Kwenye msiba wa mwizi lazima vibaka wawepo

Habari wakuu,

Niende kwenye kisa moja kwa moja.

Hapa jirani yangu kuna kijana alikuwa ana jishughulisha na kazi ya wizi,sasa si mnajua siku za mwizi ni 40, sasa jana kaingia sehemu mbaya wakambananisha, akala kichapo heavy hadi kupelekea Kifo

Sasa tukiwa msibani mara kibaka kafanya jaribio la kuiba simu; wazee wakamshitukia, kala kichapo mixer kukatwa mikono

Nb: Wazazi tuwe makini na watoto wetu, maisha au shughuli zisitufanye kusahau majukumu ya malezi ya watoto wetu.
Kuna jamaa alikuwa anaishi tegeta wazo, jamaa bonge la mtanashati, anajipenda kinoma. Madem wanampenda sana ila story za chini chini ikawa wanasema ni mwizi wa boxer na bajaj. baba yake ni mtu mwenye pesa ya kawaida yani gari tatu nyumba kadhaa fremu za kupangisha moja kampa dogo afanye biashara ya kukodisha vifaa vya mziki kwenye shughuli.

Dogo alikuwa na wanawake si chini ya watano na wote kawapangishia anawalisha. Pale ofisini kwake vitoto vyote vya mtaani vilivyonyoa kiduku ndipo yalikuwa makazi yao. Alikuwa anafahamiana na vibaka wote mtaani na alikuwa ana principal moja hakuna kuiba mtaani. Ikitokea vile vitoto vimeiba mtaani habari zikamfikia anaongozana na jeshi lake kwenda kumsaka huyo aliyeiba mtaani anampiga mpaka nusu kumtoa roho.

Za mwizi ni arobaini, siku moja nasikia kaenda tabata kuiba pikipiki, kaiba deal ikaenda ovyo wakamfukuza, wakamkamata wakapiga na kuua. Sasa kwenye msiba wake ilikuwa ni kufuru. Vibaka wote wa tegeta wazo madem wanalia viabaka ndo wanabeba jeneza. Kufika makaburini wakamfukuza Sheikh, mazishi wakaendesha wenyewe, kaburini wakamwaga karata maana alikuwa mecheza kamari.

Aliyenitia simanzi ni demu wake mmoja akawa analia eti, "Masikini jana kanipigia niende chukua pesa ya kodi, nikajifanya niko busy nitaifuata leo sasa kafa jamani mimi nitaendawap".
 
Kulikuwa na haja gani ya kumdhulumu iyo nafsi ya huyo mwizi? Roho mbaya tu. Tanzania kila mtu ni mwizi kwenye nafasi yake. Hata wewe mleta mada ni mwizi vilevile kwenye nafasi yako. Mnafanya vibaya sana mkiwapiga na kuwatesa wezi wenzenu. Kuna sheria za nchi akamatwe apekekwe polisi na Sheria itafuata mkondo wake. Wote nyinyi ni maboriti.
Mkuu umewahi kuibiwa?
 
Kuna jamaa alikuwa anaishi tegeta wazo, jamaa bonge la mtanashati, anajipenda kinoma. Madem wanampenda sana ila story za chini chini ikawa wanasema ni mwizi wa boxer na bajaj. baba yake ni mtu mwenye pesa ya kawaida yani gari tatu nyumba kadhaa fremu za kupangisha moja kampa dogo afanye biashara ya kukodisha vifaa vya mziki kwenye shughuli.

Dogo alikuwa na wanawake si chini ya watano na wote kawapangishia anawalisha. Pale ofisini kwake vitoto vyote vya mtaani vilivyonyoa kiduku ndipo yalikuwa makazi yao. Alikuwa anafahamiana na vibaka wote mtaani na alikuwa ana principal moja hakuna kuiba mtaani. Ikitokea vile vitoto vimeiba mtaani habari zikamfikia anaongozana na jeshi lake kwenda kumsaka huyo aliyeiba mtaani anampiga mpaka nusu kumtoa roho.

Za mwizi ni arobaini, siku moja nasikia kaenda tabata kuiba pikipiki, kaiba deal ikaenda ovyo wakamfukuza, wakamkamata wakapiga na kuua. Sasa kwenye msiba wake ilikuwa ni kufuru. Vibaka wote wa tegeta wazo madem wanalia viabaka ndo wanabeba jeneza. Kufika makaburini wakamfukuza Sheikh, mazishi wakaendesha wenyewe, kaburini wakamwaga karata maana alikuwa mecheza kamari.

Aliyenitia simanzi ni demu wake mmoja akawa analia eti, "Masikini jana kanipigia niende chukua pesa ya kodi, nikajifanya niko busy nitaifuata leo sasa kafa jamani mimi nitaendawap".
Duuh umenikumbusha kisa flani! Hawa vibaka huwa ni shida sana wanapoenda kuzika! Kwanza wanakuwa wengiii na boda boda zao! Humo barabarani ni vurugu tupu. Kuna wengine walikuwa wanaenda kumzika mwenzao wametokea Goba wanaenda malamba, si wakafunga barabara pale Mbezi mwisho njia panda ya Goba! Wakasimamisha magari yoote wakakaa kati kati ya barabara vurugu tupu! Bahati nzuri polisi wa gogoni walipata taarifa mapema dakika sifuri FFU wakaja kuwatawanya na walifanikiwa kuwakamata wa kutosha tu!! Ni shida sana...

NB:sina huruma na wezi
 
Wezi si watu wazuri aisee maana anaweza kutoa roho ama kukurudisha nyuma.

Ila wazazi inabidi kufuatilia watoto. Kuna jamaa yangu mtu mzima sana ana kijana ana miaka 19. Alikuwa anasema watoto wa majirani anamsifia mwanae kuwa mtulivu. Kumbe jamaa mwizi wa boda boda na bajaj. Jamaa alikuja kujua dogo sijui waliiba wapi wakanaswa. Jamaa akasema haendi kumtoa dogo kakaa alivyo mafia walikuwa wanampeleka sijui akawaonyeshe wenzake, akaiwa kwenye gari akaruka na pingu akakimbia mpaka leo mwaka wa pili haijulikani yuko wapi
 
😂😂😂😂😂😂

Ila bro mwizi anakera sana. Hawa vibaka wa mtaani wakikukuta kwa 18 zao wanaweza hata kukuchoma visuu au bisibisi. Wezi wanarudisha nyuma sana maendeleo yetu.
Jambazi anaibia wale wanaofaa kuiba...matajiri,mabank,wadosi.
Lakini vibaka wanawaibia sisi masikini kapuku wenzao watembea kwa miguu.
 
Back
Top Bottom