Opportunity Cost
JF-Expert Member
- Dec 10, 2020
- 9,035
- 6,907
Majengo ya Tanesco yanatumia gharama kubwa Sana bila sababu za msingi ..Hii ndio nchi yetu ambayo inajali wananchi na kuwasogezea huduma. Hili ni jengo la Tanesco lenye thamani ya milioni 408.
--
Mchanganuo wa gharama zilizotumika kujenga ofisi ya TANESCO Wilaya ya Kyerwa, Kagera ambayo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amekataa kuifungua (TZS):
1. Chumba cha walinzi: Milioni 7
2. Uzio: Milioni 94.2
3. Jengo la ofisi: Milioni 253.8
4. Stoo: Milioni 51.55.
View attachment 1946973
Jengo la walinzi lililogharimu Tzs Milioni 7.3
View attachment 1946974
View attachment 1946723
View attachment 1946961
Ni ajabu Serikali imeshindwa kuwa na standards za gharama za majengo kwa taasisi zake ..