Kwenye Taifa linaloongozwa na mtu anayesema hadharani kuwa anayo Frustration,tutegemee kuona mambo makubwa zaidi.

mr mkiki

JF-Expert Member
Sep 22, 2016
5,583
11,659
Tuseme CCM yetu inapendwa sana; inakubalika sana; inachagulika sana; hofu ya inatoka wapi sasa? Matumizi makuubwa ya vyombo vya dola ya nini?

Huwa sielewi issue ya kuzuia maanandamano kama watu hawafanyi fujo, Police should be there kuhakikisha usalama wa watu na fujo hazifanyiki. Otherwise let people practice their rights

Tunapodai Haki Juu Ya Kifo Cha Aquiline Tusisahau Pia Kudai Haki Juu Ya Kifo Cha Salum Muhammed Almasi Mwanafunzi Wa UDSM Aliyepigwa Risasi Na Polisi Mchana Kweupe Huku Akiwa Hana Silaha Yoyote Tarehe 14/5/2017 Na Polisi Kumsingizia Ni Jambazi
DWUf5szXUAMngXe.jpg


Gari limeondolewa plate number unajuaje kama ni la polisi au la watekaji?
DWPkvzhXkAABxci.jpg

Hawataki kuwa traced back. Hiyo ni ishara mbaya sana kwani inaonyesha hao waliomo humo ndani wapo tayari kufanya chochote na hawatajulikana. Likitokea lolote tutaambiwa "Uchunguzi unaendelea".

Kwenye Taifa Linaloongozwa Na Mtu Anayesema Hadharani Kuwa Anayo Frustration, Tutegemee Kuona Mambo Makubwa Na Ya Kusikitisha Zaidi Kuliko Hili Tunalolishuhudia Sasa

mr mkiki.
 
Chama chenu kinaongozwa na muuza ngada mnatarajia lipi jema kutoka kwake?
 
Chama chenu kinaongozwa na muuza ngada mnatarajia lipi jema kutoka kwake?
Nyie mko salama leo ila tambueni yafuatayo:-
1. Wazazi wa Ben Sanane wanalia
2. Familia ya Lissu inalia
3. Mke wa Azory kajifungua huku analia
4. Ndugu wa John wanalia
5. Wazazi wa Acquline ndio sijui wana hali gani
6. Na wengine tusiowakumbuka bado wanalilia wapendwa wao
 
Chama chenu kinaongozwa na muuza ngada mnatarajia lipi jema kutoka kwake?
Ngada hizo mlizoshindwa kuzithibitisha? Hujapona kukurupuka na zilipendwa dogo? Au ile picha ya kumtaja huyu na yule hukuielewa? Kwa taarifa yako ule ulikuwa mchongo wa kuwazuia wauzaji wadogowadogo wasiuze ili yule jamaa yake aliyekuwa na tani moja ausambaze na kuuza wa kwake kwa faida kubwa! Mnafanya siri wakati linajulikana wazi. Mbona kama kweli alikuwa serious kina chid walimgomea na hawakufanywa lolote! Na wale waliosema wameacha nenda mitaa ya stereo pale studio kama hujamkuta anabembea njoo nikupe zawadi! Sanaa kwa wasanii unajichosha!
 
Nyie mko salama leo ila tambueni yafuatayo:-
1. Wazazi wa Ben Sanane wanalia
2. Familia ya Lissu inalia
3. Mke wa Azory kajifungua huku analia
4. Ndugu wa John wanalia
5. Wazazi wa Acquline ndio sijui wana hali gani
6. Na wengine tusiowakumbuka bado wanalilia wapendwa wao
Mawazo pia
 
Back
Top Bottom