Kwenye vipaumbele vya budget ya serikali sijaona elimu, kulikoni? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwenye vipaumbele vya budget ya serikali sijaona elimu, kulikoni?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kayabwe, Jun 6, 2012.

 1. Kayabwe

  Kayabwe JF-Expert Member

  #1
  Jun 6, 2012
  Joined: Jan 8, 2012
  Messages: 338
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Wana jf,nimesoma kwenye vyombo vya habari sijaona kama serikali Elimu imeipa kipaumbele.Mimi nadhani serikali imeamua kuachana na Elimu.Naomba mawazo na mchango kwa hili.
   
 2. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #2
  Jun 6, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,798
  Likes Received: 36,824
  Trophy Points: 280
  Serikali haihitaji watu waelimike, kwani ni elimu pekee inayoweza kuwasaidia watanzania kugundua udhalimu na unyonyaji wa serikali hii dhidi ya watanzania maskini.
  Ni elimu pekee inayaoweza kumsababisha mtanzania kuhoji sababu za umaskini wa nchi yetu ukizingatia sisi ni nchi ya 16 kwa uzalishaji wa dhahabu duniani na ni nchi ya 3 kwa uzalishaji wa dhahabu africa.
  Ni elimu pekee inayoweza kuwasababisha watanzania kuhoji iweje bajeti inayopitishwa bungeni inaishia kwenye tarakimu zinazotamkwa mdomoni tu na katika utendaji fedha hizo hazionekani.
  Ni elimu pekee inayoweza kumsababisha mtanzania kugundua kuwa kila bidhaa tunayonunua tunakatwa kodi ila uchumi ni mbovu na maendeleo yamedorora.
  Ni elimu pekee inayoweza kuwasababisha watanzania kuhoji ukubwa wa bajeti unaoishia kwenye usafiri wa viongozi.
  Ni elimu pekee inayoweza kumsababisha mtanzania anayelima pamba kuhoji sh.30 anazokatwa kwenye kila kilo anayouza zinamnufaisha vipi.
  Ni elimu pekee inayoweza kumsababisha mtanzania kuhoji matumizi mabovu ya rasilimali ya nchi hii yanayofanywa na serikali.
  Kwa ujumla, elimu haiwezi kuwa sehemu ya maeneo yanayopewa kipaumbele na serikali kwa nia ya kuendelea kuzalisha jamii ya wajinga kwa lengo la kuendelea kuwanyonya na kuwakandamiza watanzania kwani wajinga ndio waliwao.
   
 3. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #3
  Jun 6, 2012
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  vijana mmetutupa sana watawala,mmejifanya mnaijua sana peoples power! Tumeamua kuwanyima elimu tuone kama mtakula jeuri yenu! Tumewasomesha kaka zetu ndo sasa wanaikamata ccm yetu shingo!ona zito,filikunjombe,wenje..marando,lisu ,mdee nk tuliowapa elimu wanavotunyanyasa serikal yenu,kuanzia sasa mikopo hatutoi wala special kozi...kama wataka kusoma subiri 2014 ndo tutatoa mikopo kwa wote kwa ajili ya kampeni ya 2015...
   
 4. s

  sugi JF-Expert Member

  #4
  Jun 6, 2012
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,367
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 160
  "na mtanyooka mwaka huuu"
   
 5. w

  wikolo JF-Expert Member

  #5
  Jun 6, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 801
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Hili la elimu kutokuwa kwenye vipaumbele limenifikirisha sana. Nakumbuka mwaka jana ilikuwa kwenye vipaumbele na ninachojiuliza sasa ni kama yale yaliyokuwa yamedhamiriwa kwenye bajeti iliyopita yametekelezwa na kwa sasa hatuna tena matatizo upande wa elimu? Kwa upande mwingine ukiangalia ni kuwa matatizo kwenye sekta ya elimu bado ni makubwa sana. Zipo shule wala si za vijijini bali ndani ya miji na majiji yetu ambako utakuta watoto wanakaa chini sakafuni na hili nimelishuhudia jijini mwanza. Nadhani watawala wetu wanawajibika kutupa mrejesho nyuma kwenye hili wakati wa bajeti ijayo.

  Binafsi hapa mimi naona mambo mawili. La kwanza ni kwamba kama taifa hatujui nini ni vipaumbile vyetu na la pili ambalo linaweza kuwa linasababishwa na hilo la kwanza, ni kwamba kila kitu kwetu ni kipaumbele na hivyo hatujui wapi tuanzie na wapi tuishie. Matokeo ya hili ni kwamba tutakuwa pale pale tu miaka nenda rudi na maendeleo kwetu itakuwa ni ndoto!
   
Loading...