Kwenye suala la Chanjo wasomi wetu nao wana sehemu ya lawama

Kilemakyaaro

JF-Expert Member
Jul 19, 2016
5,050
5,078
Inashangaza sana tuna Taasisi za Utafiti wa magonjwa na Afya ya binadamu kama NIMR na IFHI, tuna vyuo vikuu vya tiba na huko kote kuna wasomi wanaojiita wabobezi na wa watafiti, nimejiuliza sana wakati hao wasomi wa Kizungu wanalala na kuamkia Maabara hawa wa kwetu wao wanafanya nini?

Sijawahi kusikia ni zao gani la tafiti zao ktk tiba limesaidia kuondoa changamoto ktk jamii yetu iwe ni ya Homa ya Dengue ama chochote. Sasa nnajiuliza usomi wao una faida gani kwa jamii yetu?

Jambo la kushangaza ni pale hata wale tunaowaamini wakiwa na majina makubwa na Uprofesa na Udokta wao sasa wamegeuka wapiga ramli, yaani wanatuchanganyia viungo vya mboga wanaziita ni dawa, wengine wameenda mbali wameamua kutuambia eti wana mashine za kujifukiza tena ktk Taasisi kubwa za tiba, yaani unamuangalia Professor akiongea unashindwa kumtofautisha na mwanafunzi wa vidudu, kweli yaan wasomi wetu tunawatofautisha vipi na kina Mwaka ama yule bwa majini wa mabibo?

Yapo mambo yakisemwa na mtu unaetegemea aje na suluhu za kisayansi unapata Ganzi kama kweli hawa wasomi wako serious au kama na wao wana machapisho ktk majirida makubwa ya dunia ya sayansi ikiwa yeye anaiambia jamii inayomtegemea ikajipashe moto kutibu maradhi makubwa.

Mimi nnadhani ifike mahala ikiwezekana kuwepo sheria inayowalazimisha wasomi wetu kuja na majawabu ya kisomi kwenye changamoto za kijamii au laah waondolewe huko wakafanye kazi zingine kuliko kujiaminisha tuna vichwa msaada kumbe tuna wachanganya viungo ambavyo hata Marehemu babu yangu alifanya akiwa hajakanyaga hata darasa moja. Inatia kinyaa now days kumsikiliza Profesa akiongea kuliko hata mwanangu wa vidudu
 
Aisee tuna jambo kubwa tunalotakiwa kufanya maana sasa ni fedheha, ikiwa kama Taifa tumeshatilia shaka chanjo za wenzetu jambo ambalo linaweza kua na nia njema tu, sisi tunafanyaje ili tupate ya kwetu ikiwa wasomi wetu wapo kama sisi wengine tuliosoma kiswahili tu, yaani Mungu tu anatupenda na kutuepusha na baadhi ya mabalaa vinginevyo tungeisha
Mkuu Tanzania hakuna wasomi, bali kuna wenye makaratasi (vyeti) tu yanayooneshq wamesoma.
 
Tutajie tafiti na papers ulizosoma za hawa wataalamu., hata tano tu
 
Dawa ya NIMRCAF unaijua?

COVIDOL?
UNADOL ya UDSM je?

Tupe product moja tu ya mwanao wa vidudu
Scientifically imekuwa proved wapi? Unapoita dawa unamaanisha nini wakati mpaka leo hakuna cure ya Corona virus??
 
Inashangaza sana tuna Taasisi za Utafiti wa magonjwa na Afya ya binadamu kama NIMR na IFHI, tuna vyuo vikuu vya tiba na huko kote kuna wasomi wanaojiita wabobezi na wa watafiti, nimejiuliza sana wakati hao wasomi wa Kizungu wanalala na kuamkia Maabara hawa wa kwetu wao wanafanya nini?

Sijawahi kusikia ni zao gani la tafiti zao ktk tiba limesaidia kuondoa changamoto ktk jamii yetu iwe ni ya Homa ya Dengue ama chochote. Sasa nnajiuliza usomi wao una faida gani kwa jamii yetu?

Jambo la kushangaza ni pale hata wale tunaowaamini wakiwa na majina makubwa na Uprofesa na Udokta wao sasa wamegeuka wapiga ramli, yaani wanatuchanganyia viungo vya mboga wanaziita ni dawa, wengine wameenda mbali wameamua kutuambia eti wana mashine za kujifukiza tena ktk Taasisi kubwa za tiba, yaani unamuangalia Professor akiongea unashindwa kumtofautisha na mwanafunzi wa vidudu, kweli yaan wasomi wetu tunawatofautisha vipi na kina Mwaka ama yule bwa majini wa mabibo?

Yapo mambo yakisemwa na mtu unaetegemea aje na suluhu za kisayansi unapata Ganzi kama kweli hawa wasomi wako serious au kama na wao wana machapisho ktk majirida makubwa ya dunia ya sayansi ikiwa yeye anaiambia jamii inayomtegemea ikajipashe moto kutibu maradhi makubwa.

Mimi nnadhani ifike mahala ikiwezekana kuwepo sheria inayowalazimisha wasomi wetu kuja na majawabu ya kisomi kwenye changamoto za kijamii au laah waondolewe huko wakafanye kazi zingine kuliko kujiaminisha tuna vichwa msaada kumbe tuna wachanganya viungo ambavyo hata Marehemu babu yangu alifanya akiwa hajakanyaga hata darasa moja. Inatia kinyaa now days kumsikiliza Profesa akiongea kuliko hata mwanangu wa vidudu
Upo sahihi kuhoji mchango wa wasomi wa nchi yetu katika nyanja mbalimbali za maisha ya mtanzania.

Ila usomi au wasomi ni tasnia pana sana. Tunao wasomi wachumi (umeshawahoji kwa nini nchi yetu ni miongoni mwa nchi duni sana kiuchumi?), tunao wasomi mainjinia (umewahoji kwa nini miradi yote mikubwa ya nchi hii contractors wanatoka uchina na nchi nyinginezo za nje?), tunao wasomi wanasiasa (umewahi kuwahoji kwa nini uongozi wao umekuwa na tija hafifu sana kwa maendeleo ya nchi yetu tangi uhuru?)

Anyway, jibu la hayo yote ni kwamba huwezi kuwalaumu kiujumla "wasomi" wa nchi hii bila kuweka bayana unazungumzia wasomi wapi na ngazi gani ya usomi.

Pia siyo haki kuwatuhumu "wasomi" hao kwa mambo yaliyo nje ya uwezo wao. Kama unajaribu kulinganisha mchango wa wanasayansi waliochangia kutengeneza chanjo za corona huko nchi za ng'ambo na mchango wa wanasayansi wetu, basi watengenezee wasomi wetu wanasayansi mazingira yale yale waliyo nayo wenzao wa huko ng'ambo. Usione vyaelea!
 
Mkuu Tanzania hakuna wasomi, bali kuna wenye makaratasi (vyeti) tu yanayooneshq wamesoma.
... Wawinda teuzi hao watembelee ma V8 hayo mengine is up to you. Corona isipowazindua hamtakaa mzinduke milele.
 
Wasomi wetu wengi wanakariri madesa tu wafaulu mtihani ukibisha kafie Yanga.

Usitegemee kupata vitu kama chanjo toka kwao.

Kingine wana stresa na ukata wa pesa asikae awaze pesa na ajira, aje kuwaza chanjo ya covid
 
Upo sahihi kuhoji mchango wa wasomi wa nchi yetu katika nyanja mbalimbali za maisha ya mtanzania.

Ila usomi au wasomi ni tasnia pana sana. Tunao wasomi wachumi (umeshawahoji kwa nini nchi yetu ni miongoni mwa nchi duni sana kiuchumi?), tunao wasomi mainjinia (umewahoji kwa nini miradi yote mikubwa ya nchi hii contractors wanatoka uchina na nchi nyinginezo za nje?), tunao wasomi wanasiasa (umewahi kuwahoji kwa nini uongozi wao umekuwa na tija hafifu sana kwa maendeleo ya nchi yetu tangi uhuru?)

Anyway, jibu la hayo yote ni kwamba huwezi kuwalaumu kiujumla "wasomi" wa nchi hii bila kuweka bayana unazungumzia wasomi wapi na ngazi gani ya usomi.

Pia siyo haki kuwatuhumu "wasomi" hao kwa mambo yaliyo nje ya uwezo wao. Kama unajaribu kulinganisha mchango wa wanasayansi waliochangia kutengeneza chanjo za corona huko nchi za ng'ambo na mchango wa wanasayansi wetu, basi watengenezee wasomi wetu wanasayansi mazingira yale yale waliyo nayo wenzao wa huko ng'ambo. Usione vyaelea!
... Takwimu ni zao muhimu sana la research. Research hazifichwi makabatini.
 
Sometimes huwa nawaza kuwa watanzania hawajui nini kinatakiwa kufanywa ili kuweka mazingira wezeshi ya tafiti za kimaendeleo, Research and Develepment au R&D. Ni hivi R&D ni uwekezaji kama uwekezaji mwingine wowote. Nchi zilizoendelea huwekeza hadi 10% ya GDP kwenye R&D, yaani matrillioni ya dola humwagwa kwa wanasayansi kufanya tafiti tu. Ikiwemo hata kujenga miundo mbinu ya kufanyia tafiti. Sasa hapa Tanzania tulijiwekea walau 1% ya GDP iende kwenye tafiti, lakini nenda kaulize taasisi zetu za utafiti zilipokea sh ngapi mwaka 2020 na tembelea hali halisi ya maabara za kufanyia tafiti. Halafu mnakuja hapa kulaumu tu wanasayansi wetu.
 
Hizo ulizotaja ni dawa? Zimethinitishwa wapi na nani? Au nawe mbeba tunguli tu, yaani unaandika mchanganyiko wa mbogamboga ndio unaita dawa ebu acha utani bwana
Dawa ya NIMRCAF unaijua?

COVIDOL?
UNADOL ya UDSM je?

Tupe product moja tu ya mwanao wa vidudu
 
We uliesoma tueleze hapa na matokeo yake acha kujificha nyuma ya paper, paper hata zingejaa matani kama hazina products ya kutatua changamoto ni makabrasha hewa kama mengine
Tutajie tafiti na papers ulizosoma za hawa wataalamu., hata tano tu
 
Na mimi sijalaumu kiujumla, nimekua very specific kwenye eneo moja tu la Afya, na pia sijalaum nimewapa changamoto muhimu ili waje na majibu muafaka kusaidia Taifa na kumsaidia Rais sio tunahaha tu wakati kuna watu wanajiita ma Proff wapo wanajisifia tu

Back
Top Bottom