Kwenye Utungaji Katiba Mpya, Kila Kipengele Hujadiliwa?

LordJustice1

JF-Expert Member
Jan 19, 2011
2,263
530
Siku hizi nakuwa mzito sana kuanzisha mada kwa kuhofia kuchanganywa na nyingine na lengo la mada hupotea kabisa.
I hope hii itabaki hapa hapa.
Sasa naanza:
Tumesikia kuwa kuna kipengele kwenye Katiba ya CHADEMA ya mwaka 2006 hakikujadiliwa kabisa.
Kwa mtizamo wangu inawezekana kwamba hakukuwa na haja ya kujadili kwa kuwa kilikuwa OK. Na kwa uzoefu wangu katika kufuatilia jinsi Sheria zinapotungwa si LAZIMA kujadili kila kipengele. Bahati mbaya sana kwenye vyama hakuna HANSARD ya kurekodi kila tukio lililojiri kwenye kikao. MUHTASARI wa kikao usitafsiriwe kama ndio HANSARD ambapo utakuta kila kilichojadiliwa au kusemwa!

Kutunga Katiba mpya si kufuatisha yaliyokuwemo katika Katiba ya zamani (2004) na kudai kuwa kifungu "kiliondolewa" as if Katiba ilikuwa inafanyiwa marekebisho (amendment) na si kutungwa mpya. Ndio maana kwenye Rasimu ya Katiba mpya ya JMT haifanani kwa kiasi kikubwa na ile Katiba ya JMT, 1977! Kwa hiyo tuseme kwa kuwa vifungu havikuwekwa kwa hiyo "viliondolewa kinyemela?"

Na kama "viliondolewa kinyemela" kama wao wanavyoamini mbona walikaa kimya muda wote huo tangu 2006? Of course maswali ninayouliza si mageni, hata Mnyika aliwahi kuuliza baadhi ya haya!

Nawasilisha kwa mjadala!
 
Hapa naona kuna vitu haviwekwi wazi mwigamba anadai hiki kipengele kilinyofolewa wakati katiba inaenda kuchapwa

Mnyika anasema hiki kipengele kilikuwepo katika katib ya 2004 lakini katiba ya 2006 hakikuwekwa kabisa...

Dr.W.Slaa yeye ndo aliharibu kabisa yeye alidai hiki kipengele hakijawahi kabisa kuwepo kwenye katiba ya 2004 wala katiba ya 2006

sasa hapa ndo mchanganyo unapojitokeza
 
Last edited by a moderator:

Mkuu kama utaweza naomba utuwekee link kuhusu kauli za Mwigamba, Mnyika na Dr Slaa kuhusu suala hili!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom