LA DOWANS: Sitta afungwa mdomo; Ikulu yakanusha! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

LA DOWANS: Sitta afungwa mdomo; Ikulu yakanusha!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by muhogomchungu, Jan 19, 2011.

 1. muhogomchungu

  muhogomchungu JF-Expert Member

  #1
  Jan 19, 2011
  Joined: Jan 9, 2011
  Messages: 375
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  • Baraza la Mawaziri chini ya JK lamshambulia yeye na Mwakyembe

  na Mwandishi wetu

  RAIS Jakaya Kikwete amemfunga mdomo Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Samuel Sitta aliyeingia katika mzozo na waziri mwenzake wa Nishati na Madini, William Ngeleja.

  Mzozo huo uliibuka baada ya Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi (ICC), kuamua Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) iilipe Dowans fidia ya sh bilioni 94 kutokana na TANESCO kuvunja mkataba nayo.

  Uamuzi wa kumziba mdomo Sitta, ulifikiwa jana katika kikao cha Baraza la Mawaziri, kilichofanyika Ikulu, jijini Dar es Salaam, chini ya Rais Kikwete, ambapo pamoja na mambo mengine, mjadala wa malipo ya Dowans ulitawala kikao hicho.

  Mwingine aliyepigwa kufuli katika kikao hicho ni Naibu Waziri wa Miundombinu, Dk. Harrisson Mwakyembe, ambaye naye aliungana na Sitta kumpinga Ngeleja kuilipa Dowans.

  Vyanzo vyetu vya habari vilisema Sitta na Mwakyembe walikuwa na wakati mgumu kutetea hoja ya kutaka serikali isiilipe Dowans na kwamba hata Rais alisema hafurahishwi na hukumu ya malipo hayo.

  "Kikao bado kinaendelea, lakini Sitta na Mwakyembe walibanwa sana na mawaziri na hata Bwana mkubwa (Rais) aliungana na mawaziri wengine kuwalaumu kwa kupeleka mjadala huo hadharani," kilisema chanzo chetu cha habari.

  Kwa mujibu wa habari hizo, kuanzia sasa Sitta na Dk. Mwakyembe, wamefungwa mdomo kuzungumzia suala la malipo ya Dowans hadharani na kwamba wanapaswa kuwa kitu kimoja kuhakikisha mipango ya serikali inatekelezwa kama ilivyopangwa.

  Kabla ya kibano hicho jana, wiki iliyopita katika kikao cha kamati ndogo ya mawaziri uliibuka msuguano wa hoja kati ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema na Waziri Sitta.

  Habari kutoka ndani ya kikao hicho ambacho kilifanyika chini ya uenyekiti wa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, zinaeleza kuwa Jaji Werema alieleza kusikitishwa na matamshi ya Sitta katika vyombo vya habari.

  Taarifa kutoka ndani ya kikao hicho zimemkariri Werema akieleza kushangazwa na hatua ya Sitta kuwashambulia yeye na Ngeleja huku akijua kuwa walichokifanya na kuamua kilikuwa kinagusa moja kwa moja mamlaka yao ya kiwajibu na kimamlaka.

  Jaji Werema amekaririwa akimweleza Waziri Sitta kwamba iwapo kweli alikuwa ana uchungu na suala la Dowans, basi wakati kesi ikiendelea alipaswa kuisaidia serikali katika kuwasilisha utetezi dhidi ya malalamiko 17 yaliyokuwa yamewasilishwa na kampuni hiyo.

  Habari zinaeleza kwamba hatua ya Sitta ambaye alikuwa akitambua fika namna kesi hiyo ilivyokuwa ikiendelea kutochangia jambo lolote wakati shauri hilo likiwa ICC na badala yake kusubiri hadi serikali ishindwe ndipo aanze kutoa matamshi katika vyombo vya habari ilikuwa ni ya kuchochea hasira za wananchi dhidi ya viongozi pasipo sababu zozote.

  Wakati Jaji Werema akimshushia lawama Sitta kwa muda usiopungua dakika 15, Waziri Mkuu Pinda alikuwa kimya muda wote.

  Baada ya kumaliza hoja yake, Waziri Mkuu aliwataka wajumbe wa kamati hiyo ya mawaziri iliyokuwa ikijadili kuhusu Muswada wa Mabadiliko ya Sheria ya Manunuzi unaotarajiwa kuwasilishwa katika Bunge lijalo kuendelea na mjadala.

  Awali kabla ya Werema kuzungumza, Sitta alichangia kuhusu muswada huo na akaeleza haja ya kuwekwa kwa masharti magumu zaidi ili kuzuia uwezekano wa makampuni ya kitapeli kujipenyeza nchini na kuigharimu serikali mamilioni ya fedha kauli ambayo ilionekana kumkera Werema.

  Awali hofu ilitawala kwamba Sitta na Mwakyembe, wangeweza kupoteza nafasi zao za uwaziri kutokana na hatua yao ya kuibua mjadala dhidi ya mawaziri wenzao nje ya Baraza la Mawaziri kuhusu uamuzi wa serikali kukubali kuilipa Kampuni ya Dowans Holdings SA.

  Mkanganyiko wa kauli ya Sitta na Mwakyembe, ulisababisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Mathias Chikawe, kutoa matamshi makali ya karipio kwa mawaziri hao wawili.

  Ukali wa matamshi hayo ya Chikawe ambaye anadaiwa kupata baraka za Rais Kikwete, uliongezwa na tamko lake la kuwataka Sitta na Mwakyembe iwapo wanataka kuendeleza malumbano hayo nje ya utaratibu wa kawaida wa mawasiliano wa mawaziri, wajiondoe serikalini.

  Chikawe amekaririwa akisema kitendo cha Sitta kumtuhumu Ngeleja kwamba alitangaza kulipwa kwa Dowans kabla suala hilo halijafikishwa katika Baraza la Mawaziri kinakwenda kinyume cha miiko ya uwaziri kinachomtaka kutotoa siri za baraza.

  Kwa mujibu wa Chikawe, Waziri Ngeleja kwa mamlaka aliyonayo kama waziri mwenye dhamana na masuala ya nishati alikuwa na mamlaka ya kutoa tamko alilotoa baada ya kufanya mashauriano na wataalamu mbalimbali wa masuala ya sheria serikalini.

  Chikawe alisema iwapo Sitta na Mwakyembe walikuwa hawajaridhishwa na uamuzi wa Waziri Ngeleja walikuwa na njia za kuwasilisha hoja zao pasipo kutumia vyombo vya habari.

  Kwa upande wake, Mwakyembe ameingia matatani kutokana na kunukuliwa na gazeti la Uhuru linalomilikiwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) akieleza kushangazwa na hukumu ya Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Uwekezaji (ICC) iliyoipa ushindi Dowans dhidi ya serikali na kutakiwa kulipwa fidia ya shilingi bilioni 94. ICC iliamua katika hukumu yake Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) iilipe Dowans fidia ya sh bilioni 94 kutokana na TANESCO kuvunja mkataba nayo.
   
 2. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #2
  Jan 19, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,421
  Likes Received: 435
  Trophy Points: 180
  6 , mwakyembe tokeni humo!
   
 3. M

  Masauni JF-Expert Member

  #3
  Jan 19, 2011
  Joined: Aug 15, 2010
  Messages: 378
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Watanzania tuache unafiki, hakuna mtu atakayesema anatetea maslahi ya watanzania akiwa ndani ya CCM. Mwakyembe, 6,anna Kilango ni geresha tu. Niliwahi kusema hapo nyumba kuwa wanachotafuta hawa watu ni kujihakikishia ubunge tu. Kama kweli mtu anauchungu na nchi hii kutoka moyoni hawezi akakubali Makamba kuwa bosi wake katika Chama.
   
 4. m

  mzambia JF-Expert Member

  #4
  Jan 19, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 885
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Ni kweli kabisa
   
 5. K

  Keil JF-Expert Member

  #5
  Jan 19, 2011
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Manaibu Waziri nao huwa wanahudhuria vikao vya Baraza la Mawaziri?
   
 6. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #6
  Jan 19, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,175
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280
  ogopa kitu kinaitwa njaa mkuu.
   
 7. C

  Chief Rumanyika Senior Member

  #7
  Jan 19, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sitta, Mwakyembe na Mawaziri wengine wengi humo,

  tokeni haraka humo msije mkapakwa uchafu bure na hao mafisadi wa kimataifa na kampuni za kitapeli.

  Wapiganaji wetu ondokeni huko haraka sana kwani Chikawe ndio leo agundue maana ya utawala bora kwa kutetea wezi?
   
 8. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #8
  Jan 19, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Ushauri wangu kwa Sitta na mwakyembe:
  Kupitia bunge lililopita na kauli zenu huvi karibuni kwenye vyombo vya habari mmeudhihirishia umma kwamba mna uchungu na nchi hii. Wananchi wanajivunia kuwa na watu wa aina yenu. Ili kulinda heshima yenu mbele ya jamii na kuandika historia katika nchi yetu, nawaomba mjiuzuru na kujitenga na serikali dharimu dhidi ya wapiga kura wake. Nawahakikishia mkifanya hivyo, yatafanyika maandamano nchi nzima kuwaunga mkono. Kazi kwenu.
   
 9. s

  sss Member

  #9
  Jan 19, 2011
  Joined: Apr 27, 2010
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Amezidi naye.....Loh
   
 10. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #10
  Jan 19, 2011
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135

  Wakuu ni swali tu. Kujiuzulu kwa Mwakyembe na Sitta ndio kutafuta ufisadi tanzania? Au ndio kutaifanya serikali isiilipe Dowans? I really doubt.

  Hiring and sacking of Sitta and Mwakyembe seems that were preplanned, i am just waiting to hear the later happening. Theyr were hired so as they can be silenced, kwa maoni yangu ilikuwa ni njia ya mafisadi kuwafunga mdomo wapinga ufisadi.

  Kujiuzulu kunaweza kuwa good gesture ya kupinga, lakini kama wameamua kuilipa Dowans kujiuzulu kwao hakutabadilisha msimamo wa serikali. Mtu peke anayetakiwa kushinikizwa kujiuzulu ni Pinda, si Mwakyembe na sio Sitta.

  Ninachofuatilia sana ni kuona kama kweli Mheshimiwa Pinda ni mtoto wa mkulima, ofisa usalama wa taifa, mzalendo na kama ni kweli kutoka moyoi mwake anakubaliana na uamuzi wa Ngeleja wa kuwalipa Dowans. Nitamlaani sana kama yeye atakuwa msimamizi wa wizi wa fedha za umma, badala ya kuwa true mtoto wa mkulima anayejali watanzania.
   
 11. j

  johnmashilatu JF-Expert Member

  #11
  Jan 19, 2011
  Joined: Sep 16, 2010
  Messages: 538
  Likes Received: 265
  Trophy Points: 80
  Mimi sina Imani na Tanzania daima, nawaona kama wameingia ubia na watu wa dowans ili kuwapigia debe, habari yao kwa hakika haimaniiki na ili kuonyesha usafi wao nawashauri waache kuandika habari zinazohusu suala hili kwani tayari wameonyesha kusimamia upande moja

  Mhariri mkuu wa tanznaia daima, amendika makala yenye utata kuhusu sitta, sitegemei kama gazeti hilo linaweza likaandika habari iliyo "sawa" kumhusu Sitta

  mimi nafikiri kuna watu wamendaliwa kuwasemea Dowans ili walipw amabilioni hayo, miongoni mwao ni Majira, tanzania daima na jaji Bomani
   
 12. Msaranga

  Msaranga JF-Expert Member

  #12
  Jan 19, 2011
  Joined: Feb 10, 2009
  Messages: 959
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  mimi nawashauri SITA na Mwakyembe wajiuzulu kwenye uwaziri kwasababu serekali inampango wa kuilipa kampuni ya kitapeli Dowans wakati bunge lilidhibitisha Richmond ni kampuni ya kitapeli iweje leo tuwalipe?
  jamani wabunge mtusaidie kwa hilo hakuna kulipa kitu hapa,
  wananchi tupo pamoja na Sita na Mwakyembe kwa keli wasiwatishe kabisa
   
 13. k

  kilolambwani JF-Expert Member

  #13
  Jan 19, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 395
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  acheni wawalipe dowans, ili serikali ya ccm ijimalize, wanazani mpaka 2015 tutakuwa tumesahau kuwa 2011 waliwalipa dowans? Wale wazee wa afrika mashariki nao waanze kudai kwa nguvu haki yao
   
 14. k

  kilimajoy Senior Member

  #14
  Jan 19, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 132
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hakuna uwajibikaji Tanzania. Kama Sitta na Mwakyembe wanaona hawaridhiki na maamuzi wakae pembeni kuonyesha uwajibikaji. Waache huo uwaziri waendelee kua wabunge, au wameogopa watafukuzwa CCM, basi wakifukuzwa CCM wala wasijali kwani watarudi tena kua wabunge kwa ticket ya chama kingine..kwani watakua wamekua mashujaa.. Ila nahofia kama nao kweli wapo kimageuzi kama wanavyojiita. Kama ni wana mageuzi kweli waonyeshe kwa mfano wa kujipiga chini wenyewe kwa kupinga msimamo wa serikali wa kutaka kulipa deni. Hapo itakua wameonyesha uchungu wao na kila mmoja atawaelewa. Ila iwapo bado tuu na ni sehemu ya hii serikali dhalimu sioni kwa nini wanalalamika hivyo.
   
 15. makandokando

  makandokando JF-Expert Member

  #15
  Jan 19, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 300
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  wajiuzuru kuonyesha msimamo wao
   
 16. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #16
  Jan 19, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Waache wabaki huko huko,wawape shida wenzao hadi kieleweke,na tupate taarifa za vikao vya baraza la mawaziri.
  Sitta na Mwakyembe si watu wa kufunga mdomo,hawakupinga uamuzi wa ICC na Ngeleja bila kujua consequence za matendo yao,they have guts to do what other ministers can not do.:frusty:
   
 17. Terminator

  Terminator Member

  #17
  Jan 19, 2011
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  haka ka-nchi ketu bwana yaani usipokuwa mwana mtandao lazima uangukie pua,maana wenye uchungu na rasilimali ya nchi hii ndio wanaoonekana wabaya.
   
 18. Makindi N

  Makindi N JF-Expert Member

  #18
  Jan 19, 2011
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 1,068
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Yeye Ngeleja na Werema walianzaje kupayuka bila baraka za baraza la mawaziri. Wao kupayuka sawa, 6 na Mwakyembe kosa! Alaaaaaaaah!
   
 19. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #19
  Jan 19, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  The silence of our friends hurts more than the noise of our enemies..........
   
 20. m

  matawi JF-Expert Member

  #20
  Jan 19, 2011
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 2,055
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Agree with u Michelle. Kuna njia nyingi za kupigana na adua yaani ukiwa ndani au nje lakini zote ni muhimu na zote zina faida na hasara zake. Jf members ni wapiganaji wengi wakiwa nje na tuwaache hawa wapiganaji wa ndani siku ikifika watatoka
   
Loading...