G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,555
- 35,880
Uthibitisho wa kupungua kwa Corona nchini ni lazima utolewe kwa kupewa scientific data kitu ambacho si Rais wala waziri wa afya wanacho. Wanatoa tu maoni yao kwa kutumia hisia jambo ambalo kwa kiongozi mwenye vyombo kufanya ni ukosefu wa maarifa.
Ukiwasikiliza mawaziri mfano Kabudi ni kama unaona kabisa hawaelewi chochote kuhusu mwenendo wa janga hili. Ni kama wako gizani wanapapasa. Aidha ukimsikiliza waziri wa afya Ummy Mwalimu halafu ukamsikiliza Rais Magufuli hasa hapa "Ukiwa vitani hakuna kubembelezana" unaona kabisa waziri Ummy alikuwa anashurutishwa kufanya mambo ambayo yapo nje ya taratibu.
Sasa basi, kwa kuwa hawana data zozote kuthibitisha kile wanachokinena, majukumu yote ya kupambana na janga hili ameachiwa Mwananchi huku huyo mwananchi akihakikisha kuwa Magufuli anapata stahiki zake za kodi kama kawaida.
Kwa Magufuli maneno "Uchumi kwanza" ni yakuchukuliwa kwa tahadhari kubwa sana na hasa akitazamwa mwenendo wake dhidi ya utu wa binadamu! Kwake yeye ni "Hakikisha unaleta mapato" haijalishi uko katika hali gani na unapambana na nini.
Niseme, kiongozi yeyote aliye na uwezo wa kiuongozi hawezi kuja hadharani kwa staili ya Magufuli. Haya ni mapungufu makubwa kwa kiongozi kuja na jambo linalohitaji ulinganifu wa kisayansi kisha ukaja staili kama ya Magufuli isiyo na takwimu yoyote ile kuthibitisha kile anachonena. Sisi wanansayansi hizo tunaita "Chai" na tunazipuuza mara moja.
Hakuna uthibitisho wowote wa kile anachoeleza Rais Magufuli kuhusiana na janga la Corona hivyo basi chukua tahadhari wewe na jamii yote unayohudumia kama unaipenda. Chukua tahadhari huku ukijua kuwa watanzania wenzetu zaidi ya hao 16 waliotangazwa wamekufa kwa Corona. Wamekufa na hakuna aliyejali baada ya hapo na ndiyo maana tunaambiwa kila kitu kiende kama kawaida.
Ukimtazama Magufuli kwa haya utamfahamu ni mtu wa aina gani.
1. Unakataa vifaa vya msaada vya kupambana na huu ugonjwa kwa kuhofia hujuma huku unaruhusu utalii.
2. Unakataa kutoa takwimu halisi hadharani huku unasema ugonjwa unapungua.
Kwa hayo mawili "Kuwa na akili za mbayuwayu"