Kwenye Upande wa matengenezo: Nini cha kuzingatia kabla na ukiwa kwenye safari ndefu

Thelionden

Senior Member
Apr 7, 2018
165
156
Wakuu habari za majukumu huko mlipo.

Kama ilivyo kawaida kupeana elimu juu ya vyombo mbalimbali vya usafiri hapa JF na kweli na kiri kujifunza mambo mengi sana hapa JF.

Sasa wakuu miezi kadhaa iliyopita nilijipatia
Kagari kangu aina ya Carina TI kako kwenye hari ya kuridhisha, nataka nisafiri nako kutoka Mbeya hadi Musoma japo sio mzoefu wa safari ndefu

Naomba ushauri wenu nini cha kuzingatia katika service ya gari kabla sijaanza safari hiyo na nini cha kuzingatia wakati wa safari na wazoefu wa gari aina hii ya carina je inahimili safari ndefu kama hii.

Natanguliza shukrani zangu.
 
Kama bandiko ulivyolisoma fuatilia hilo. Kila unapofika kwenye vituo vya mafuta, jaza full tank. Pumzika hata dk.15 ukitoka mbeya mpaka Iringa. Ukifika katikati kama kuna kituo kabla ya dodoma, pumzika na ongeza mafuta. Dodoma chukua msosi na kuongeza mafuta.
Check maji na Oil kila wakati. Ukifika Singida weka mafuta ingawa pale huwa wanakuwa na usumbufu. Angalia mwendo wako wakati unafika Sekenke.
Usiovertake. Baada ya kuingia Tambarare itakuwa jioni nadhani itabidi ulale Nzega. Usilazimishe kuendesha usiku. Kuna hotel moja Nzega baada ya round about sina uhakika kama iko chini ya NBC au ila ni nzuri na parking imo ndani. Mimi natumia hiyo kila wakati. Saa Kumi na moja anza safari kwenda kwenu.Samahani naandika kama naongea maana mimi nimefanya hivi lakini toka Dar na Dod kwa miaka zaidi ya 30 tena wakati hakuna lami ila hakukuwa na matuta wala magari mengi. Ila sasa mhu!
 
Nakushukuru sana mkuu wangu kwa maelezo mazuri sana umenijuza mengi sana piv kadilio kamili la mafuta limekaaje kutoka mbeya mpaka mwanza kwa hii gari ndogo ti
 
Pia umegusia swala la usumbufu hapo singida ni usumbufu gani huu mkuu
 
Nakushukuru sana mkuu wangu kwa maelezo mazuri sana umenijuza mengi sana piv kadilio kamili la mafuta limekaaje kutoka mbeya mpaka mwanza kwa hii gari ndogo ti
Mbeya sijafika ila toka Dod mpaka Singida utatumia about 40,000/ ili iwe full tank. Sijui bei ya sasa maana nipo porini mbali na home.
 
Safari hatua.. Jitahidi kucheki oil na maji kula baada ya mda...
Usinywe Redbull kwani mda wa kupunzika zinakosesha usingizi..
Ukijiona umechoka fika sehemu salama upunzike.Usiizime gari chini ya 15 minutes..
 
Nimekupata mkuu wangu nashukuru sana
 
Kwa maelezo yako, nafikiri umeinunua hapa hapa kwetu. Hiyo changamoto yake ni kupata maintence record ya uhakika. As huwezi jua jamaa alikuwa anaitunzaje. So kama ulivyoshauriwa, fanya vyote ila zingatia saana mwendo kasi. Ingekuwa ndani ya uwezo, ningekwambia ujaribu walau Dsm Moro na kurudi. Safari yako ni ndefu saana kwa mtu asie na uzoefu na safari za namna hiyo. Kuendesha gari salama highway kunahitaji umakini mkubwa, na uzoefu pia.
 
Machine iko kwenye Hari nzuri tu mkuu, kikubwa ni umakini kama ulivyo sisitiza
 
Wakuu habari za majukumu huko mlipo.

Kama ilivyo kawaida kupeana elimu juu ya vyombo mbalimbali vya usafiri hapa JF na kweli na kiri kujifunza mambo mengi sana hapa JF.

Sasa wakuu miezi kadhaa iliyopita nilijipatia
Kagari kangu aina ya Carina TI kako kwenye hari ya kuridhisha, nataka nisafiri nako kutoka Mbeya hadi Musoma japo sio mzoefu wa safari ndefu

Naomba ushauri wenu nini cha kuzingatia katika service ya gari kabla sijaanza safari hiyo na nini cha kuzingatia wakati wa safari na wazoefu wa gari aina hii ya carina je inahimili safari ndefu kama hii.

Natanguliza shukrani zangu.
Kwa uzoefu wangu WA safari ndefu kwanza angalia Tairi zako Kama zimexpire au kuisha, upepo stahiki kwenye Tairi.
2.ball joint, tire road end Kama zipo vizuri.
3. reckend na hyrolic Kama zipo vizuri.
4.kagua rejeta na coolant hakikisha iko sawa.
5.AC ikague inasaidia Sana mvua inaponyesha kuondoa ukungu kwa kioo, pia hufanya usichoke unapokuwa njiani.
6. Fuata Sheria na Alama au ishara za barabarani pia nenda kwa tahadhari (usiamini gari lililo Mbele yako au nyuma yako hata unalopishana nalo)
7.epuka kuendesha speed kubwa ukiwa umefungulia Mziki
8 Mtangulize Mwenyezi Mungu
 
Back
Top Bottom