Kwenye mahojiano na Wasafi TV, Polepole kaupiga mwingi

Pole Pole mpaka 2014 alikuwa ana msimamo kuwa, Katiba mpya ni jambo la lazima, CCM ni chama kilichopaswa kuondolewa madarakani siku nyingi sana.
Vipi bado ana msimamo huo?
Maendeleo hayaletwi na chama cha siasa Jambo la msingi na muhimu ni ushirikiano wa wananchi na serikali Yao China wangeangalia mambo ya vyama wasingefika hatua waliyopo leo
 
Jana kwenye MAHOJIANO NA kipindi cha msumari wa Moto kinachorushwa na WASAFI TV mheshimiwa Humphrey Polepole kazungumza nje ndani Yani Kwa kizungu ndo kusema Black and White kuhusiana na Hali ya kisiasa nchini Kwa sasa ukilinganisha na awamu iliyopita.

MAHOJIANO hayo yamezua gumzo na mjadala miongoni mwa wananchi huku wengi wakijiuliza Kwa nn Polepole kabadilika ghafla na kuanza kutema cheche tena hata Kwa chama chake ambacho hapo awali alikua katibu mwenezi.

Baadhi ya aliyozungumza Polepole ni kuhusu kutokumalizwa Kwa wahuni wote wakati wa uongozi wa hayati Rais John Pombe Magufuli, kuhusiana na ilo mbunge wa mtama Nape Nnauye ameonekana kuguswa baada ya KUCHAPISHA kwenye ukurasa wake wa Twitter akimdai Polepole atoe orodha ya wahuni hao waliosalia huku akiambatanisha na emoji za kucheka Jambo ambalo wapwa kama wanavyojiita watu wa Twitter wamedai kuwa ni kebehi Tu ambazo Nape anamuonyesha mstaafu mwenzake kwnye cheo cha katibu uenezi CCM.

Polepole KAUPIGA mwingi Sana na waliotazama MAHOJIANO hayo watakubaliana na mm kwani alikuwa na majibu ya uhakika, yenye uwazi na aliyoyatoa Kwa kujiamini hasa alipozungumzia swala la Rais Samia Suluhu Hassan kufanya mazungumzo na waziri mkuu wa zamani wa uingereza bwana Tony Blair ambaye Polepole amemtambulisha kama mtu hatari.

Aidha Polepole huko Instagram katuma video akieleza kwamba kuna baadhi ya watu wameanza kumtafuta na kuanza kumlaumu kutokana na aliyoyazungumza katika MAHOJIANO hayo.

Polepole amekua na msimamo kwnye kile anachokiamini na kufundisha kupitia kwnye mafunzo yake anayotoa mtandaoni ya shule ya uongozi.

Sasa ni wakati wa wanasiasa kuwa na msimamo kwenye falsafa zao na wasiyumbishwe na uchu wa madaraka na uwoga wa wenye mamlaka kwamba nikisema nitachukuliwaje. Na Kwa misimamo yake Polepole, naomba kusema kuwa anaupiga mwingi Sana apewe balon d'Or yake.View attachment 2025467View attachment 2025468View attachment 2025469
kuna siku na yeye watu watamwona mhuni na watatafuta kummaliza.
 
Kwa hiyo CCM na serikali yake ni genge lililojaa wahuni?
Sio CCM Bali nchi Kwa ujumla kuna wafanya biashara, waajiriwa, wanasiasa, na wengine wengi ni wahuni huu uhuni anaozungumzia Polepole ni broad term inabidi uwe top notch kumuelewa
 
Pole Pole mpaka 2014 alikuwa ana msimamo kuwa, Katiba mpya ni jambo la lazima, CCM ni chama kilichopaswa kuondolewa madarakani siku nyingi sana.
Vipi bado ana msimamo huo?
Anakwenda na upepo wa kisurisuri ili ajaze tumbo lake
 
Back
Top Bottom