Mahweso
JF-Expert Member
- Jan 10, 2014
- 1,098
- 1,501
Hivi mnaona Watanzania ni walewale wa kudanganywa? Leo mnalaumu Chadema kutetea wezi, Hawa Chadema walipokuwa wanapiga kelele kuhusu Sheria Mbovu na Mikataba mibovu si mliwaona tena wanakwamisha maendeleo ya Nchi?
Haya mlisaini Mikataba haraharaka tena kwa Siri, Chadema hawakusani Mikataba na Wala hawakupitisha Sheria, CCM walipitisha Sheria mbovu na Serikali ikasani Mikataba mibovu , haya Chadema kosa lao kusema fuateni Sheria mlizozitunga wenyewe?
Sheria mlizitunga wenyewe kwanini hamtaki kuzifuata? ACACIA wanasema wanafanya kazi kwa mujibu wa Sheria za Tanzania na Mikataba yao inawaruhusu kusafirisha Mchanga, Nakumbuka wapinzania walipiga sana kelele oooooo mnatuachia mashimo wajukuu zetu watakuja kutuuliza, CCM wakasema wapinzania wanapinga maendeleo.
Huu mzigo ni wenu CCM, matakataka yote mliyaleta nyinyi, msimtafute wa kumtwisha zigo lenu, bebeni wenyewe,
Utafungaje ndoa, harafu baada ya ndoa ndio uanze kusema oooo mwanamke Mzee nisaidieni nimwache, kwani hukumwona kabla kabla ya kuoa? na uliambia mbona unaoa mzee ulijibu nimempenda usinipangie, Zigo lenu hili .