Kwenye majanga tuacheni tukeshe ninyi mkalale.

MWITONGO MAARIFA

JF-Expert Member
Aug 11, 2018
276
1,428
Mara itokeapo misiba na majanga mengine katika jamii wapo wanaojisikia kulala na wengine ukesha na kufanya juhudi zote kutatua janga lililoifika jamii.

Wanaokwenda kulala si kwamba hawana uchungu bali nafsi zao uwatuma hivyo na si busara kuwalazimisha wawepo kwenye mkesha maana watalala tu, busara nikuwaruhusu wakalale na ninyi wenye Nia na moyo wa kukesha mkaendelea kukesha.

Niwakumbushe pia miaka ya nyuma kuliwahi kutokea njaa kali hadi baadhi ya familia zikawa zinabandika mawe jikoni na watoto kuchochea moto wakiamini wanapika chakula kumbe wanapika mawe. Wazazi waliokuwa wanafanya hivyo hawakufanya kwa kupenda bali walifanya kwa ajili ya kuwapa moyo watoto walale siku zisogee na kuwaondoa watoto katika lindi la mawazo ya njaa.

Naamini katika janga lililotokea ziwa Victoria serikali ina sababu za msingi za kusitisha uokoaji lakini sababu kuu waliuotoa si sababu inayoweza kutolewa na mzazi kwa familia yake na ni sababu ya kibaguzi na isiyokuwa na utu ndani yake "GIZA".

Kuna watu wana wapendwa wao kwenye maji na wapo tayari kutumia juhudi zozote kuwaokoa iwe Giza au mwanga, endapo kundi flani la watu liliamini usiku Ni muda wa kulala walipaswa kujua wapo ambao kwao usiku wa leo hawapati usingizi na wangependa kukesha ziwani kusaka ndugu zao. Kuwatangazia kuwa usiku ni muda wa kupumzika wakalale Hadi kesho wakati unajua kabisha wana mitumbwi na vifaa mbalimbali vyenye mwanga nikuangamiza ndoto za kuwaona upya ndugu zao. Hi ni sawa na kuwaambia ndugu zenu hatunao tena Duniani bila kuwapa miili yao.

Nimalizie kwa kuuliza, hiyo boti ingekuwa na kundi flani la watu ambao tunaamini niwakubwa aidha kiuchumi, kimadaraka au vinginevyo tungelala?Ingekuwa imebeba watalii au kundi la wageni wa mataifa ya kigeni tungekwenda kulala?

Wakati mwingine ni Bora kukaa kimya na kuwasikiliza watu wanataka nn kuliko kuwaamulia watu kila kitu kulingana na unavyoona wewe.
 
Back
Top Bottom