Kwenye koo langu kuna kitu nakisikia kama kimekwama sasa nashindwa kuelewa ni kitu gani

shujaa bangili

New Member
Sep 4, 2019
4
3
Nahitaji msaada na ushauri wenu wa dhati WAKUU,kuna kitu huwa kinanisumbua Sana sielewi tatizo NI nini.kwenye Koo LANGU KUNA kitu nakisikia Kama kimekwama Sasa nashindwa kuelewa NI kitu gani maana nikiwa nakula sikisikii Wala nikinywa maji sikisikii Bali nikiwa nameza mate ndiyo huwa nakisikia ama ikitokea nimemeza kidonge Cha aina yoyote Ile basi Siku ya pili yake au BAADA ya masaa kadhaa Hali iyo huwa inaongezeka kuliko awali ninachokishangaa KUNA kipindi HIYO Hali huwa inatoweka KABISA ila BAADA ya wiki au Siku kadhaa Ina Rudi Tena NAOMBA msaada wenu wa kitabibu WAKUU.
 
Mkuu nenda hosipitali ya rufaa ukakutane na wataalamu wa kitengo cha macho, masikio na koo. Tatizo lako litafahamika dhahiri na litakwisha.

Asitokee mtu akakupotosha na tiba za kienyeji ama tiba mbadala. Wahi hospitali, haujachelewa mkuu.
 
Siamini kama nakutana na hii kwako, my wife alikuwa na tatizo hilo ,sisi watu wa IMANI ya maombezi tulivyotoka kanisani jpili mwenzangu kufika home akapiga chafya na kutoa kitu cheupe kina harufu hatukujua ni nini tulishukuru Mungu ila sasa sijui nikushauri nini???
 
siamini kama nakutana na hii kwako, my wife alikuwa na tatizo hilo ,sisi watu wa IMANI ya maombezi tulivyotoka kanisani jpili mwenzangu kufika home akapiga chafya na kutoa kitu cheupe kina harufu hatukujua ni nini tulishukuru Mungu ila sasa sijui nikushauri nini???
Nashuru mkuu
 
Mkuu nenda hosipitali ya rufaa ukakutane na wataalamu wa kitengo cha macho, masikio na koo. Tatizo lako litafahamika dhahiri na litakwisha.

Asitokee mtu akakupotosha na tiba za kienyeji ama tiba mbadala. Wahi hospitali, haujachelewa mkuu.
Umenipa mwanga nashukuru mkuu pia Kama UNAFAHAMU jina la ugonjwa nijuze.
 
Kabla ya kuhangaika kutafuta tiba kubwa je unaelewa nini kuhusu Tonsils??
Watu wengi huwa hawaelewi kuhusu tonsils.
Kuna wengine wakiwa na tonsils hufanya uvimbe ambao huwa nkama vifuko ambavyo vyakula vikiingia hugandiana humo na kusababisha vyakula hivyo kuoza na kutengeneza kitu kama Mtindi ulioganda kabisa ambao husababisha harufu mbaya ya kinywa. Ambapo pia mtu huyu akimeza mate ndio huhisi kama kuna kitu kimekwama kooni. Kikawaida huwa hakuna kitu kilichokwama kooni bali ni kutokana na uvimbe (tonsils) huwa ndio ubakaba kooni...Kamuone daktari wa magonjwa ya koo, akutoe hizo taka ambazo huwa zimeganda kwenye tonsils, ukitoka hapo hautahisi tena kitu kukwama kooni.
 
Umemaliza kila kitu, sidhani kama huyu Bwana aliyeleta huu uzi anahitaji zaidi ya hapa. Umeweka kila kitu bayana; ugonjwa na nini anatakiwa afanye (kwenda hospitali kumuona daktari wa magonjwa ya masikio, pua na koo, wanafahamika kama Ear, Nose & Throat simply ENT-Specialists). Hata mdau aliyesema hapo juu kuhusu mkewe kupiga chafya na kutoa kitu cheupe amekuwa muwazi kwa kusema "hajua ashauri nini". Ukweli halisi ni huu ulioandika.
 
Nahitaji msaada na ushauri wenu wa dhati WAKUU,kuna kitu huwa kinanisumbua Sana sielewi tatizo NI nini.kwenye Koo LANGU KUNA kitu nakisikia Kama kimekwama Sasa nashindwa kuelewa NI kitu gani maana nikiwa nakula sikisikii Wala nikinywa maji sikisikii Bali nikiwa nameza mate ndiyo huwa nakisikia ama ikitokea nimemeza kidonge Cha aina yoyote Ile basi Siku ya pili yake au BAADA ya masaa kadhaa Hali iyo huwa inaongezeka kuliko awali ninachokishangaa KUNA kipindi HIYO Hali huwa inatoweka KABISA ila BAADA ya wiki au Siku kadhaa Ina Rudi Tena NAOMBA msaada wenu wa kitabibu WAKUU.
Hiyo ni hali inayosababishwa na vumbi mkuu yaan umevuta vumbi jingi ndan ya mwil.

Epuka kulala na kukaa sehemu zenye vumbi .
 
Hiyo hali inakutokea baada ya kula!...koo linakuwa kavu kama limekauka ? Je unapata maumivu ya kifua? Unapata maumivu ya tumbo?... Kifua kinawaka moto?..

Nina uhakika ila tatizo lako ni acid kujaa tumboni
 
Mkuu, habari? Hiyo hali inaitaa Globus Pharyngeus. Ni hali ya kuhisi una kitu kooni laki kiuhalisia kitu hiko hakipo na mtu hupata ahueni akila ama kunywa kitu lakini yaweza kukaa kidogo na kurudi tena. Sifa kubwa ya hali hii ni kwamba hupati shida kwenye kumeza wala kunywa.

Hukera kwakweli na haina tiba ya mojamoja. Hali hiyo huweza sababishwa na vitu vifuatavyo,

1. Acid reflux - hii huambatana na muwasho wa koo na hata maumivu kifuani. Hali hii husababishwa na kiasi kingi cha Acid tumboni ambacho hujirejesha kooni kutoka tumboni na kusababisha hali hiyo kwenye mlango wa koo.

Dawa yake ni kupunguza intake ya acidic foods na hata pia kutake anti-acids. Pia kutafuna big g itasaidia kwenye acid digestions, vilevile ukitumia maji yalochanganywa na baking soda.

2. Huweza sababishwa na matumizi makubwa ya koo kama vile kupaza sauti ama kuongea kwa muda muda mrefu. Kitaalamu huitwa Laryngitis.

3. Mfadhaiko, woga ama msongo. Kuna watu wakiwa kwenye hofu ama msongo hali ya koo kuuma hutokea.

Nakutakia kupona kwema.
 
Nahitaji msaada na ushauri wenu wa dhati WAKUU,kuna kitu huwa kinanisumbua Sana sielewi tatizo NI nini.kwenye Koo LANGU KUNA kitu nakisikia Kama kimekwama Sasa nashindwa kuelewa NI kitu gani maana nikiwa nakula sikisikii Wala nikinywa maji sikisikii Bali nikiwa nameza mate ndiyo huwa nakisikia ama ikitokea nimemeza kidonge Cha aina yoyote Ile basi Siku ya pili yake au BAADA ya masaa kadhaa Hali iyo huwa inaongezeka kuliko awali ninachokishangaa KUNA kipindi HIYO Hali huwa inatoweka KABISA ila BAADA ya wiki au Siku kadhaa Ina Rudi Tena NAOMBA msaada wenu wa kitabibu WAKUU.
Mkuu kama hujapata tiba mpaka sasa na upo Dar ni PM nikuelekeze sehemu ukanujue dawa. Kuna mtu alikua na tatizo hilohilo miezi kadhaa nyuma na alipona fasta tu.
 
Nahitaji msaada na ushauri wenu wa dhati WAKUU,kuna kitu huwa kinanisumbua Sana sielewi tatizo NI nini.kwenye Koo LANGU KUNA kitu nakisikia Kama kimekwama Sasa nashindwa kuelewa NI kitu gani maana nikiwa nakula sikisikii Wala nikinywa maji sikisikii Bali nikiwa nameza mate ndiyo huwa nakisikia ama ikitokea nimemeza kidonge Cha aina yoyote Ile basi Siku ya pili yake au BAADA ya masaa kadhaa Hali iyo huwa inaongezeka kuliko awali ninachokishangaa KUNA kipindi HIYO Hali huwa inatoweka KABISA ila BAADA ya wiki au Siku kadhaa Ina Rudi Tena NAOMBA msaada wenu wa kitabibu WAKUU.
Nunua jeneza tu, mkuu...

Nakutania muone dk.
 
Kabla ya kuhangaika kutafuta tiba kubwa je unaelewa nini kuhusu Tonsils??
...Kamuone daktari wa magonjwa ya koo, akutoe hizo taka ambazo huwa zimeganda kwenye tonsils, ukitoka hapo hautahisi tena kitu kukwama kooni.
Hiyo procedure inaweza kugharimu kiasi gani roughly? Na huduma hiyo inaweza patikana hospitali za mikoani? Ninahisi kuwa na tatizo kama hilo.
 
Kama sikosei check up ni 15,000 tu hadi 30,000. Ila pia unaweza kujichunguza mwenyewe. Je ukikohoa unahisi kama kitu kimekwama kooni? Jaribu pia kumtumia mtu akucheki kwenye Tonsils hakuna kitu kama taka, kwa macho ya kawaida pia anaweza kutizama na kuona. Cha kufanya, tanua kinywa, toa ulimi nje then fanya kama unavuta hewa ndani muda huo yeye anakutazama kinywani, kwenye tonsils anaweza kuona huo uchafu unaorundikana kama umo.
 
Na kama akiona huo uchafu nini kifanyike doctor ? Je anaweza kuutoa kwa kidole au mpaka hospital..
Na kingine kwa hao ambao wanakohoa au kupiga chafya ndio kinatoka wana haja ya kuja hospital tena..
Hata mimi nahisi kama nna hiyo kitu..
Ni kweli kwa mwenye hicho kitu anakua na tatizo la kunuka mdomo ?
Manaake unaweza kuwa unanuka mdomo bila wewe kujijua
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom