Kwenye mkutano wa Berlin Conference, nani alipewa Tanganyika?

enery

JF-Expert Member
Aug 21, 2015
368
437
Naomba kupata ufafanuzi wakati wanagawana bara la Afrika nani alipewa Tanganyika, na Muingereza alipewa kututawala ama kutusimamia mpaka tukipata uwezo wa kujisimamia wenyewe ama?

Nashindwa elewa hapo, je uhuru tuliupata baada ya mjeruman kunyang'anywa na muingereza akapewa kutusimamia tu ama atutawale?
 
Umewezaje kufungua a/c jf pasipo kujua iyo historia.
Baada ya mkutano wa Berlin Ujerumani alijichukulia tanganyika ikiwamo burundi na rwanda, baada ya vita vya pili vya dunia mjerumani akaporwa makoloni yake. Tanganyika akapewa uingereza kuisimamia, rwanda na burundi wakapewa ubelgiji.
 
Tanzania mwingeleza hakuwa mkoloni yeye alikuwa msimamizi hadi tukijielewa
 
Tanzania mwingeleza hakuwa mkoloni yeye alikuwa msimamizi hadi tukijielewa
Asante, kwaiyo kwanini wanatuambia uhuru tumeupata 1961 na sio baada ya vita ya pili ya dunia kuna nini nyuma hapo kinafichwa napatwa na mashaka sana
 
Duh. Kwahali hii bado tunasafari ndefu make hata anaemsaidia mwenzio nae anaenda chaka.Mjeruman alitolewa baada ya vita yakwanza ya dunia ndipo muingereza alipopewa kuwa msimamizi na mdhamini wa Tanganyika
 
Umewezaje kufungua a/c jf pasipo kujua iyo historia.
Baada ya mkutano wa Berlin Ujerumani alijichukulia tanganyika ikiwamo burundi na rwanda, baada ya vita vya pili vya dunia mjerumani akaporwa makoloni yake. Tanganyika akapewa uingereza kuisimamia, rwanda na burundi wakapewa ubelgiji.
Ni vita ya kwanza mkuu sio vita vya pili.
 
Berlin conference pale Tanganyika..Rwanda na Burundi alipewa Mjerumani...(German East Africa)...Baada ya vita ya kwanza ya dunia 1918 kumbuka wazungu walikaa pale Indonesia na kusaini mkatab wa amani katik mji wa Versailes na kuamua kumuadhibu mjerumani kwa kuanzisha vita ile..
Adhabu mojawapo ilikuwa ni kumpokonya makoloni yake yote kwahyo na Tanganyika ikiwemo...Lakini makoloni hayo yakawekwa chini ya uangalizi maalum ili baadae yajitawale na Tanganyika ikawekwa chini ya Mwingereza...huo ni mwaka 1919...
Kama sikosei mwaka 1920 ndo jina Tanganyika likaanza kutumika rasmi....mwaka 1926 gavana Donald Cameroon akaanzisha bunge la Tanganyika wakati huo likiitwa LEGCo...Legislative Council...ni historia ndefu...
 
Naomba kupata ufafanuzi wakati wanagawana bara la Afrika nani alipewa Tanganyika, na Muingereza alipewa kututawala ama kutusimamia mpaka tukipata uwezo wa kujisimamia wenyewe ama? Nashindwa elewa hapo, je uhuru tuliupata baada ya mjeruman kunyang'anywa na muingereza akapewa kutusimamia tu ama atutawale?

Mtoa mada fuatana na Mimi ktk historia ya Tanganyika na bara La afrika,Kwanza nianze kwakukufahamisha kuwa Bara la afrika limepata kutawaliwa na Mataifa saba tu ambayo ni Italia,Ufaransa,ujerumani,ureno,ubeligiji,uhispania,Uingereza, baada ya mkutano wa kuligawa bara la Afika,mnamo 1884/85 Tanganyika,Togo,Namibia,etc zilipewa kwa mjerumani,hadi 1919 Tanganyika ilikuwa chini ya ujerumani lkn mwaka huo huo 1919 Mara baada ya vita vya kwanza vya dunia 1914-18 wakubwa wadunia hasa wakuu Wa magaribi wakilishikiana na marekani (kumbuka kabla ya vita vya pili vya dunia kuisha 1945 bado ulaya ilikuwa na nguvu hasa Uingereza) hivyo rais wa USA anapendekeza Hoja 14 kujadiliwa ktk mji wa versalies nchi ufaransa ktk mambo waliozungumza wakakubaliana kuwa ujerumani ndiye aliyekuwa chanzo cha vita kuu ya kwanza ya dunia na anatakiwa apewe adhabu na Moja ya adhabu ni kuchukuliwa makoloni yake,Tanganyika ikiwemo,Ndipo ktk hoja zile kumi na mne zilizoletwa mezani ya kumi na mne ilitaka uundwe umoja wa kuepusha vita nyingine kutokea na umoja huo huwe mwangalizi Wa yale makoloni waliyoyatoa kutoka kwa mjerumani kwa uangalizi maalum(mandate territory) ndipo umoja huo ukaanzishwa Na kuitwa shirikisho la Kimataifa (league of Nation) na umoja huo ukaporomoka na Mnamo mwaka 1945 ukaundwa umoja uliorithi mambo mengi ya shirikisho LA awali(LN) Moja ya mambo ilikuwa hilo la kuamisha makoloni yale na kuitwa Trustship territory ndio maana Uhuru wa Tanganyika Nyerere alienda UNO umoja wa mataifa kudai hiyo hati na muingereza akawa hana ujanja tukapewa Uhuru kwa ufupi Uhuru wetu ni wa briefcast kama asingekuwa Nyerere hata wewe mtoa Uzi ungeleta Uhuru asante Vevenononombo2016
 
Berlin conference pale Tanganyika..Rwanda na Burundi alipewa Mjerumani...(German East Africa)...Baada ya vita ya kwanza ya dunia 1918 kumbuka wazungu walikaa pale Indonesia na kusaini mkatab wa amani katik mji wa Versailes na kuamua kumuadhibu mjerumani kwa kuanzisha vita ile..
Adhabu mojawapo ilikuwa ni kumpokonya makoloni yake yote kwahyo na Tanganyika ikiwemo...Lakini makoloni hayo yakawekwa chini ya uangalizi maalum ili baadae yajitawale na Tanganyika ikawekwa chini ya Mwingereza...huo ni mwaka 1919...
Kama sikosei mwaka 1920 ndo jina Tanganyika likaanza kutumika rasmi....mwaka 1926 gavana Donald Cameroon akaanzisha bunge la Tanganyika wakati huo likiitwa LEGCo...Legislative Council...ni historia ndefu...
upo sawa kk ila mji wa versailles haupo Indonesia upo france
 
kwa mantiki hii kama mwingereza alipewa kujumu la kutusimamia tu na si kututawala basi yatakiwa tumdai vyote alivyobeba wakati huo atulipe mana hatukuwa joloni lake
 
Berlin conference pale Tanganyika..Rwanda na Burundi alipewa Mjerumani...(German East Africa)...Baada ya vita ya kwanza ya dunia 1918 kumbuka wazungu walikaa pale Indonesia na kusaini mkatab wa amani katik mji wa Versailes na kuamua kumuadhibu mjerumani kwa kuanzisha vita ile..
Adhabu mojawapo ilikuwa ni kumpokonya makoloni yake yote kwahyo na Tanganyika ikiwemo...Lakini makoloni hayo yakawekwa chini ya uangalizi maalum ili baadae yajitawale na Tanganyika ikawekwa chini ya Mwingereza...huo ni mwaka 1919...
Kama sikosei mwaka 1920 ndo jina Tanganyika likaanza kutumika rasmi....mwaka 1926 gavana Donald Cameroon akaanzisha bunge la Tanganyika wakati huo likiitwa LEGCo...Legislative Council...ni historia ndefu...
Versailes ipo Ufararansa mkuu acha kutupiga fix
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom