Kwenye mahojiano na Wasafi TV, Polepole kaupiga mwingi

2025 CCM itakataliwa na nguvu kubwa upande wa Kanda ya ziwa...
Unajua mtwara na mzozo wa gesi walikua wamoto kuliko hyo kanda ambayo geita,kagera,shinyangana mwanza wanainyooshea chato kama ndiko waliko wapendwa wa jpm
Subiri ujionee màajabu ya 2025 Ccm hawajawahi kuona uchaguzi mgumu siku zote na popote pale
 
Kwa hiyo CCM na serikali yake ni genge lililojaa wahuni?
Mr Slouslou na Mtama wote wapo sahihi.Kosa moja wanakidhalilisha chama kilichowalea nakuwadhamini wawe viongozi.
Ikiwa wahuni walikuwepo wakathibitiwa kwa mujibu wa PGO ya chama basi hata waliobaki kama kweli wahuni sio kazi ya Polepole kuwaita wahuni.
Ofisi ina mwenezi mpya,kama mafaili yanaonyesha kuna wahuni basi Nape awezajibiwa.
Nje ya hapo mhuni No 1 ni Polepole.
 
Jana kwenye MAHOJIANO NA kipindi cha msumari wa Moto kinachorushwa na WASAFI TV mheshimiwa Humphrey Polepole kazungumza nje ndani Yani Kwa kizungu ndo kusema Black and White kuhusiana na Hali ya kisiasa nchini Kwa sasa ukilinganisha na awamu iliyopita.

MAHOJIANO hayo yamezua gumzo na mjadala miongoni mwa wananchi huku wengi wakijiuliza Kwa nn Polepole kabadilika ghafla na kuanza kutema cheche tena hata Kwa chama chake ambacho hapo awali alikua katibu mwenezi.

Baadhi ya aliyozungumza Polepole ni kuhusu kutokumalizwa Kwa wahuni wote wakati wa uongozi wa hayati Rais John Pombe Magufuli, kuhusiana na ilo mbunge wa mtama Nape Nnauye ameonekana kuguswa baada ya KUCHAPISHA kwenye ukurasa wake wa Twitter akimdai Polepole atoe orodha ya wahuni hao waliosalia huku akiambatanisha na emoji za kucheka Jambo ambalo wapwa kama wanavyojiita watu wa Twitter wamedai kuwa ni kebehi Tu ambazo Nape anamuonyesha mstaafu mwenzake kwnye cheo cha katibu uenezi CCM.

Polepole KAUPIGA mwingi Sana na waliotazama MAHOJIANO hayo watakubaliana na mm kwani alikuwa na majibu ya uhakika, yenye uwazi na aliyoyatoa Kwa kujiamini hasa alipozungumzia swala la Rais Samia Suluhu Hassan kufanya mazungumzo na waziri mkuu wa zamani wa uingereza bwana Tony Blair ambaye Polepole amemtambulisha kama mtu hatari.

Aidha Polepole huko Instagram katuma video akieleza kwamba kuna baadhi ya watu wameanza kumtafuta na kuanza kumlaumu kutokana na aliyoyazungumza katika MAHOJIANO hayo.

Polepole amekua na msimamo kwenye kile anachokiamini na kufundisha kupitia kwenye mafunzo yake anayotoa mtandaoni ya shule ya uongozi.

Sasa ni wakati wa wanasiasa kuwa na msimamo kwenye falsafa zao na wasiyumbishwe na uchu wa madaraka na uwoga wa wenye mamlaka kwamba nikisema nitachukuliwaje. Na Kwa misimamo yake Polepole, naomba kusema kuwa anaupiga mwingi Sana apewe balon d'Or yake.

Misimamo yake isiyoyumba juu ya katiba mpya iliishiaga wapi?
 
Wasafi hawajawahi kuwa na kipindi hiki cha msumari wa moto.
 
Back
Top Bottom