La Parka: Afariki baada ya kuanguka wakati wa pambano

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,000
9,861
La Parka: Afariki baada ya kuanguka wakati wa pambano
1578903839330.png

Nguli wa mieleka, anayeitwa Jesús Alfonso Huerta Escoboza, maarufu kama La Parka amefariki baada ya kunguka katika uwanja wa mieleka

La Parka aliruka kama anapiga mbizi, mguu wake ulinasa kwenye Kamba kitu kilichomfanya aanguke nje ya zulia la ulingo. Kuanguka huko kulimfanya mcheza mieleka huyo kuwa katika hali ya kutojitambua na alikimbizwa hospital kwa matibabu

Ilijulikana kuwa La Parka alivunjika shingo na nyonga lakini kampuni ya AAA, ilisema kuwa alifariki kutokana na mapafu na figo kushindwa kufanya kazi

"Tunahuzunika kusema ya kuwa rafiki yetu mkali wa mieleka mexico Jesús Alfonso Escoboza Huerta "LA PARKA" ametutoka" taarifa ya AAA ilisema

La Parka alitwaa ushindi wa dunia katika the IWC World Heavyweight, the IWC World Hardcore na the IWL World Heavyweight championships vyote kwa wakti mmoja

Alianza kucheza mieleka mwaka 1987, akawa mwanamieleka kwa Zaidi ya miaka 20
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom