La Dr Ulimboka ni Kubwa au ?? Bi Simba na wenzako ! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

La Dr Ulimboka ni Kubwa au ?? Bi Simba na wenzako !

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwiba, Jun 28, 2012.

 1. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #1
  Jun 28, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Kwa hapa tulipofikishwa na serikali zetu ni sehemu ambayo sisi wananchi kama wananchi tukae chini na kujiuliza ,tunasubiri nani atuondolee tatizo hili , la watu kutekwa kupigwa na kuumizwa vibaya sana na wengine kufariki huku wakitelekezwa mwituni au kandokando ya njia ?

  Mimi kama mwananchi katika jamii sitasimamia la Dr ulimboka pekee na kuona mhusika ametenda jambo ovu na hivyo inanipasa au inatupasa kuinua sauti zetu ,kumtetea na kuwatafuta wahusika watueleze kilichowafanya ikibidi sheria ifuate mkondo wake na sio ikibidi bali wahusika wawe na kesi ya kujibu kwa kosa la kukusudia kuua.

  Ieleweke ya kuwa lililomkuta Dr Ulimboka ni jambo la kawaida kuwakuta raia wengine wa kawaida wasio kuwa na wakuwatetea wala kuwasemea hapa JF au pengine popote pale,ni umaarufu tu wa Dr Ulimboka ndio uliomfanya tukio lake kuwa la kimataifa.

  Dr Ulimboka kama raia wengine wa kawaida wote wana haki sawa katika jamii na Katiba ya Nchi , hivyo basi kuna umuhimu wa kusema kuwa kamba imekatikia pabaya kwa hawa ndugu zetu wa polisi na usalama wa raia,mali zao na Taifa.Kwani kama jambo hili linamtokea raia wa kawaida ndio ingekuwa hakuna mshituko kwa Watanzania na ni jambo la kawaida kwa matukio ya aina hiyo na vyombo husika vingekuwa vimefanikiwa katika kutekeleza kwa ufupi inasemwa hakuna ushahidi na uchunguzi ni mgumu hauwezi kufanyika ,yaishe.

  Kwa tukio hili inaonyesha haya yote wa kubeba lawama ni jeshi la polisi na Waziri wa mambo ya ndani ,hivyo basi ile tabia ya mtu kuzolewa mzobamzoba kwa kuwa tu wanaomhitaji mtu huyo ni jeshi la polisi au kituo cha polis au ofisi ya usalama wa taifa ni lazima iondolewe mara moja na iwepo sheria inayoonyesha mtu huyo amesombwa kukifuatwa taratibu zote ,kwa mfano kama ni mtaani polisi ijulishe imemkamata fulani na inampeleka popote watakapo ,ijulishwe serikali ya mtaa ,hata kama hiyo serikali ya mtaa haimfahamu mtuhumiwa huyo.

  Polisi na vyombo vingine viache kujichukulia sheria mikononi mwao ,sio wao wanawambia wananchi wasichukue sheria mikononi mwao wakati wao ,wana kesi kibao za kuwachukua watu na kuwarudisha maiti au mahututi na kuwavunjavunja.

  Na hawa wahusika na haki za binadamu sijui wanaharakati akina Bi Simba na wenzake wasiwe wanajitokeza kwa watu ambao ni maarufu peke yao hata kwa wanyonge wawe mstari wa mbele ,ili jamii iwakubali la si hivyo itakuwa inatumika na serikali ili kuwaponza wananchi wenye hasira kwa kuwambia wananchi wanalifuatilia ili watu watulie na kupoteza hasira.
   
 2. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #2
  Jun 28, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,343
  Likes Received: 1,810
  Trophy Points: 280
  Mwiba, inashangaza kweli jamaa bado wanatumia sheria za mwaka 47 wakati leo tuko Dot.com time. Zile enzi za kuwafanyia watu lolote wanalojisikia kwa kigezo cha kuhatarisha usalama wa Taifa nadhani sio sahihi kabisa. Usalama wa Taifa unatishiwa na hizi rushwa na utoroshwaji wa resources za nchi etc...kuwapigapiga raia ni ukosefu wa akili tu kwenye vichwa vya watawala
   
 3. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #3
  Jun 28, 2012
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Mwiba ninafikiri hawa wamelifanya hivyo kwa kuwa wanaamini Dr. Ulimboka anafanyiwa haya kwa sababu ya wengine! Yaani anakuwa kama ni mtetezi wa haki za binadamu (Madaktari). Ingawa kusema ukweli hawa wanaharakati nilitegemea kuwaona kwenye maTV mara tu mgomo ulipoanza, wakitetea haki za wagonjwa mahospitalini wanaoteseka kutokana na mgomo.

  Anyway tunawapongeza angalau wanaishikia fimbo serikali (hata kama fimbo yenyewe ni ya ufagio wa chelewa)
   
Loading...