Kwimba: Serikali imewasimamisha kazi maafisa Utumishi wa Halmashauri, hawakusimamia vizuri uhakiki wa vyeti

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,491
54,884
389160c9c03093677834df39763096ff.jpg

Maafisa Utumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Kwimba wamesimamishwa kazi kwa kosa la kutosimamia vyema zoezi la uhakiki wa vyeti vya ufaulu wa elimu ya Kidato cha nne, sita na ualimu.

“Nimemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashuri ya Wilaya ya Kwimba Pendo Malabeja kuwasimamisha kazi na kuwachukulia hatua za kinidhamu Mkuu wa Idara ya Utawala na Rasilimaliwatu Christina Bunini na Wasaidizi wake wane (4) ambao ni Edward Cornel, Rey Lema, Julius Kiduli na Clavery R.M,” alisema Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro.

Dkt. Ndumbaro ametoa maelekezo hayo, baada ya kufanya ziara ya kikazi katika Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba na kujiridhisha kuwa Maafisa Utumishi wa Halmashauri hiyo kutozingatia maelekezo ya kuwaondoa watumishi ambao taarifa zao walizojaza wakati wanaajiriwa zinaonesha kuwa wamehitimu na kufaulu kidato cha nne lakini wakati wa zoezi la uhakiki watumishi hao hawakutakiwa kuwasilisha vyeti husika kwa kigezo kuwa wana elimu ya darasa la saba.

“Kwa msingi huo na kwa kuzingatia kuwa Maafisa Utumishi hawakuwataka watumishi hao kuwasilisha vyeti vya elimu walizojaza wakati wanaajiriwa katika fomu ya taarifa binafsi, huko ni kukiuka na kupuuza agizo la Mhe. Rais Magufuli la kuwataka waajiri wote nchini kufanya uhakiki wa vyeti vya watumishi wa umma na kuwaondoa katika orodha ya malipo ya mshahara ya watumishi wa serikali (Payroll),” alisema Dkt. Ndumbaro.

Dkt. Ndumbaro amesema maafisa hao wameitia Serikali hasara kwa kuwaacha watumishi wasio na sifa kuendelea kuwepo kwenye (Payroll). Miongoni mwa watumishi walioachwa ni Bw. Ligwa Simando Simon aliyestaafu kwa hiari mnamo tarehe 04/01/2010 na Fundi Sanifu Mkuu Bw. Kalala Elieza Seleman ambaye amekiri kufanya udanganyifu kwa Katibu Mkuu-UTUMISHI Dkt. Ndumbaro baada ya kukutana nae katika Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba.

Dkt. Ndumbaro amemtaka Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza, Kamishna wa Polisi, Bw. Clodwing Mtweve kupeleka Maafisa Utumishi wengine katika Halmashauri ya Kwimba ili kutoathiri utendaji kazi, sanjali na hilo Dkt. Ndumbaro amewataka waajiri wote nchini kuhakikisha zoezi la uhakiki wa vyeti vya watumishi linafanyika kwa umakini.

Aidha, Dkt. Ndumbaro ameanisha kuwa, suala hili litawasilshwa kwa Mamlaka ya uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Pendo Malabeja kuona hatua stahiki za kuchukuliwa dhidi yake.
78f7ffcc5d8e6ad761464589770c4da3.jpg
ac6c8c941964091f3e6ab8fab5b7022e.jpg
 
Watasimamisha nchi nzima,zoezi hilo halikufanywa kwa weledi.
Wadai wengi halali majina hakuna!
Shame on them!
 
Daaa.., hizi kazi za Serikali hivi sasa zimegeuka kuwa Shubiri, kufukuzwa kazi hivi hakuhitaji Kikao wala cha uchunguzi kibaya zaidi hao Watumishi Wazembe nao hawaishi ati!!!
 
1. Bado Uhakiki unawaendesha watu.
2. Something is wrong with public officials.
3.TAMISENI itatuvusha?
 
389160c9c03093677834df39763096ff.jpg

Maafisa Utumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Kwimba wamesimamishwa kazi kwa kosa la kutosimamia vyema zoezi la uhakiki wa vyeti vya ufaulu wa elimu ya Kidato cha nne, sita na ualimu.

“Nimemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashuri ya Wilaya ya Kwimba Pendo Malabeja kuwasimamisha kazi na kuwachukulia hatua za kinidhamu Mkuu wa Idara ya Utawala na Rasilimaliwatu Christina Bunini na Wasaidizi wake wane (4) ambao ni Edward Cornel, Rey Lema, Julius Kiduli na Clavery R.M,” alisema Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro.

Dkt. Ndumbaro ametoa maelekezo hayo, baada ya kufanya ziara ya kikazi katika Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba na kujiridhisha kuwa Maafisa Utumishi wa Halmashauri hiyo kutozingatia maelekezo ya kuwaondoa watumishi ambao taarifa zao walizojaza wakati wanaajiriwa zinaonesha kuwa wamehitimu na kufaulu kidato cha nne lakini wakati wa zoezi la uhakiki watumishi hao hawakutakiwa kuwasilisha vyeti husika kwa kigezo kuwa wana elimu ya darasa la saba.

“Kwa msingi huo na kwa kuzingatia kuwa Maafisa Utumishi hawakuwataka watumishi hao kuwasilisha vyeti vya elimu walizojaza wakati wanaajiriwa katika fomu ya taarifa binafsi, huko ni kukiuka na kupuuza agizo la Mhe. Rais Magufuli la kuwataka waajiri wote nchini kufanya uhakiki wa vyeti vya watumishi wa umma na kuwaondoa katika orodha ya malipo ya mshahara ya watumishi wa serikali (Payroll),” alisema Dkt. Ndumbaro.

Dkt. Ndumbaro amesema maafisa hao wameitia Serikali hasara kwa kuwaacha watumishi wasio na sifa kuendelea kuwepo kwenye (Payroll). Miongoni mwa watumishi walioachwa ni Bw. Ligwa Simando Simon aliyestaafu kwa hiari mnamo tarehe 04/01/2010 na Fundi Sanifu Mkuu Bw. Kalala Elieza Seleman ambaye amekiri kufanya udanganyifu kwa Katibu Mkuu-UTUMISHI Dkt. Ndumbaro baada ya kukutana nae katika Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba.

Dkt. Ndumbaro amemtaka Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza, Kamishna wa Polisi, Bw. Clodwing Mtweve kupeleka Maafisa Utumishi wengine katika Halmashauri ya Kwimba ili kutoathiri utendaji kazi, sanjali na hilo Dkt. Ndumbaro amewataka waajiri wote nchini kuhakikisha zoezi la uhakiki wa vyeti vya watumishi linafanyika kwa umakini.

Aidha, Dkt. Ndumbaro ameanisha kuwa, suala hili litawasilshwa kwa Mamlaka ya uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Pendo Malabeja kuona hatua stahiki za kuchukuliwa dhidi yake.
78f7ffcc5d8e6ad761464589770c4da3.jpg
ac6c8c941964091f3e6ab8fab5b7022e.jpg
Sawa kabisa ...kuwasimamisha kwakuwa.wamefanya uzembe. Hapo dr.ndumnaro hmwalimu wangu wa organization theory japo ulikuwa unafundisha ps kwa ubane utadhani unafundisha hesabu umeitendea vyema taaluma.kama mtu hana vyeti kwann aendlee.kuwa kazini
 
Kwa maandishi haya wew na huyo mwalimu wako mna walakini.Hakuna jipya ni kutafuta kick tu aliyemteua.
 
Wewe ulitaka dr.ndumnaro afanyaje hapo? Negligence/kupuuzia.itavyovyote vile ni kosa kubwa sana kwenye jambo lolote lile. Kwann watu jwenye vyeti feki waondolewe wao wabaki kwa.uzembe wa wachache? Sawa kabisa dr ndumbaro
 
Hivi bado uhakiki haujaisha?, au ndiyo wana tafuta sababu ya kuchelewesha kupandisha mishahara
 
Back
Top Bottom