Kwitega: Haki za Watoto sio hisani bali ni wajibu

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,000
9,862
Katibu tawala mkoa wa Arusha Richard Kwitega ameitaka jamii kutambua kuwa haki za watoto sio hisani bali ni wajibu wao wa kutimiza haki hizo.

Ameyasema hayo wakati alipokuwa akiongea na watoto , walimu katika maadhimisho ya kimataifa ya siku ya mtoto duniani yaliyofanyika leo Arusha School.

Amesema ni wajibu wa wazazi kutambua kuwa familia ndio taasisi ya kwanza kuweka msingi wa maendeleo ya watoto kwa mujibu wa makubaliano ya kimataifa yaliyosainiwa na mataifa yaliyo mengi duniani, ikiwemo Tanzania.

Amesema, mataifa yanapokaa na kukubaliana malengo kwa ajili ya ustawi na maendeleo ya watoto haimaanishi kuwa serikali na wadau wa maendeleo wanao wajibu kuyatekeleza, lakini zaidi wazazi na jamii kuanzia katika ngazi ya familia wanayo sehemu ya kutekeleza, vinginevyo familia zitaachwa nyuma.

Amebainisha kuwa ni vyema kukumbushana kwamba gharama ya kutokufanya chochote ili kubadili hali ya watoto ni kubwa mno na kushindwa kuwekeza katika huduma muhimu na ulinzi wa watoto wote sio tu kunawanyima watoto haki zao lakini kutaingiza gharama kubwa zaidi baadaye kwa ajili ya maisha tegemezi watakayoishi, kunapoteza na kupunguza uzalishaji.

Ameongeza kuwa maadhimisho hayo yanatumika kuwakumbusha viongozi, wananchi na vyombo vya habari kuwa maendeleo ya taifa letu hayawezi kupiga hatua bila kutilia maanani mahitaji ya watoto, ikiwa ni pamoja na watoto masikini na walio na mazingira magumu zaidi kutengewa mafungu toka katika bajeti kuu ya serikali na zile za Halmashauri.

Amesema kuwa ni wajibu wa jamii kuwapatia watoto haki zao zote za msingi na sio hisani ,kwani watoto Wana haki yakupatiwa kila kitu ambacho wanakihitaji .

Kwa upande wake Mratibu wa haki za watoto na vijana taifa kutoka shirika la Sos vilage kutoka makao makuu Mpeli Ali, amesema kuwa siku ya kimataifa ya mtoto inawapa nafasi kutetea haki zao za msingi na hivyo kuwapa nafasi ya kujadili hali ya usalama wao ulivyo.

Naye afisa maendeleo ya jamii mkoa wa Arusha Blandina Mkini ameeleza kuwa, mtoto akiwezeshwa anaweza, hivyo Ni vyema kumuezesha mtoto katika Mambo mbalimbali kuanzia katika swala zima la elimu .

Wakizungumza katika maadhisho hayo baadhi ya watoto walioshiriki wamesema kuwa wamekuwa wakikumbana na changamoto mbalimbali zinazowanyima haki zao za msingi ikiwemo ukatili wa kijinsia, mimba za utotoni pamoja na baadhi ya wazazi kuzima kesi pindi zinapofikishwa mahakamani.
 
Back
Top Bottom