gimmy's
JF-Expert Member
- Sep 22, 2011
- 3,283
- 3,271
Natamani hapa nilipo ningeletewa mashekhe,wachungaji,mapadre na waganga wakienyeji waniapishe ili nikisema uongo basi nguvu za kiroho za kokote baina yao zinihukumu.
Hapa mtaani kwetu tuna chama chetu cha kufa na kuzikana na huwa tunagawana madaraka kila baada ya miaka mitano.Kwenye uchaguzi wa mwaka jana kwenye huu umoja wetu wakuchagua viongozi wetu mgombea mmoja hakutenda haki.
Vipo vituo vingi mawakala badala ya kuwa wasimamizi walikuwa robed wakaanza kupiga kura kutwa nzima kwa mgombea mmoja huku wakiwa chini ya uangalizi madhubuti.
Kwenye umoja wetu sisi tumepiga sana hatua kwani Kila mwanachama anakadi maalumu yakupiga kura na kila kadi ina namba maalumu ikiitofautisha na zingine.
Mawakala walikuwa wanachukua makaratasi ya kura wanatizama kwenye register wanahamisha namba za kadi za mpigakura wanapiga tiki kwa yule mwenye mabavu.
Mwaka huu muitikio wa watu kupiga kura ulikuwa mdogo,vituoni kulikuwa tulivu kipindi kingi,hivyo hili zoezi likawa rahisi,
Ni kweli mgombea mwenye nguvu wanasema alishinda lakini zipo kura nyingi sana zilipigwa na wasimazi wa vituo badala ya wapiga kura.
Chaguzi za sarakasi zinaumiza sana tunaiomba serikali iwe inasimamia hivi vyama vyetu vya kufa na kuzikana ili hawa wenye nguvu wasishinde kimabavu.