Kwenye ubunge kuna nini?

RUTAJUMBUKIRWA

Senior Member
May 3, 2009
185
89
Inaonekana kilele cha mafanikio kwa kila Mbongo ni kugombea ubunge. Mwandishi wa habari akiwa maarufu badala ya kufikiria kwenda Al Jazeera, CNN, etc. anafikiria kutumia umaarufu kupata ubunge. Legal officer kama Ngeleja akipata mipesa, anakimbilia ubunge. Yasoda, ameonekana kwenye luninga mara kadhaa sasa anataka kutumia hako ka-umaarufu kwenda kugombea ubunge. Mfanyakazi wa serikali akivuna fedha ya kutosha ya rushwa, huyoooo ubunge.
Kuna nini? Je, ubunge ndo mafanikio ya juu kabisa?
Wadau mnasemaje.
 
Mishahara ya wabunge, mawaziri na majaji juu!
Chaku
user_offline.gif
25th August 2009, 09:22 AM
Mishahara ya wabunge,mawaziri na majaji imepandisha huku wa spika wa bunge ukipanda mara dufu.
Kwa kifupi tu;

Spika na Jaji mkuu Tshs 2,760,000/= mpaka 4,850,000/=
Naibu spika Tshs 2,080,000/= mpaka 2,172,000/=
Mbunge Tshs 1,840,000/= Mpaka 1,921,000/=
jaji wa mahaka kuu tshs 2,160,000/= mpaka 3,645,000/=
jaji Mahakam ya rufaa Tshs 2,310,000 mpaka 4,250,000/=
__________________
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/37077-mishahara-ya-wabunge-mawaziri-na-majaji-juu-3.html
 
Mishahara ya wabunge, mawaziri na majaji juu!
Chaku
user_offline.gif
25th August 2009, 09:22 AM
Mishahara ya wabunge,mawaziri na majaji imepandisha huku wa spika wa bunge ukipanda mara dufu.
Kwa kifupi tu;

Spika na Jaji mkuu Tshs 2,760,000/= mpaka 4,850,000/=
Naibu spika Tshs 2,080,000/= mpaka 2,172,000/=
Mbunge Tshs 1,840,000/= Mpaka 1,921,000/=
jaji wa mahaka kuu tshs 2,160,000/= mpaka 3,645,000/=
jaji Mahakam ya rufaa Tshs 2,310,000 mpaka 4,250,000/=
__________________
[URL="https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/37077-mishahara-ya-wabunge-mawaziri-na-majaji-juu-3.html"]https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/37077-mishahara-ya-wabunge-mawaziri-na-majaji-juu-3.html[/URL]

kitu wanaita marupurupu na mianya ya kufanya biashara ufisaadi huku wakilindwa na bunge ndo wanachofata
 
ndiko ambako waweza iba, vunja sheria, foji vyeti halafu ukatetewa kwa nguvu zote na chama chako hasa ukiwa kwenye hiki cha mapinduzi that never was. ukalipwa mshahara na allowances kwa kusinzia tu pale bungeni. ukapewa gari la thamani ambalo ukalitumia kuendea kwa vimada na usiguse jimboni kwako mpaka wakati wa uchaguzi.uka sign mikataba nyeti kabisa inayoihusu nchi hii halafu ukaulizwa na wawekezaji tukufanyieni nini ninyi wa tz eti kiwanja changu sijakiendeleza nahitaji mifuko 20 ya cement, tiles na bati, hahaha nyie acheni msione hawa jamaa wanaendesha ma vx yale ya milioni 150 wana njaa ya kufa mtu.
 
Kuna ulaji wa kufa mtu

jamani si ulaji mkubwa huo,

linganisha na utumishi wao na mazingira ya kazi zao. mimi siijawa mbunge bado, lakini kwa mishahara aliyoweka paka jimy hapo juu, siwezi kukubali hiyo kazi, kwani nilio nao sasa ni mkubwa zaidi.

tunagombea ubunge kwa sababu unatupa uwakilishi wa wannchi katika kushiriki michakato mbalimbali ya maendeleo. ni utumishi mzito kiasi kwamba ni wenye wito tu ndio wanaweza kuutekeleza kwa ufanisi.

msitumie mifano ya walioshindwa kuponda wote waliosalia. tafadhali jamani angalieni maendeleo wabunge mbalimbali waliyofanikiwa kuchochea na kupeleka majiboni mwao kama huduma za maji, zahanati, ujenzi wa shule nk. msiwe negative kila mara.

tuombeane, sie tuko mboni kuelekea majimboni. kwa sasa mikakakti imepamba moto, safari bado ndefu, tuombeane, tutafika tu.

enjoy your week end
 
Back
Top Bottom