Kwenye suala la kuuza mahindi nje Rais Samia aache kumfurahisha Uhuru Kenyatta

Kununua ndege za ATCL mpya hamuwatafuti kuwauliza wakulima maoni yao kama hitaji lao ni ndege zisizo na manufaa kwao au kitu kinachowagusa kama ruzuku ya pembejeo na soko la ndani lenye bei nzuri ndiyo suala muhimu na nyeti kwao.

September 14, 2021

CPB Yajipanga kutafuta mikopo ili Kununua Mahindi ya Wakulima Kwa Bei ya Soko - Dr. Moshi


Source : KILIMO TV
 
Mkuu
Njia pekee serikali inaweza kudhibiti mahindi kwenda nje ninpale itakapoamua kununua mahindi hayo direct kwa mkulima na huku ikihakikishq kuwa inampatia ruzuku kwenye pembejeo.
Serikali haimsaidii chochote mkulima anapo bet na pesa yake shambani, halafu inataka kuja ku control soko lake ,
serikali akitangaza bei nzuri nani atauxa Kenya?
 
Mtoa mada itakua vizuri ukinunua maindi yako saivi uyahifadhi ili njaa isikupate, wao waache wauze kenya hukuwasaidia kuyalima usiwapangie pakuuza
 
Ukweli ni uonevu kunizuia kuuza ninakotaka zao ambalo nimetaabika nalo mathalan miezi 7-10.

Napata hasira sana. Nimeamua kumwagilia mahindi ya kuchoma ekari moja kwa hesabu ya kuuza mahindi mabichi 19,000 kuuza kila moja shs 200 ili nipate Shs 3,800,000.

Anatokea mtu aitwae kiongozi anatoa amri hakuna kuuza mahindi mabichi.

Wapi tuliwekeana mkataba mimi mkulima nilishe wengine?

Kwanini isiwe ni jukumu la serikali kununua mahindi kwa wakulima wenye ziada na kuwasaidia wenye njaa?

Nikiamua kuzalisha mahindi ya kuchoma tumeni viongozi waje kunikagua kama sina akiba ya kutosha mwaka mzima mimi na kaya yangu.

Kunizuia kuuza nilichotaabikia ni dhulma.
 
Ukiangalia Biashara ya kuuza nafaka Kenya hasa Mahindi imejikita kufurahisha Wakenya zaidi na hasa Raisi wao.

Kwa Mujibu wa vituo vya hali ya hewa Duniani, swala la ukame hasa ukanda wa Africa Mashariki linatarajia kuwepo hata mwakani na huenda tukushahudia mvua chache sana za Masika na ukame wa kutisha kabisa.

Kuendelea kuuza Mahindi Kenya ni kutafuta Balaa ni bora Serekali ikaangalia jinsi ya kuongeza Bei na yale Maghala ya Taifa yanunue mahindi kwa wingi sana.

Tukiendelea kuwafurahisha Wakenya tujiandae Mwakani kununua mahindi kutoka nje tena hao hao Wakenya watatuuzia.

Nazani wote tunakumbuka 2017 kipindi Magufuri RIP anaombwa chakula barabarani na wananchi.

Hii lugha - "kumfurahisha" - ina ukakasi
 
Serikali walilima hayo mahindi? Tatizo sio ukame ni vita ya ukrane, isitoshe bei yetu iko chini ukilinganisha na marekani
 
Back
Top Bottom