Kwenye sekta ya Madini - huu ni uwekezaji au ni ukwapuaji? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwenye sekta ya Madini - huu ni uwekezaji au ni ukwapuaji?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Juaangavu, Mar 16, 2011.

 1. Juaangavu

  Juaangavu JF-Expert Member

  #1
  Mar 16, 2011
  Joined: Nov 3, 2009
  Messages: 915
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Wachumi tusaidieni kutafakari hizi takwimu: Mnamo mwaka 1998 - uzalishaji wa madini Tanzania ulikuwa chini ya tani 1 na mchango wake ktk pata la taifa ulikuwa ni 2%; na mara baada ya kupokea wawekezaji wengi ktk sekta hii kufikia mwaka 2005 uzalishaji ulikuwa ni zaidi ya tani 50 na mchango wake ktk pato la taifa ni 3.5%. Wataalam wa mahesabu tusaidieni hapo kuna uwiano wowote; nany watalaam wa uchumi mtusaidie kuelewa sarakasi ya hizi namba.

  Hivi haya madini yangeliendelea kubaki huko chini ili hali tunajipanga sisi wenyewe ili tuweze kuyachimba yangilioza au vipi.
  Gonga hapa upate details:

  Ministry of Energy and Minerals - Documents - Mineral Sector
   

  Attached Files:

 2. Juaangavu

  Juaangavu JF-Expert Member

  #2
  Mar 16, 2011
  Joined: Nov 3, 2009
  Messages: 915
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Kwa mchango wa namna hii kwa pato la taifa, ndo maana Nyerere alitamani tuvune kwanza misitu ili hali tukijijengea uwezo kama taifa wa kuvuna rasilimali zilizoko chini ya ardhi.
   
 3. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #3
  Mar 16, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,782
  Likes Received: 2,392
  Trophy Points: 280
  Tunaibiwa sana!
   
 4. Juaangavu

  Juaangavu JF-Expert Member

  #4
  Mar 16, 2011
  Joined: Nov 3, 2009
  Messages: 915
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35

  Mi binafsi natamani kulia. Kwani tungetumia VETA ikasaidia vijana kufanya uchimbaji mdogo mdogo wakia na zana ambazo zimeboreshwa zaidi; na angalau tukaongeza uzalishaji toka hiyo tani moja angalu zikafika hata nne kwa mwaka. Na pia serikali ikaboresha soko la ununuzi wa hayo madini; kwa kuwa hicho kipato kingelikuwa kinaingia kwenye mifuko ya watz wenzetu mchango wa haya madini ungekuwa zaidi ya hiyo 3.5% (kwa zaidi ta tani 50). Mungu na atusamehe; tumeamua kutupa rasilimali zetu wenyewe kama vile zina upupu
   
 5. mbogo31

  mbogo31 JF-Expert Member

  #5
  Mar 16, 2011
  Joined: Nov 28, 2008
  Messages: 687
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Hii yote inatokana na ubinafsi wa viongozi walioshikilia Dola, Kwa nini tusingekopa ili tuwekeze sisi wenyewe na kulipa taratibu, maana hata hayo makampuni yanayowekeza yanakopa mitaji, na Wataalam katika migodi yote ni sis vijana wakitanzania, sasa unashangaa wakina Ngeleja wanacheka cheka tu kwa kuwa wamo kwenye payroll za hawa wawekezaji wanyonyaji. na ndio maana wanajeuri ya hata kutunyanyasa, wanakuja kutoka kwao hawana pesa wanatajirikia hapa kwetu na wanatubagua katika ardhi yetu!, tembelea migodini uone wafanyakazi wanavyobaguliwa kwa rangi zao. ni hatari sana.

  Wnapata kipato kikubwa sana hawa jamaa, na kwa kuwa serikali ipo mifukoni mwao haiwezi kuongea ukweli.
   
 6. F

  Froida JF-Expert Member

  #6
  Mar 16, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Unaambiwa huko Liganga tayari makaburu wameanza kukimbiza makaa ya mawe kupitia Mbamba Bay- malawi ,wananchi wanshangaa yanavyovunwa kwa haraka ,nchi ya mazuzu italiwa mpaka imalizwe
   
 7. Juaangavu

  Juaangavu JF-Expert Member

  #7
  Mar 16, 2011
  Joined: Nov 3, 2009
  Messages: 915
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35

  Hakika huo unaweza kuwa ni mzizi wa tatizo, sijui dhamira zao zimekufa au vipi! Makanisa na misikitini wanahudhuria kwa wingi na wanatoa michango mikubwa mikubwa, lakini inapokuja kwenye masuala ya kulisaidia taifa kwa ujumla inakuwa kama vile ni misukule.
   
 8. Juaangavu

  Juaangavu JF-Expert Member

  #8
  Mar 16, 2011
  Joined: Nov 3, 2009
  Messages: 915
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Ooh! Ina maana intelenjensia inaishia kwa watanzania peke yake. Wapo wapi wana usalama ili waweze kuzuia hii hali.
   
 9. mbogo31

  mbogo31 JF-Expert Member

  #9
  Mar 16, 2011
  Joined: Nov 28, 2008
  Messages: 687
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Hawawezi kuzuia, hivi hufahamu kwamba wakati Mali ikiwa inasafirishwa kutoka mgodini walinzi huwa ni FFU wetu! yaani Helicopter hutua chini ya ulinzi mkali wa FFU! jamaa (Wazungu hasa Makaburu) wanapakia mzigo na helicopter inaruka no ukaguzi no what! sasa shanga data wanapata wapi kwamba ton kazaa zimezalishwa na zimepelekwa nje! Na hawa ndugu zetu FFU wapo tayari kukuchapa risasi ukikatiza tu hata kwa bahati mbaya wakati wa zoezi, na wakati katika nchi hii nafikiri hawa jamaa ndio wanalipwa kiduchu saaaana! Inashangaza kuona mali amabayo ingelitumiwa vizuri ingeongeza hata kipato chao wanailinda wakati ikiibwa mchana kweupeee.
   
 10. Juaangavu

  Juaangavu JF-Expert Member

  #10
  Mar 16, 2011
  Joined: Nov 3, 2009
  Messages: 915
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Duh! Sijui tufanyeje, kumbe ndo maana tunaambiwa na wana siasa wa upande wa pili kuwa tutabaki na maandaki pale reserves za madini yetu zitakapokwisha.
  Afrika nakulilia afrika, afrika nakulilia afrika.
   
 11. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #11
  Mar 16, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  mkuu uwe unaandika vitu vya uhakika. msikitini hakuna michango ya aina hiyo inayoingia labda huko kwenu makanisani. kwani wengi wa wanaoiba na jamii yenu (ambao wako kwenye system nyonyaji tangu unaoitwa uhuru) na hata hao ambao wanaiba na wangetoa michango labda huko misikitini huwa hawaendi zaidi ya kuishia bar na nyinyi. so please do re-read, usiandike tu kwasababu unataka kujifurahisha.
   
 12. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #12
  Mar 16, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Kaka ililie Tanzania yako ambayo ndio uozo umezidi, angalau nchi nyingine za Africa zinaanza kujiondoa mtabaki Watanzania wenyewe.
   
 13. Juaangavu

  Juaangavu JF-Expert Member

  #13
  Mar 16, 2011
  Joined: Nov 3, 2009
  Messages: 915
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Nikilia mimi mwenyewe sijui kama hata machozi yangu yatawashitua hawa walo-amua kuifanya tz kuwa shamba la bibi. Kitu zaidi kinatakiwa kufanyika ktk taifa hili
   
 14. m

  matawi JF-Expert Member

  #14
  Mar 16, 2011
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 2,055
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Jua angavu umeongea kitu cha ukweli lakini kinauma, ningejua nisingefungua jf leo yaani siku imeharibika
   
 15. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #15
  Mar 16, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,762
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145

  mkuu usiwe kama pinda kulia do something! tuwaondoe haya MAFISADI TUU!
   
 16. Juaangavu

  Juaangavu JF-Expert Member

  #16
  Mar 16, 2011
  Joined: Nov 3, 2009
  Messages: 915
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  <br />
  <br />

  Nimeacha kulia. Hivi Tahir square ya bongo ipo wapi tukajikusanye hapo mpaka kieleweke! Haiwezekana tukawa shamba la bibi kiasi hiki.
   
Loading...