Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,266
Halmashauri ya Wilaya ya Kyela, imewasimamisha kazi watumishi sita kwa tuhuma za uhujumu uchumi, wakidaiwa kutafuna shilingi milioni 222, fedha za Uchaguzi Mkuu wa 2015 na ushuru wa Kakao
Halmashauri hiyo imeziagiza mamlaka husika kuchukua hatua kama hizo, kwa aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Clement Kasongo ambaye sasa ni Ofisa Uchumi katika Ofisi ya Katibu Tawala (Ras) Mbeya pamoja na aliyekuwa Mweka Hazina, Arafa Baraza ambaye alihamishiwa katika Halmashauri ya Kilindi mkoani Tanga
Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Hunter Mwakifuna na Kaimu Mkurugenzi wakithibitisha taarifa hiyo, jana walisema uamuzi huo umefikiwa baada ya tume mbili kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla na kikosi kazi kutoka Ofisi ya Rais, Tawala ya Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) kukamilisha uchunguzi
Alisema kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na tume hizo mbili, watumishi hao walibainika kutenda makosa hayo ya matumizi mabaya na ukiukwaji wa sheria na miongozo ya fedha zilizotolewa na serikali kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa 2015 pamoja na ubadhilifu katika fedha za ushuru wa Kakao.
"Sisi kama Halmashauri tumeshachukua hatua kutokana na mapendekezo ya tume zote mbili, ambapo katika uchunguzi wa fedha za Uchaguzi shaka imeonekana katika kiasi cha shilingi milioni 191 na kwa upande wa fedha za ushuru wa Kakao fedha ambazo zinatiliwa shaka na Takukuru wanatakiwa kuchunguza ni shilingi milioni 31", alifafanua Mwakifuna.
Chanzo: Mtanzania