Kwenye kila watu 8, mmoja ana tatizo la Afya ya Akili Tanzania

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,365
8,097
1664868729486.png

Sababu inayochangia hali hiyo ni mabadiliko katika Malezi, Msongo wa Mawazo wa Kushindwa Kuhimili Changamoto, Ongezeko la Magonjwa yasiyoambukiza na Matumizi ya Vilevi hususan Pombe, Bangi na Dawa nyingine za Kulevya.

Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam, Rehema Madenge aliyemwakilisha Waziri wa TAMISEMI katika Wiki ya Afya ya Akili, amesema mtu mmoja katika kila watu 8 ana tatizo la Afya ya Akili, wakati awali ilikuwa mtu mmoja katika kila watu 10.

Amesema wanawake wanne kati ya 10 wenye umri kuanzia miaka 15 hadi 45 wamefanyiwa ukatili wa kimwili huku wanawake wawili kati ya 10 ikiwa ni ukatili wa kingono na wote wanaelekea kupata tatizo la Afya ya Akili.
---

Mtu mmoja katika kila watu nane imeelezwa kuwa hivi sasa ana tatizo la ugonjwa wa afya ya akili, wakati awali ilikuwa mtu mmoja katika kila watu 10.

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), katika mwongo mmoja uliopita, kumekuwa na ongezeko la watu kwa asilimia 13, ambapo watu bilioni 1 wanaishi na tatizo hilo duniani.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, wakati wa uzinduzi wa maonesho ya Wiki ya Afya ya Akili, Mwakilishi wa Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali ya Mitaa (TAMISEMI), ambaye ni Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam, Rehema Madenge amesema Tanzania inakadiriwa kuwa wa wagonjwa milioni 7 wenye matatizo hayo na wengi wao wanaishi na sonona.

“Sambamba na ongezeko la ugonjwa wa akili, lakini pia kumekuwa na matukio ya kikatili ambapo wanawake wanne kati ya 10 wenye umri kuanzia miaka 15 hadi 45 wamefanyiwa ukatili wa kimwili.

“Pia wanawake wawili kati ya 10 wamefanyiwa ukatili wa Kingono na hao wote baada ya kufanyiwa ukatili huu wanaelekea kwenye tatizo la afya ya akili,” amesema.

Madenge ameeleza kuwa sababu kubwa ya magonjwa ya akili na ukatili ni mabadiliko katika mfumo wa malezi ya familia, msongo wa mawazo wa kushindwa kuhimili changamoto, ongezeko la magonjwa yasiyoambukiza na matumizi ya vilevi hususan pombe, bangi na dawa zingine za kulevya.

Habari LEO
 
da!! kumbe kumwagilia moyo kuna leta matatizo ya akili!!!...basi mimi nshakua chizi!!
 
Back
Top Bottom