Kyela: Mwalimu mmoja wa shule ya sekoondari Kyela ampiga mwanafunzi kwa fimbo zisizo na idadi hadi kulazwa

Ukifukuza shule si ndo unataka na wewe ufukuzwe kazi mkuu.
Kizazi cha sasa ni dhaifu na kitukutu mno.
Walimu visirani wapo tunajua ila kama mwalimu kambonda mtoto kwa kosa stahiki acha abonde.
Tufikirieni kipindi cha shule utukutu waliokua nao wanafunzi jamani afu jifanye wewe ndo mwalimu siutaua

Sent using Jamii Forums mobile app
vp na kama mtoto wako si mtukutu na hukuwahi pewa kesi yoyote ya utukutu kama mzazi ghafla tuu unaambiwa mtoto wako kalazwa hospital hajiwezi na hapo umeuguza week mbili mwanao...

hupati ushirikiano wowote toka kwa walimu hadi mawanao anapona vp kama mzazi hapo utasemaje!?
 
Mwalimu mmoja wa kiume maarufu kwa jina la Mpogolo apiga mwanafunzi wa kike kidato cha nne fimbo zisizo na idadi hadi kulazwa na leo siku ya tatu huyo mwanafunzi bado kalazwa..
Inaelezwa kwamba kyela secondary imekua kama jehanamu ya moto kwa watoto wanao soma hapo kwani fimbo zimekua ndio chakula cha kila siku..
Imeelezwa kwamba mwanafunzi huyo alikua hajafauru mtihani vizuri hivyo akapigwa fimbo nyingi alivyo ona anazidiwa akakimbilia chooni hivyo mwalimu akatuma wanafunzi wakamchukue na kumpelekea kwake basi akaendelea kummiminia fiboko visivyo na idadi..
Mwanafunzi huyo ikabidi aombe ruhusa arudi nyumbani.. alipokua njiani akaishiwa nguvu ndipo wasamalia wema wakamchukua na kumpeleka kwao..
Imeelezwa kwamba baada ya kufika nyumbani kwao huyo mtoto alikua analia mda wote na hakuweza kukaa wala kusimama sababu ya nguvu kuishiwa..
Alipofika hospitalini vipimo havikuonesha gonjwa lolote.. lakini mwanafunzi huyo akawa bado anaishiwa nguvu na kutapika na imeelezwa kwamba hali yake inabadilika mara kwa mara...
TUNAOMBA AFISA ELIMU WA WILAYA NA WANAO SIMAMIA MASWALA YA HAKI ZA WATOTO WALIANGALIE HILI SWALA KWA JICHO LA KIPEKEE..
NB: walimu inatakiwa tujifunze kwa mwl mwingine aliye hukumiwa kunyongwa kwa kosa la kuuwa mtoto... Fimbo kwa miaka hii haimfanyi mtoto afauru vizuri zaidi ya kuwaweka ukaribu na kujua udhaifu wao..
Sent using Jamii Forums mobile app
Shida wanayokumbana nayo walimu mwisho wake kutoa adhabu kali kwa wanafunzi ni kwamba shule zina mchanganyiko wa wanafunzi wengi ambao miongoni mwao wapo wenye nidhamu na wasio na nidhamu jambo ambalo hata wazazi wanajua, sasa mwalimu anapochukua jukumu la kumkanya mwanafunzi kwa kumchapa fimbo ingawa Mara nyingi wamekuwa wakitoa adhabu hiyo kinyume na sheria na katika hali ya hasira kali utafikiri wapo wapi vitani kumkabili adui ndipo hujikuta wamesababisha madhara makubwa na wazazi wale wale ama ndugu wa mwanafunzi yule asiyekuwa na nidhamu wanakuja juu kuwatupia lawama walimu hao hao ambao waliamini wanaweza kurekebisha nidhamu ya mtoto wao.
Jambo la msingi ni kuzingatia sheria za shule kama mwanafunzi kafanya kosa ambalo anasitahili kufukuzwa basi afukuzwe ila fimbo zisitumike kama adhabu rahisi itakayombakisha shule ilihali anatakiwa kufukuzwa kitu ambacho kitapunguza rungu la mashambulizi ya jamii kwa walimu hasa wanapotoa adhabu ya viboko.
Pia kuna sheria zinazowaongoza walimu kama watumishi wa umma ukiachilia mbali wale walioajiriwa katika shule binafsi, walimu wengi wamekuwa wakikiuka sheria hizo mwisho wa siku kujifanyia mambo yao kana kwamba jamii haiwaoni. Mwalimu akikiuka sheria hizo ni haki yake kuwajibishwa na mamlaka husika.
 
moja kati ya mchango bora sanaa fimbo zimekua sifa na mtu anajikuta ni master wa kuchapa.... inafika wakati mikono inamuwasha akiona mtoto anatatizo ata dogo ama yupo na mwl mwengine anajribu kuyajenga yeye anaomba amchape kwa niaba
 
sijui wanafunzi nao siku hizi laini,pale TAQWA wakati tunasoma mwanafunzi kula kipigo hadi cha kuchakaa kawaida sana,hadi tukawa tunaona raha kupigwa tu!
 
maisha yana badirika ukipiga mtu miaka hii hadi kuchakaa utakua na kesi ya kujibu ya mauwaji... ona vituoni watuhumiwa wanakufa ona mashuleni watoto wanakufa.... ni mwendo wa kufuata sheria zilizo wekwa kupigwa hadi kuchakaa ishapitwa na wakati mwisho uuwe kumbuka RAIA YOYOTE NI MALI YA SERIKALI
 
Mwalimu mmoja wa kiume maarufu kwa jina la Mpogolo apiga mwanafunzi wa kike kidato cha nne fimbo zisizo na idadi hadi kulazwa na leo siku ya tatu huyo mwanafunzi bado kalazwa..

Inaelezwa kwamba kyela secondary imekua kama jehanamu ya moto kwa watoto wanao soma hapo kwani fimbo zimekua ndio chakula cha kila siku..

Imeelezwa kwamba mwanafunzi huyo alikua hajafauru mtihani vizuri hivyo akapigwa fimbo nyingi alivyo ona anazidiwa akakimbilia chooni hivyo mwalimu akatuma wanafunzi wakamchukue na kumpelekea kwake basi akaendelea kummiminia fiboko visivyo na idadi..

Mwanafunzi huyo ikabidi aombe ruhusa arudi nyumbani.. alipokua njiani akaishiwa nguvu ndipo wasamalia wema wakamchukua na kumpeleka kwao..

Imeelezwa kwamba baada ya kufika nyumbani kwao huyo mtoto alikua analia mda wote na hakuweza kukaa wala kusimama sababu ya nguvu kuishiwa..

Alipofika hospitalini vipimo havikuonesha gonjwa lolote.. lakini mwanafunzi huyo akawa bado anaishiwa nguvu na kutapika na imeelezwa kwamba hali yake inabadilika mara kwa mara...

TUNAOMBA AFISA ELIMU WA WILAYA NA WANAO SIMAMIA MASWALA YA HAKI ZA WATOTO WALIANGALIE HILI SWALA KWA JICHO LA KIPEKEE..

NB: walimu inatakiwa tujifunze kwa mwl mwingine aliye hukumiwa kunyongwa kwa kosa la kuuwa mtoto... Fimbo kwa miaka hii haimfanyi mtoto afauru vizuri zaidi ya kuwaweka ukaribu na kujua udhaifu wao..

Sent using Jamii Forums mobile app
Mwishoni hapo Nb: Unasema walimu tujifunze ina maana na wewe ni Mwalimu? Kama ndio umeiandika kishabiki sana siungi mkono adhabu za kupitiliza lkn adhabu ni lazima ziendelee ili mambo y sawa!
 
Acha kujifanya unaelewa sana maana ya malezi kwa Watoto kuliko hata Mungu aliyeruhusu Mtoto achapwe viboko.

METHALI 23:13.

"13 Usimnyime mtoto wako mapigo; Maana ukimpiga kwa fimbo hatakufa."

METHALI 22:15.

"15 Ujinga umefungwa ndani ya moyo wa mtoto; Lakini fimbo ya adhabu itaufukuzia mbali."

binafsi viboko havikunifanya ni fauru bali yale maonyo ya wazazi pamoja na walimu mnaita canceling basi hivyo tuu vilinipa shauku ya kupambnania future yangu.... wale wote ambao walikuwa wanapigwa viboko sana hawakufauru.... binafsi viboko naona sio mkombozi kwa watoto zaidi ya cancelling ambayo itambadirisha fikra na kuwaza mambomakubwa tuuu

imefika wakati watoto wanalia sanaa wakifauria shule flani na wanakua wanaishi kwa wasi wasi....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mjulishe mwalimu wa nidhan ikiwezekana lipeleke kwa mkuu wa shule usipanic mim mwenyeww mwalimu sina syida na wanafunzi busara ndio siraha fimbo haifundi mwanafunzi bali humlemaza tumia saikolojia na unasihi pia tafuta taarifa kuhusu mwenendo wa mwanafunzi huyo umfahamu kwa undani na kwanin kakukimbia.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sema kweli mkuu ww ni mwalimu?!!!😃😃
 
Hapo kwenye kufa ndipo unapojifichia na huo upofu wako, Mtoto achapwe sana tu viboko inapobidi kimalezi, huko kuiga iga kwako styles za kizungu/haki sawa ndipo mnapokoromewa na Watoto wenu wakiwaambia "ungechelewa kidogo tu hata mimi ningekuzaa" Pumbavu
maisha yana badirika ukipiga mtu miaka hii hadi kuchakaa utakua na kesi ya kujibu ya mauwaji... ona vituoni watuhumiwa wanakufa ona mashuleni watoto wanakufa.... ni mwendo wa kufuata sheria zilizo wekwa kupigwa hadi kuchakaa ishapitwa na wakati mwisho uuwe kumbuka RAIA YOYOTE NI MALI YA SERIKALI

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi jana kuna mwanafunzi amekimbia kipindi changu kisa hakufanya zoezi..

Nilipowaambia wenzake wamtafute..akatokomea porini.

Aliporudi saa nane kuchukua daftari zake nikamwambia simpi anione leo asubuhi.
Leo hajaja shule kabisa..

Sasa tukutu kama hilo dawa yake nini!??
Mwalimu samahani njoo PM

Sent using my Nokia Torch
 
kama mwalimu hupigi bakora za kikatili hupati cheo, asilimia kubwa ya waakuu wa shule ni watu katili au walikuwa katili sana ndipo wakapata cheo. we kuwa oyaoya uone
 
Wanaacha kupambna na maisha wao wanapambana na watoto... Nikuwachakaza wakachakaa.. enyi walimu tupambanie maisha yetu hivyo vitoto vingi ni dhaifuuu...
 
Back
Top Bottom