Kwikwi (Hiccups): Chanzo na Tiba (matibabu) yake

Kwikwi hutokana na kushtuka na kusinyaa kwa ghafla kwa misuli mikuu ya upumuaji (diaphragm) ambako hujirudia rudia na kusababisha hewa kuingia kwa kasi kwenye mapafu.

Hii husababisha milango ya sauti katika koo (vocal cords or voice making cords) kufunga ghafla na kutoa sauti inayosikika wakati wa kwikwi.

C8D8E48E-1D1E-45B7-BC02-8007C6D57EFA.jpeg


Kwikwi sio ugonjwa; kwikwi ya muda mfupi ni kero ndogo tu ambayo inapita, lakini kwikwi isiyokatika inaweza kuwa dalili ya tatizo lingine ambalo huenda likahitaji uchunguzi wa kitaalamu.

Sababu zinazopelekea kupata kwikwi;
  • Kula haraka haraka au kula sana (kuvimbiwa)
  • Kula vyakula vyenye viungo sana (very spicy foods)
  • Kunywa vinywaji vyenye gesi(carbonated beverages) au vya baridi sana
  • Ulevi au kunywa pombe nyingi kwa mpigo
  • Upungufu wa maji na madini mwilini (dehydration)
  • Tumbo kujaa gesi, asidi (hyperacidity) au vidonda vya tumbo
Sababu hizi mara nyingi husababisha kwikwi ya muda mfupi ambayo huisha bila kuhitaji matibabu wala uchunguzi wa kitaalamu.

Sababu nyingine (Rare but serious) ni pamoja na;
  • Upungufu au kuvurigikwa kwa kiasi cha madini mwilini(electrolyte imbalances)
  • Kukusanyika kwa sumu mwilini kama vile sumu ya figo (Uremia)
  • Magonjwa ya mapafu kama vile vichomi(pneumonia), pumu(asthma), TB au maji kukusanyika nje ya mapafu(pleural effusion),
  • Saratani au uvimbe kwenye mapafu, ubongo, uti wa mgongo au tumboni.
  • Magonjwa ya moyo (heart attack, arrhythmias, infections to the heart)
  • Kidole tumbo(Apendix illness) na magonjwa ya kufanania nayo
  • Magonjwa ya Ini, kongosho au mfuko wa nyongo
  • Madawa au kunywa sumu aina fulani
  • Kuumia katika eneo la misuli ya upumuaji (diaphragm injuries).
Kwikwi itokanayo na matatizo haya huwa ya muda mrefu au inayojirudia rudia sana, na huisha tu kama tatizo lililosababisha likigundulika na kutibiwa. Ukiona dalili ya kwikwi isiyoisha tafadhali muone daktari.

Sababu ya kisaikologia (psychological reason)– Hii huwapata watu wachache. Watu hawa hujidhania kuwa wana kwikwi isiyokatika, hivyo huendelea kutoa sauti kama mtu mwenye kwikwi. Kwikwi ya aina hii haina mfumo maalum, na haitokani na kusinyaa kwa misuli ya upumuaji; kwa mtu mwenye tatizo hili ni muhimu kutafuta tatizo alilo nalo kisaikologia na kulitatua.

Namna ya kuzuia Kwikwi
  • Kula taratibu – haraka haraka hujaza gesi tumboni na kusababisha kuvimbiwa
  • Kula kiasi kidogo kwa wakati – Inashauriwa kuongeza idadi ya milo kwa siku badala ya kiasi; milo mitano midogo midogo badala ya mitatu mikubwa kwa siku.
  • Punguza au ondoa kabisa vyakula vyenye viungo vingi/vikali.
  • Kunywa maji – Unywaji mzuri wa maji huzuia na kutibu kwikwi, pia hulinda mwili na maradhi kama vile upungufu wa maji na madini(dehydration) na figo kutofanya kazi vizuri.
  • Fanya mazoezi - huboresha ufanyaji kazi wa mapafu na misuli ya upumuaji, pia husaidia kuongeza kinga mwilini na kuimarisha ufahamu (mind state)
Kuzuia kwikwi ni muhimu tu kwa wale wanaopata mara kwa mara.

Matibabu ya asili: (Usifanye kwa mtoto)
  1. Kumshitua mhusika, au kumzubaisha ili kuondoa mawazo yake kwenye kwikwi
  2. Kunywa glasi ya maji iliyojaa bila kukata pumzi
  3. Kubana pumzi na kuhesabu mpaka kumi
  4. Kuweka sukari chini ya ulimi
  5. Kulala. Usingizi ni dawa moja nzuri sana ya kwikwi
  6. Kwa mtoto anayenyonya waweza kumnyonyesha, au kumuweka begani acheue.
  7. KWIKWI-twanga hiliki changanya na maziwa kisha kunywa glasi moja.

Matibabu ya kitaalam

Muone daktari kwa matibabu endapo:
  • Kwikwi haikatiki kwa muda mrefu (siku au zaidi),
  • Kwikwi inakusababisha kuchoka sana,
  • Kama mapigo ya moyo yanabadilika,
  • Kama unashindwa kulala kutokana na kwikwi
  • Kama inasababisha msongo mawazo kutokana na kujirudia mara kwa mara.
Kabla ya kuanzisha dawa ni muhimu kufanya vipimo ili kuhakikisha magonjwa yanayoweza kusababisha kwikwi yanapatiwa matibabu kama yapo.

Kama chanzo cha kwikwi kimefahamika katika uchunguzi, tibu chanzo na kwikwi itaisha.
 

Kivumah

JF-Expert Member
Jan 7, 2008
2,428
1,050
Nina tatizo kila nikinywa bia inapofikia ya tatu au ya nne huwa nashikwa na kwikwi, hivi ni kwanini inanitokea hivyo?

Suluhisho ni nini?

Pia Soma, Kwikwi kwa mtoto mchanga: Chanzo na Tiba

-
habari za mchana wakuu hivi tatizo la kwikwi ya muda mrefu, inasababishwa na nini?
-
Habari!mimi nina tatizo la kusumbuliwa na kwikwi kila ifikapo usiku wakati wa kula chakula,kwa anayejuwa dawa au mtaalam naomba anisaidie kwa hili kwani ikifika usiku wakati wa kula sipati raha


--------- Maelezo--------
Kwikwi husababishwa na nini?





Baada ya kusoma makala inayohusu kijana mmoja aliyesumbuliwa na kwikwi kwa zaidi ya miaka miwili na nusu, na baadaye kutibiwa tatizo hilo kwa kufanyiwa upasuaji wa ubongo na kutolewa tezi, nimeamua leo nizungumzie kwikwi.

Kwiki ni kitendo kisichozuilika ambacho hutokana na kusinyaa kwa kuta za kiwambo cha moyo au diaphragm. Kwa kawaida kwikwi ni

kitendo kinachojirudia rudia mara nyingi. Sauti ya 'hic' inayotokea wakati unapokuwa na kwikwi husababishwa na kidaka tonge

(epiglottis) ambacho hufunga haraka wakati hewa inapoingia kwenye koo. Kupiga kwikwi kwa kawaida hakuna maumivu lakini mara

nyingine husumbua hasa inapoendelea kwa muda mrefu. Kwikwi ya kawaida huweza kutulizwa kwa kunywa maji, lakini wakati mwingine kufanya hivyo hakusaidii.

Zifutazo ni sababu zinazoweza kukuletea kwikwi
1. Kula kwa haraka.
2. Kula chakula cha moto na kunywa maji baridi baada yake.
3. Kulia au kukasirika.
4. Kula chakula chenye viungo vingi au pilipili.
5. Kula chakula cha moto sana.
6. Kunywa pombe au soda kwa wingi.
7. Kukohoa sana.
8. Kucheka kupita kiasi.
9. Kufurahi sana, kusisimka au kupatwa na msituko.

Kwa ujumla tunaweza kusema kuwa, vitu ambavyo vinakiletea karaha kiwambo cha moyo au diaphragm husababisha kwikwi. Kuna sababu nyingi ambazo husababisha jambo hilo na hizo tulizotaja hapo juu ni miongoni mwazo,ambapo matokeo yake ni humfanya mtu

apige kwikwi. Kwikwi kwa kawaida huisha baada ya dakika chache au hata sekunde. Lakini iwapo kwikwi itaendelea kwa masaa au kwa siku, huweza kuwa ni tatizo muhimu la kitiba na pengine hali kama hiyo inaweza ikawa inasababiswa na ugonjwa.

Kuna baadhi ya watu hupata kwikwi sana wakati wa ujauzito, baada ya kufanyiwa operesheni na hata watoto wachanga pia hupatwa na kwikwi mara kwa mara. Wajawazito hupata kwikwi sana mwishoni mwa miezi mitatu ya mwanzo ya ujauzito na mwanzoni mwa miezi

mitatu ya pili. Kwikwi hutokea wakati wa ujauzito ni kwa sababu wakati huo uwezo wa kuvuta hewa ndani ya mapafu na kutoa nje huongezeka kwa asilimia 30 hadi 40 ikilinganishwa na hali ya kawaida. Hakuna sababu inayojulikana inayosababisha kwikwi kwa watoto

wachanga, na wazazi wanashauriwa wasitiwe hofu na suala hilo. Hii ni katika hali ambayo kwikwi baada ya upasuaji husababishwa na nusu kaputi au anesthesia.

--
Mkuu dawa ya kwikwi ya haraka sana ni maji ya kunywa..

Kwanza kabisa weka maji safi ya kunywa katika chombo cha kunywea maji i.e kikombe, glass etc

Pili, hii ndiyo hatua muhimu kabisa katika matibabu...

Fanya hivi....

Wakati utakapotaka kunywa maji, usinywee ule upande wa kawaida ambao huwa tunaweka mdomo na kupata kimiminika, hapana!
Jaribu kunywea upande wa pili ambako pua yako inaelekea, wakati ukinywa utaona unainama kadiri maji yanavyozidi kuisha kwenye glass yako!

Usihofu kudondoka! Hayo ndiyo matibabu yenyewe tena yasiyo na gharama duniani hapa! Hakikisha unakunywa bila kusimama (non stop drinking).

Baada ya muda kama dakika 1 hivi, kwikwi itakatika!

NB : USIPOONA MABADILIKO TAFADHALI WAHI HOSPITALINI UONANE NA WATAALAMU.

hii njiaimenisaidia sana mimi na jamii yangu,
Ashukuriwe mwalimu wangu wa sayansi darasa la kwanza mwaka 1999.
 
ninalo tatizo kila nikinywa bia inapofikia ya tatu au ya nne huwa nashikwa na kwikwi, hivi ni kwanini inanitokea hivyo?, na solution ni nini?.nisaidieni mabingwa

Kwikwi ni involuntary action mwilini ambapo mwili unakuwa unafanya marekebisho ya baadhi ya mifumo yake, na huwa haina dawa ya haraka, inaacha yenyewe ndani ya wastani wa dakika 20!

Lakini watu wengine wanasema ukishituliwa na kitu au na mtu kwikwi inaacha automatically, ndo maana baadhi ya watani akiona una kwikwi anaweza akakulamba ngumi ya mgongo, na kwikwi ikakatika hapohapo!
 
Ni kuondoa gesi mkuu, punguza au acha pombe. watoto wadogo inawatokea sana, kwasababu ya kunyonya maziwa.
 
Mwili unakuwa umepata kiasi kikubwa kuhimili kilevi na hivo mwili una alert kuwa sasa kiwango kinatosha. pata mbili tuu kwa afya na kama unataka ta tatu agiza na nyama choma kusindikizia. ukinywa kavu kavu tuu mbili inatosha.
 
Hi Doctor mimi ni kijana wa miaka 22 nina tatizo la kwikwi huanza nikiwa nakula au nikiamka asubui hukaa kwa masaa kama matano then hukata. Je hili tatizo hasababishwa na nini na dawa yake ni nini.
 
Hi Doctor mimi ni kijana wa miaka 22 nina tatizo la kwikwi huanza nikiwa nakula au nikiamka asubui hukaa kwa masaa kama matano then hukata. Je hili tatizo hasababishwa na nini na dawa yake ni nini.

Kwikwi inaweza kusababishwa na matatizo kwenye central nevous system, mfumo wa chakula, ubongo (mental), au hata miwasho (irritation) kwenye baadhi ya neva. Kimsingi ni kwikwi ni dalili ya tatizo fulani.

Nakushauri uende hospitali bila kuchelewa.
 
hivi jamani kwikwi ni ugonjwa au hali fulani tu ya mwili.kama ni ugonjwa, je tiba yake ni ipi? nakumbuka zamani tulikuwa tunabandika kipande kidogo cha karatasi usoni pindi kwikwi inapoanza kama tiba. sina uhakika kama kwikwi iliisha yenyewe au kwa sababu ya kile kikaratasi.na kwa kiengereza kwikwi inaitwaje,nimejaribu kuwauliza watu wengi hili swali bila mafanikio?
 
habari za mchana wakuu hivi tatizo la kwikwi ya muda mrefu, inasababishwa na nini?
 
Hujafafanu inakutokea wakati gani ili wataalamu wakusaidie, Kama inakutokea mara tu baada ya kula kunywa maji kila unapomaliza kula na jaribu kunywa maji nusu saa kabla ya mlo uone itakuwaje. Mimi si mtaalamu ila wanaojua watakuja na maelezo ya kina. Wapo wanaoamini kuwa kwikwi ni dalili ya mtu aliyelogewa chakula hivyo unapaswa ukatapishwe kwenu, hayo si maneno ya wataalamu subiri nao watasemaje.
 
Habari!mimi nina tatizo la kusumbuliwa na kwikwi kila ifikapo usiku wakati wa kula chakula,kwa anayejuwa dawa au mtaalam naomba anisaidie kwa hili kwani ikifika usiku wakati wa kula sipati raha
 
Dawa yake fanya mazoezi haya: ukishikwa tu na kwikwi jaribu kubana pumzi kwa muda wa kama dakika 1 halafu baada ya hapo shushu pumzi kwa nguvu hapo ndugu yangu hautashikwa na kwikwi tena.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom