ni upungufu tuu wa maji au kuna tatizo jingine hatuelezwi?. Japo ni kweli kuna upungufu wa maji, hili linaeleweka kuwa limesababishwa na ukosefu wa mvua, swali ni jee linavumilika?

Maji ni uhai! Mtu unaweza kuishi bila umeme, na maisha yakawezekana, tena wengi wetu tumezaliwa, kukulia, kusomea vijijini ambako hakuna umeme, tumeishi, na maisha yamewezekana, lakini kuishi bila maji , hakuwezekani kwasababu maji ni uhai, huwezi kuishi bila maji! Je, tunaweza kuishi bila maji?, huu ukosefu wa maji unavumilika? Tufanyaje?

Paskali
 
Sijui kwa maeneo mengine, lakini kwa hapa jijini DSM, uongozi wa DAWASA umedhihirisha kuwa ni wababaishaji wa kutupwa. Yaani pamoja na kadhia kubwa inayoendelea kuhusu utapatikanaji wa maji kwa shida kupitia utaratibu wao hovyo wa mgao usioeleweka, bado wala hawaonyeshi kusumbuka na jambo hili.

Kutoa ratiba ya mgao wa maji, huku hata maji yenyewe hayapatikani, ni kiashiria cha wazi kuwa wanafanya kazi kwa mazoea tu. Yaani imeshindwa hata kuwatumia wasoma mita wao kupeleka thathimini juu ya uhalisia wa uhaba wa maji katika baadhi ya maeneo!?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanakula rushwa so Maji hupelekwa upande mmoja tu
 
11 Reactions
Reply
Back
Top Bottom