kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,428
- 13,935
Kikulacho kinguoni mwako, kinachotula na kuturonga watanzania tusizunguuke kiko nguoni mwetu. Alichokifanya Rais Magufuli ni kuwaonyesha tu watanzania kitulacho na kuturoga. Lakini kutuonyesha peke yake hakutoshi kama hatutakichukulia kitulacho hatua kali na za wazi.
Mimi napendekeza yafuatayo kwa kitulacho na kiturogacho:
1. Kumpongeza Rais Magufuli na kumpa "zawadi maalum" ya kuliongeza taifa kwa miaka 15 mfululizo kama mwenyewe atakubali na sisi tutakubali ili aweze kukamilisha baadhi vitu ambavyo vilishindikana au vilikwenda hovyo kwenye awamu za 1,2,3 na 4. Huyu sio Rais wa miaka 5 au 10 tu kama wengine waliopita na kutuingiza hasara zote hizi. Umeona wapi twiga anaingizwa kwenye ndege na kuondoka bila hata vyombo vyooote vya ulinzi na usalama wa nchi kukohoa.
2. Kutambua vitulavyo na viturogavyo vyooooote na njia walizotumia na kiasi walichotutafuna na kuturoga.
3. Tutaifishe mali zoote (ndani na nje ya nchi) za vitulavyo na viturogavyo bila huruma hata chembe.
4. Tuwape adhabu kali sana kitulacho na kiturogacho kwa mujibu wa sheria.
5. Tuandike katiba mpya itakayoakisi safari ya taifa letu huko mbele ya safari ndani ya utandawazi
6. Tuziangalie sheria zetu zoooote ili kuzikarabati. Kitulacho na kiturogacho walishirikiana na wakoloni mamboleo kutunga sheria chafu kwetu kwa makusudi. Sasa hivi tukiwahoji wanadai "tulifuata sheria zenu kikamilifu" ambazo waliagiza na kushinikiza namna kuzitunga na kuzipitisha. Mara nyingi zilipitizwa kwa njia ya "Kimangungo" ya ndiyoooooooooooooo kule bungeni.
7. Mikataba yote ya uwekezaji nchini isimame kwanza ili ipitiwe yoooote ili kutafuta vitulavyo kwenye mikataba hiyo.
Haya ni maoni yangu tu mimi kavulata, msinisonye.