Kwenye mahojiano na Wasafi TV, Polepole kaupiga mwingi

Joel Kisoka

Member
Dec 21, 2018
23
31
Jana kwenye MAHOJIANO NA kipindi cha msumari wa Moto kinachorushwa na WASAFI TV mheshimiwa Humphrey Polepole kazungumza nje ndani Yani Kwa kizungu ndo kusema Black and White kuhusiana na Hali ya kisiasa nchini Kwa sasa ukilinganisha na awamu iliyopita.

MAHOJIANO hayo yamezua gumzo na mjadala miongoni mwa wananchi huku wengi wakijiuliza Kwa nn Polepole kabadilika ghafla na kuanza kutema cheche tena hata Kwa chama chake ambacho hapo awali alikua katibu mwenezi.

Baadhi ya aliyozungumza Polepole ni kuhusu kutokumalizwa Kwa wahuni wote wakati wa uongozi wa hayati Rais John Pombe Magufuli, kuhusiana na ilo mbunge wa mtama Nape Nnauye ameonekana kuguswa baada ya KUCHAPISHA kwenye ukurasa wake wa Twitter akimdai Polepole atoe orodha ya wahuni hao waliosalia huku akiambatanisha na emoji za kucheka Jambo ambalo wapwa kama wanavyojiita watu wa Twitter wamedai kuwa ni kebehi Tu ambazo Nape anamuonyesha mstaafu mwenzake kwnye cheo cha katibu uenezi CCM.

Polepole KAUPIGA mwingi Sana na waliotazama MAHOJIANO hayo watakubaliana na mm kwani alikuwa na majibu ya uhakika, yenye uwazi na aliyoyatoa Kwa kujiamini hasa alipozungumzia swala la Rais Samia Suluhu Hassan kufanya mazungumzo na waziri mkuu wa zamani wa uingereza bwana Tony Blair ambaye Polepole amemtambulisha kama mtu hatari.

Aidha Polepole huko Instagram katuma video akieleza kwamba kuna baadhi ya watu wameanza kumtafuta na kuanza kumlaumu kutokana na aliyoyazungumza katika MAHOJIANO hayo.

Polepole amekua na msimamo kwenye kile anachokiamini na kufundisha kupitia kwenye mafunzo yake anayotoa mtandaoni ya shule ya uongozi.

Sasa ni wakati wa wanasiasa kuwa na msimamo kwenye falsafa zao na wasiyumbishwe na uchu wa madaraka na uwoga wa wenye mamlaka kwamba nikisema nitachukuliwaje. Na Kwa misimamo yake Polepole, naomba kusema kuwa anaupiga mwingi Sana apewe balon d'Or yake.


20211127_211500.jpg
 
Wanasiasa hawaaminiki, wanapokuwa nje ya system wanakuwa pamoja na wananchi wakitupiwa mfupa wanawasaliti wananchi, ni Polepole huyuhuyu kipindi cha mchakato wa katiba mpya,alikuwa pamoja na wananchi alipotupiwa mfupa akageuka fisi wa kuwatafuna wananchi walewale aliokuwanao katika mchakato wa katiba mpya.

Hata huku kuupiga mwingi siyo bure kuna mahari atakuwa kabanwa hivyo hana namna zaidi ya kujifanya kuupiga mwingi.
 
Wanasiasa hawaaminiki,wanapokuwa nje ya system wanakuwa pamoja na wananchi wakitupiwa mfupa wanawasaliti wananchi, ni Polepole huyuhuyu kipindi cha mchakato wa katiba mpya,alikuwa pamoja na wananchi alipotupiwa mfupa akageuka fisi wa kuwatafuna wananchi walewale aliokuwanao katika mchakato wa katiba mpya.

Hata huku kuupiga mwingi siyo bure kuna mahari atakuwa kabanwa hivyo hana namna zaidi ya kujifanya kuupiga mwingi.
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom