KYELA: Madiwani wazichapa kavu kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wakipinga ulaji pesa

mwamajinja mapunga

JF-Expert Member
Dec 23, 2014
1,074
607
Na Amos Msuli toka Kyela.

MADIWANI watatu katika halmashauri ya wilaya ya Kyela mkoani Mbeya,kupitia chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Kaini Mwakanyemba,Tukupasya Kalinga na Ayubu Mwaisobwa (Mangoloto) wamesimamishwa kuhudhuria vikao vitatu mfururizo pamoja na kutochukua posho na stahiki zingine kwa muda huo wakidaiwa kutenda makosa ya kimaadili na kusababisha fujo katika kikao cha baraza.

Kikao hicho cha baraza la madiwani kilichokaliwa juzi kwenye ukumbi wa halmashauri ya wilaya hiyo,kilichokuwa na ajenda moja ya kuijadili ubadhirifu wa zaidi ya milioni mia saba,kiliibua sintofahamu kwa wakazi wa wilaya hiyo baada ya madiwani wa Chadema kupingana na uendeshaji wa kikao hicho wakimtuhumu mwenye kiti kuwa anawabeba mafisadi na kupelekea kuchapana makonde.

Awali madiwani hao waliwasimamisha kazi kupisha uchunguzi wakuu wa idara wawili ambao ni mhasibu wa halmashauri Arafa Baraza na mkuu wa kitego cha manunuzi Salome Lyimo wakidaiwa kuisababishia hasara ya mamilioni halmashauri hiyo ambayo.

Miongoni mwa tuhuma zilizopo kwa watumishi hao,ni kuwepo kwa vitabu feki vya kutolea lisiti za malipo,mikataba feki kati ya halmashauri na makampuni ya ununuzi wa zao la kakao,fedha za uchaguzi,fedha za mafuta pamoja na mambo mengine ambayo yalipelekea watumishi hao kusimamishwa kupisha uchunguzi.

Baada ya kukamilika kwa uchunguzi huo,kupitia timu iliyoundwa na mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiy,Joseph Mgata ambapo jana kiliitishwa kikao cha baraza la madiwani kwa ajenda hiyo moja ambapo mkaguzi wa ndani hakuwepo katika kikao akidaiwa kupewa likizo huku mkurugenzi mtendaji akikosekana hali iliyochafua hali ya hewa kwa madiwani hao.

Kwa mujibu wa mwenyekiti wa halmashauri hiyo,Dkt,Hunter Mwakifuna,ni kuwa madiwani hao wamekiuka kanuni namba 17 ya vikao vya halmashauri kwa kusababisha fujo na kupelekea kikao kuvunjika kwa saa kadhaa kabla ya kufanyika tena ambapo alisema kwa mujibu wa kiti cha mwenyekiti kupitia kanuni hiyo ametoa hukumu hiyo ya kutohudhuria vikao vitatu na kutopata stahiki zao zote ili iwe fundisho kwa wengine.

Hata hivyo madiwani hao walisema tuhuma ya ubadhirifu wa milioni mia saba unaodaiwa kufanywa na watumishi hao,ni sehemu ndogo ya ubadhirifu mkubwa katika matukio sita kutosomwa ikiwemo ya ubadhirifu wa fedha za uchaguzi mkuu na fedha za miradi mbalimbali ya halmashauri hiyo,na kupelekea madiwani wa Chadema kupinga kuzimwa hoja hizo zisisomwe na kuzuka kwa vurugu kubwa.

Kutokana na vurugu hizo,Mwenyekiti Mwakifuna,alisoma kanuni hiyo na kuwataka madiwani hao kutoka nje ya ukumbi,lakini waligoma na kupelekea madiwani wa chadema kuanza kupinga kutolewa nje madiwani wenzao na kuanza zomea zomea iliyopelekea meza kuu chini ya Mwenyekiti kutoka nje ya ukumbi huku kikao kikisimama kwa saa kadhaa.

Wakiwa nje ya ukumbi diwani wa kata ya Mikoroshoni,Cheusi Sanga,na kada mmoja wa chama cha amapindizi,Kalison Bongo ambaye pia ni mwenyekiti wa mamlaka ya mji mdogo wa Kyela walianza kushambuliana kwa maneno na kutaka kutwangana makonde ambapo diwani wa kata ya Bondeni Ayub Mangoroto,alianza kumzuia diwani Cheusi na kupelekea washikane mashati na baadaye hali ikatulia.

Baada ya masaa mawili wakiwa nje ya ukumbi,mwenyekiti Mwakifuna,aliamuru wajumbe waingie ndani,ndipo alipotaja vifungu hivyo vya kanuni na kuwaamuru madiwani hao watatu wavue majoho na kutoka nje ya kikao wakihukumiwa kutohudhuria vikao hivyo vitatu.

Wakizungumza na wandishi nje ya ukumbi,diwani wa kata ya Nkuyu Kaini Mwakanyemba,alisema hukumu hiyo haitomzuia kuwatetea wananchi ataendelea kuwatetea pindi adhabu hiyo itakapo malizika,huku diwani kata ya Bondeni Ayubu Mangoloto,akisema mwenyekiti wa halmashauri anaajenda ya siri na watumishi hao suala la utafunaji wa fedha za umma halikubaliki.

Naye diwani viti maalum Tukupasya Kalinga alisema haiwezekani halmashauri ya Kyela ichafuke kwa kuitwa shamba la bibi kwa watumishi kuchota fedha kisha kuachwa bila kuchukuliwa hatua,na kuwa hata watakaporejea kwenye vikao hivyo pindi watakapomaliza adhabu hizo,wataendelea na wembe huo huo hadi kieleweke.

Hata hivyo mwenyekiti wa halmashauri hiyo,Hunter Mwakifuna,kupitia baraza hilo,alimuamuru mkurugenzi kuitisha kikao kingine ndani ya siku saba kwa gharama zake na katika kikao hicho mkaguzi wa ndani Joseph Sengerema pamoja na yeye wawepo na wasome mbele ya kikao kuhusu taarifa zote za ubadhirifu pamoja na majibu ya tume ilichokibaini.

Mwenyekiti Mwakifuna alisema haiwezekani mkaguzi wa ndani akosekane wakati yeye ndiyo anamajibu yote na mkurugenzi kkukosekana ambapo nafasi yake alikamu Afisa mipango wilaya Fransis Mwaipopo ambaye aliwaeleza madiwani kuwa mkaguzi yupo likizo,na kwamba imeamuliwa katika kikao kijacho wawepo wote.

Mwisho.
 
Back
Top Bottom