Logikos
JF-Expert Member
- Feb 26, 2014
- 12,448
- 19,472
Duh Afya yake tena ? Sasa hapo nani analeta upotoshaji ?Tuache upotoshaji wa makusudi na kujenga fitna. Wote tunafahamu ni haki yake Mhe.Jakaya Kikwete kuvaa barakoa nk, kunakochagizwa na mazingira ya umri na afya yake !
Nalaani siasa chafu kwa jamii kwa kutumia matukio kama haya. Na kila anayeshadidia na kuanzisha upoteshaji kupitia misiba ,atanguliye mbele za haki upesi.
Pia kumbuka anayevaa Barakoa sio kwamba anaogopa asiambukizwe au hawezi kuambizwa bali ni kwamba anajali kutokuwaambukiza wengine..., (Sio kwamba yeye anao la hasha ila huwezi kujua huenda ametoka kuupata siku chache na hajui, kama mimi na wewe ambavyo hatujui ukizingatia vipimo havipo wazi)
Kwahio mara nyingine anayevaa Barakoa jua kwamba anajali kupunguza maambukizi kwa watu wengine... Wote wakivaa itapunguza maambukizi ambayo watu wakiwa hawana chochote ni rahisi kuambukizana..
Anyway kuvaa kwake Barakoa kunaweza kutafsiriwa kwamba he cares na wengine waliokuwa wanaona aibu wataonekana wa ajabu wasiogope kuvaa
Hususan baada ya Kiongozi mkuu anavyoonekana akitoa pongezi kwa wale wasiovaa